Jk kukutana na chadema

Watakuwa wanajidanganya sana kama watakutana na Chadema kwa kudhani hili ni tatizo la Chadema, mimi nawashauri waanze na kina Mgaya wa TUCTA kwanza waelewane na waongeze mshahara stahiki ( sababu nina ushahidi wa kutosha kwamba pesa hizo zipo na nchi yetu ni tajiri ).
2. wakutane na vyama vya wamachinga wajue matatizo yao halisi na sio kuwajengea machinga complex
3. wahakikishe wote wanaowasababishia maisha magumu Watanzania wanashughulikiwa mara moja bila kuacha chembe ya shaka.
4. Lianzishwe jukwaa huru la vijana wasio na hajira ( na sio vijana watoto wa vigogo) hapo pawe ni chumbiko la mijadala ya kupunguza ukosefu wa ajira kwa vijana.
Zipo sababu nyingi nimetoa mawazo yangu tu kwa uchache, lakini kama kuna mpuuzi ambaye anadhani tatizo ni CHADEMA anajidanganya, kwangu mimi Chadema naona ni kama starter tu ya kuamsha hasira za watu waliokata tamaa ya maisha na hambao hawana cha kupoteza, maana duniani hawapo na peponi hawapo, je watu hawa wako wapi? mtu anaota ndoto amekufa kwa wiki mara tatu unadhani mtu mwenye maisha bora huwa anaota ndoto za kufakufa?
 
hayo maandamano yamepunguza makali ya maisha? Wahimize wananchi kufanya kazi. Mbona hawaelezi serikali nini cha kufanya maisha yawe bora.Baada ya maandamano na mikutano huko mwz,bukoba,mara,shy, je maisha yamebadilika? Huu si muda wa kampeni,waacheni wananchi wafanye shughuli zao.Slaa anakipeleka vibaya chama watu washamchoka kila siku kasema hili mara lile,utekelezaji zero.

inaonekana wewe ni mtu wa mwisho ktk dunia hii kwa kuwa na akili ndogo..sijui nikutukane K.. wewe,inamana hauoni kabisa jinsi watanzania tunavyoteseka,kule msumbiji waliandamana kupinga ongezeko la bei ya mkate tu,sasa sisi vingapi vina bei juu mishahara haipandi wenyewe tu ndio wanajiongezea.hata vyuo vikuu boom eti wanaambiwa hazina hamna ela,hakika wananchi wamefunguka na ndio maana wanajitokeza kwa wing kwenye maandamano ya chadema bila kulazimishwa.chadema hakisitisha maandamano wananchi tutajikusanya 2anamane mpaka kieleweke.
 
Dos Santos! usilete propaganda katika ishu serious kama hii waache CDM waandamane ni haki yao kikatiba na unavyofikiria wewe kuhusu uchu wa madaraka uko wrong, na elewa kwamba JK sasa yuko katika hali tete alifikiri kuongoza inchi ni mchezo sasa ameona ikulu sio sehemu ya masikhara na hii yote ni kutokana na presha anayoipata kutoka CDM, na elewa kwamba kazi kuu ya upinzani ni kuikosoa serikali sio kujipendekeza pendekeza kama wale wenzetu wa vyama vingine.

nakukumbusha: siku ya hotuba ya JK mwisho wa mwezi Februari. alisema haya kuhusu tatizo la umeme nchini, Tarehe 15 Februari, 2011, Baraza la Mawaziri lilijadili na kuidhinisha mpango wa dharura wa TANESCO wa kukodi mitambo ya kuzalisha MW 260 za umeme. Baraza limeitaka Bodi na Menejimenti ya TANESCO kuhakikisha kuwa mchakato huo unakamilika mapema iwezekanavyo ili kupunguza makali na athari za ukosefu mkubwa wa umeme kwa jamii na uchumi wa nchi. Aidha, imesisitizwa kuwa pamoja na udharura uliokuwepo sheria na taratibu za manunuzi ya umma vizingatiwe. Pia, wahakikishe kuwa mkataba wataoingia uwe ni wenye maslahi kwa taifa. Vile vile, watoa huduma wawe ni makampuni yanayofahamika na yenye sifa stahiki na kuaminika.

