Jk kukutana na chadema

Kwani jamani kuna mzozo gani ambao unamhitaji raisi kukutana na CDM, na anamsuluhisha suala gani? Mimi ninashauri huyu mkulu atimize majukumu yake kama anaweza, na CDM waendelee na shughuli zao za kisiasa. Wameanza vizuri kutoa elimu ya uraia kwa wananchi suala ambalo ni jukumu la mkulu na serikali yake; lakini kwa kuwa ulikuwa mtaji wa kale ka-chama ka-Mwalimu, kakiwa kamejikita ktk sintofahamu ya wananchi juu wa wajibu wao ktk masuala ya siasa ktk mfumo huu wa vyama vingi. Hakika jasho la meno litawatokeni sana CCM, hali ya uchumi kwa wananchi ni ngumu, Mungu aepushe na balaa la ukame kwani walafi ndani ya ka-chama kenu watataka waendelee kunufaika ili hali wanachi watakuwa wanakufa na njaa - hapa nakumbuka RC mmoja (natumai ni huko Mara) aliwahi kukanusha kuwa wananchi wake hawana njaa na waandishi walipofika huko walikuta watu wameathirika kishenzi.
Serikali kaza buti, acha longo longo
 
Hivi mtu mwenye akili timamu anaweza kusema serikali ya ccm ipewe mda zaidi??? Tuchukue mfano rahisi tu, wakati wamjadala wa richmond Bungeni Bunge lilitoa maazimio juu ya hatua za serikali kuchukua. Hebu tuambieni imechuka hatua gani au mnahitaji mda gani kutekeleza maazimio yale ya Bunge?!
 
Ndoto ya madaraka. JK hana sababu ya kukutana na cdm. Kwa kipi hasa,wachochee watu kufanya uasi halafu watake mazungumzo na Rais.Hawana jipya waendelee na maandamano mazungumzo ya nini. Na wao wanataka kuingia serikalini kama cuf.Waendelee kupost thread humu JF

Inaonekana CDM wanaku-bore sana! Unajua, tatizo la msingi si CDM bali utendaji wa JK na serikali yake. Matatizo ya nchi hii hayawezi kuisha kama members wote wa CC-Mafisadi wataendelea kuamini kwamba kila anayewakosoa ni kwa sababu anawaonea wivu au anataka kuingia madarakani kwa nguvu.
Hata wanachi wakiwang'oa kwa maandamano si CDM watakaochukua uongozi wa nchi kwa kuwa lengo lao si kuchukua madadraka kwa staili hiyo.
 
Mkutano wa CDM na Rais hautakuwa na tija kama matatizo ya wananchi hayatatuliwa. Wao kama viongozi wanaweza kukubaliana lakini sisi wananchi tunahitaji maendeleo siyo makubalianao yao
 
Rais anataka kutimiza utabiri wa kishirikina wa mlinzi wake wa majini, Sheikh Yahya? Kutafuta kukutana na Chadema bila kupambana na ufisadi kwanza ni kutapatapa! Hiyo ni danganya toto kwa vile ameona maji yako shingoni kwani hapo tulipofikia, hata taahira anahisi kuwa upepo sio mzuri! Kuna kila dalili kwamba moto waweza kulipuka wakati wowote.

Hata Sheikh Yahya anajua hivyo, kwamba pamoja na ushirikina, sasa watanzania wako standby, na wako tayari kwa lolote. Harakati za kutaka kukutana na Chadema tu, bila kujibu kwanza tuhuma za Chadema kuhusu ufisadi na umaskini wa watanzania, ni ufukunyuku! Na mikakati yenyewe haina tija kwa vile ni mikakati ya kishirikina!
 
Heshima mbele Mkuu MMKJJ: Mimi nadhani CDM wakatae kabisa kukutana na JK au CCM. Kwa vile wazo hilo la Baraza la demokrasia limedakwa mara moja na Tendwa nadhani hii ni project ya CCM yenyewe -- ya kujitafutia life-line ya kutokea, maana sasa hivi imezidiwa mno na hoja za CDM. CCM wanatafuta ahueni kidogo -- mahala pa kupumzikia -- yaani respite maana chama hicho kimekuwa kinaendeshwa puta kwa kasi sana.

Hoja ya CCM kwamba CDM wanataka kuleta macahfuko haina nguvu sana hasa pale CCM wanashindwa, wanapotakiwa kutoa maelezo ni matamshi gani -- tena kwa nukuu husika -- ambayo viongozi wa CDM wamenena majukwaani yanayoweza kuhatarisha amani.
Mkuu mapendekezo yako mali, CDM wawateme wasiwape pumzi kwa sasa, hapa wanatapatapa hawajapata njia ya kutokea. Waendelee na mbinyo ili kitu kieleweke. Wajibu hoja kwenye majukwaa, kama hawatapigwa mawe na watu wenye usongo na nchi yao????????????
 
Ndoto ya madaraka. JK hana sababu ya kukutana na cdm. Kwa kipi hasa,wachochee watu kufanya uasi halafu watake mazungumzo na Rais.Hawana jipya waendelee na maandamano mazungumzo ya nini. Na wao wanataka kuingia serikalini kama cuf.Waendelee kupost thread humu JF
Uchochez gan ulofanywa na CDM? Uvunjifu wa aman utasababishwa na madudu ya ccm. Afu cdm kukutana na jk ili iweje? Wakati ujumbe wote anao? Jk ajibu hoja za cdm ambalo haimlazim kukutana nao kama cdm walivolianzisha bila kumuita jk na ujumbe ulimfikia na reaction yake ndo hiyo ambayo imo ndani ya uwezo wake.
 
Back
Top Bottom