JK Kukutana na Wapinzani-Ukurasa Mpya wa Demokrasia!?

Amavubi

JF-Expert Member
Dec 9, 2010
30,140
13,215
Usemi wa mnyonge mnyongeni haki yake mpeni unaendana hapa..twende mbele turudi nyuma lakini ada ya mja hunena uungwana ni vitendo..hii ni positive move ya demokratisation katika Tanzania na huenda tuione kwa jinsi ya fumbo sasa lakini itaingia katika historia ya wengi.............naiona njozi ya Katiba shirikishi ambayo itakidhi matakwa ya wengi kutokana na jinsi utashi wa serikali yetu unavyojitokeza katika hili................(kama mmegundua ni kama Big Bhang, wakati JK anakutana na wanasiasa, Mkulima anakutana na Viongozi wa Dini, sijajua kama wanaharakati watakuwemo But naamini watajumuishwa)

Angalizo langu; isije kuwa ni kiini macho tu au danganya toto.....pamoja na salamu za kumtakia heri katika mchakato mzima na kumpongeza kwa hatua aliyofikia lakini namtaka Rais wangu achukue all the best na kuacha all the rest katika mchakato huu hususam mawazo mazuri ambayo atapewa na wanasiasa wenzake ili tuione na kuithibitisha nia ya dhati aliyokuwa nayo...........vinginevyo tutaona chenga tu!!!!
 
.....Tusubiri tuone/tusikie yatakayojiri kama anataka kufanya kweli kwa maslahi ya nchi au ana lake jambo maana Kikwete ni msanii wa hali ya juu.
 
hATA mImI nInA WaSiWaSi sAnA HuEnDa nI DOMO-KRASIA TU!!!
 
Usemi wa mnyonge mnyongeni haki yake mpeni unaendana hapa..twende mbele turudi nyuma lakini ada ya mja hunena uungwana ni vitendo..hii ni positive move ya demokratisation katika Tanzania na huenda tuione kwa jinsi ya fumbo sasa lakini itaingia katika historia ya wengi.............naiona njozi ya Katiba shirikishi ambayo itakidhi matakwa ya wengi kutokana na jinsi utashi wa serikali yetu unavyojitokeza katika hili................(kama mmegundua ni kama Big Bhang, wakati JK anakutana na wanasiasa, Mkulima anakutana na Viongozi wa Dini, sijajua kama wanaharakati watakuwemo But naamini watajumuishwa)

Angalizo langu; isije kuwa ni kiini macho tu au danganya toto.....pamoja na salamu za kumtakia heri katika mchakato mzima na kumpongeza kwa hatua aliyofikia lakini namtaka Rais wangu achukue all the best na kuacha all the rest katika mchakato huu hususam mawazo mazuri ambayo atapewa na wanasiasa wenzake ili tuione na kuithibitisha nia ya dhati aliyokuwa nayo...........vinginevyo tutaona chenga tu!!!!

mkuu neno upinzani,mpinzani,kipinzani na wapinzani lina utata sana katika kuzungumzia Demokrasia.Naona msamiati huu wa opposition kama ulivyotasfiri moja kwa moja kutoka kwenye Kiingereza unamadhara saana hasa katika nchi zetu hizi.
 
Ukienda kule democrasia ilikoanzia!! huwezi kusikia mpinzani au upinzani!!
 
Kwa wakati fulaNI sisi ambao tukohuku ambako demokrasia inaishia inabidi tulikubali tu kama tunavyokubali misamiati mingine kama vile UTAWALA BORA nk
 
Back
Top Bottom