Hapo kwenye red, ina maana siku zote JK alikuwa anaelewa kuwa mikataba ya IPTL,RICHMOND,SONGAS,NET GROUP haikuwa na maslahi kwa wananchi, na hili amelisema baadae ya maandamano ya CHADEMA kanda ya ziwa, sassa mimi nakushangaa sana unaposema CDM wanapoaandamana wanaleta uasi na kuonekana wana uchu wa madaraka. Tumia akili yako vizuri sio kuleta upupu usio na maana yoyote na kwa taarifa yako ujinga unaoongea humu JF huwezi kuongea mtaaani nadhani utachomwa moto aua utapokea matusi na kipigo juu.

SONGAS,IPTL,NETGROUP,kawaulize wenzio rais alikuwa nani? Tatizo mkumbo. Inaonekana hukusiliza hotuba,umehadithiwa au umeamua kupotosha kama ilivyo kawaida yenu
 
maisha magumu mpaka watu waambiwe ni magumu? Kwani watu hawayaoni? Mbona Rais JK ktk hotuba yake amekiri kwamba maisha ni magumu.CDM wakiwahutubia watu maisha ni magumu ndo yanabadilika au kuwapotezea watu muda wa kuhangaikia maisha yao yawe mepesi. Maandamano hayana tija kwa mtz,ila ipo ajenda ambayo wewe huijui unafuata mkumbo. Kama hamkueleweka ktk kampeni ndo mtaeleweka sasa

hata kama kuna agenda(mathalani ya kujijenga kisiasa, kuongeza wanachama na kukubalika zaidi) kuna ubaya gani? jei kei anaogopa eti harakati za chadema ni za kuchochea watu waiondoe serikali iliyopo madarakani...sawa kabisa, inawezekana ni kweli, je kama ni kweli cdm wanatumia agenda zipi ku-convince wana wa nchi? hizo agenda wanazotumia ni za kweli/ zina ushahidi? kama ni za uongo cdm wapelekwe court mara moja. la kama ni za kweli, na gvt ya ccm imeshindwa kuzitatua bac ni kweli inatakiwa iondoke(kama wana wa nchi watataka hivo coz hatulazimishwi kuongozwa(kutawaliwa?) na watu tusiowataka. waacheni cdm au hata cuf au kingine chochote waseme wanayosema(mradi wawe na ushahidi nayo) halafu wana wa nch watasort out pumba na mchele na wataamua waunge mkono au la.

vingenevyo watu hawatakubali hiyo stor yenu eti wasubir had 2015. wakishasubiri halafu watajenga chama saa ngapi? hiv hujui Nyerere alijiuzulu U-PM akaingia vijijini kwenda kuimarisha chama? ndo maana mlikuta chama kina nguvu dira na mwelekeo niny mkakfisadisha. cdm huu ndo wakati wa kujenga chama chenu,ingieni hadi vijijini ndani kabisa, tumieni hoja za ufisadi, wizi wa mali ya umma na kutowajibika kwa mafisadi yaliyo serikalini sasa kuamsha wana wa nchi ili wawakubali ninyi(kwa kuwaonesha uwezo wenu) na kuwakataa mafisadi ya tanzania..kama mafisadi mtaamua kutumia nguvu ya risasi dhidi ya nguvu ya umma bac na tumien, tutaona mtaua wangapi. mawazo ya kimapinduzi hayafi, yangekuwa yanakufa leo hii nelson mangdela asingekuwa baba wa taifa la A.kUSINI and politically the most respected personality worldwide.....kifupi ni kwamba haturdi nyuma tena, itakuwa tu kama c leo ni kesho. mafisadi lazima yaondoke. hatuwezi kuongozwa na sofia simba sisi, lipstik atapaka saa ngapi?
 
SONGAS,IPTL,NETGROUP,kawaulize wenzio rais alikuwa nani? Tatizo mkumbo. Inaonekana hukusiliza hotuba,umehadithiwa au umeamua kupotosha kama ilivyo kawaida yenu

Dosantos acha mimi nimpe jibu.....Raisi alikuwa ni wa ccm
 
Do santos unaonekana una mtindio wa ubongo au ni mvivu wa kufikiria,maana ni Mtanzania wa aina gani ambaye hajui kama maisha ni magumu,yaani unadhani kubaki nyumbani kwako na kuganga njaa ni bora kuliko kuunga mkono nguvu ya umma
Viongozi wengi wa kiafrica hasa CCM in Tanzania bila kuambiwa huwa hawasikii sasa baada ya kuelewa kuwa watu wameelimishwa watawala wamepanic na kuanza kueneza ukanda, ukabila na udini na baadaye mara CDM wanachochea, kumuelimisha mtu ni kumchochea jamani, misri ,libya na Tunisia walikuwa na tatizo la viongozi kukaa madarakani muda mrefu, lakini tz we are fighting for ccm which stays in power for 50 yrs now






maisha magumu mpaka watu waambiwe ni magumu? Kwani watu hawayaoni? Mbona Rais JK ktk hotuba yake amekiri kwamba maisha ni magumu.CDM wakiwahutubia watu maisha ni magumu ndo yanabadilika au kuwapotezea watu muda wa kuhangaikia maisha yao yawe mepesi. Maandamano hayana tija kwa mtz,ila ipo ajenda ambayo wewe huijui unafuata mkumbo. Kama hamkueleweka ktk kampeni ndo mtaeleweka sasa
 
Hakuna sababu ya CDM kuomba serikali ya Mseto kama CUF kwani mbona ushindi upo nje nje tu bila hata ya kuwa kibaraka kama Seif! ushidi ambao utakuwa wa K.O...CCM mnalo hilo mkijaribu kuchomoa mmekwisha

Hawaliwezi na haliwezi kuwa hilo kwa Chama tawala kuingizwa Serikalini kama CUF Zanzibar kwani bado hawatoshi katika kuendeleza nchi.

hapo tu anaalikwa Dr Slaa akalione PAA la IKULU na kuonjeshwa kukalia viti vya ikulu tu.
 
Ndoto ya madaraka. JK hana sababu ya kukutana na cdm. Kwa kipi hasa,wachochee watu kufanya uasi halafu watake mazungumzo na Rais.Hawana jipya waendelee na maandamano mazungumzo ya nini. Na wao wanataka kuingia serikalini kama cuf.Waendelee kupost thread humu JF

Anayetaka kukutana na mwingine ni nani? Chadema ama JK, nafikiri ni JK Chadema hakinahaja ya kukutana na JK.
 
Kwa nini tuchanganye sera mbili tofauti, hawa wanaamini katika ufisadi na nguvu ya pesa, wengine wanaaminin katika nguvu na matakwa ya umma. Utawachanganyaje hawa??

ccm miaka 50 wameshindwa, sasa wasitafute wa kuwasaidia. Wakae pembeni wawaachie CDM nao wafanye peke yao kwa kutekeleza ilani yao, then wanachi (ambao ndo waajiri wao) tuwapime. Wakituridhisha tunawaongezea mkataba. Mbona ccm tumekuwa tukiwaongezea mkataba kila mwaka tangu 1961. Lakini sasa tumeona uwezo wao umefika mwisho, hawana mbinu mbadala wa kuinua maisha ya waajiri wao.

CDM ambao wamekuwa bench wakisoma mchezo wa CCM wamesoma udhaifu wao na wamekuja na mbinu mbadala. Hapa anatakiwa mtu arudi benchi na mchezaji mpya (CDM) aingie kuchukua nafasi.
 
Mkuu hata hiyo serikari ya mseto hatuitaki,nini No Preconditions!!
hakuna mjadala wala suluhu hapa.
Yani inaonyesha JF kuna watu wanaanzisha topic za kuwapa wana JF wenzao hasira,halafu hao wenzao wanaonyesha wanavyokerwa na jambo hilo,then wanakuwa wamepunguza hasira........Bahati mbaya hakuna wa kujibu(ambaye ni CCM)........SIo mbaya......JF ni sehemu nzuri ya kupooza hasira dhidi ya CCM,kama ilivyo kwa wananchi wa Tokyo na siasa za Kijapan wanavyoshauriwa kuwa na picha za viongozi wao majumbani mwao,na wakishikwa na hasira wazifanyie chochote kuondoa hizo hasira eg kuzitemea mate,kuzipiga mateke,kuzitukana nk,hahahahahahaaa
 
Chadema ni wahamasishaji tuu,lakini ngoma nzima imeshikwa na wananchi wenyewe ndio maana mtu yuko radhi kuendesha baiskeli kilomita 150 na bango lake la box ammeeandikia mkaa ili ajumuike na wengine kwenye maandamano,Wananchi wanapojumuika na kutoa kilio cha sauti moja kuhusu matatizo yao kwa njia ya ukweli na inayoruhusiwa kikatiba haina shida kabisa Chadema wanachofanya ni ushauri nasaha tuu,kuwajulisha ananchi namna bora za kudai haki yao,Wangekuwa wanaawafundisha wananchi kutmia njia za kijadi,kisasa na kuingia msituni kuonyesha hasira zao hapo wananchi tusingewaunga mkono.Lakini swala na Mawasiliano ya UMMA,Sauti ya UMMA,Sauti ya Pamoja,na Kilio cha wote useme ni la Chadema hapo utakuwa unadanganya,uwezo wa wananchi kujitoa wenyewe kwenye mihadhara na maandamano ni hatua ambayo imeshafikiwa na hakuna kitu chochote katika nchi hii kitakacho rudisha nyuma tena,Chadema waaendelee kuhamasish uMMA watumie njia ya maandamano mikutano ya wazi kufikisha ujumbe na kilio chao kwa viongozi ni RUKSA kabisa,kwa ujenzi wa nchi yetu.Hakuna muda unaopotezwa hapo kwa sababu mwanadamu anjua anavyopangilia muda wake hakuna bloger hapa ambaye anaweza kumpangia mtu muda eti kwa kudai anapozewa muda mwananchi anapotekeleza haki yake ya kujumuika na kutoa maoni
 
hakuna mgogoro wa kisiasa bongo ambao utafanya kuwe na suluhu ya vyama, tatizoni watendaji ambao hawajui maslahi ya taifa nia yapi. mtu anaposema hakuna haja ya maandamano hajui nini maana ya kufanya maandamano, huwezi kusema watz wanataka maendeleo na c maandamano kwa kuwa nafasi yao kuleta maendeleo walikuwa nayo miaka takribani hamsini iliyopita. Msifanye siasa kuwa ya msimu kutokana na utendaji wenu mbovu serikalini, hamuwezi kuwa mnakula nchi kwa ufisadi watu wasiseme kisa tu uchaguzi umeisha...........pumbavu zao na chama chao
 
Labda kama anataka akutane nao ili awakabidhi ushindi wao aliouchakachua sawa. Ila cha msingi, aanze kufanya kazi. Kufilisi mafisadi na kuwafungulia mashitaka, kuondoa viongozi wabovu (washikaji), kuondoa mizengwe ya CCM/serikali yake +wabunge wake (ona walivyolivuruga BUNGE mpaka CDM wameamua kwenda kwa wananchi moja kwa moja) nk. Ila ni kweli inabidi awashirikishe wapinzani kiukweli na siyo kiunafiki ili aweze kulihudumia Taifa kama Rais. Ila kwa bahati mbaya hana uwezo wa kutosha, hivyo hutegemea sana wasaidizi/washauri wake ambao wanampotosha either kwa manufaa yao au kwa umbumbumbu wao.
 
Watakuwa wanajidanganya sana kama watakutana na Chadema kwa kudhani hili ni tatizo la Chadema, mimi nawashauri waanze na kina Mgaya wa TUCTA kwanza waelewane na waongeze mshahara stahiki ( sababu nina ushahidi wa kutosha kwamba pesa hizo zipo na nchi yetu ni tajiri ).
2. wakutane na vyama vya wamachinga wajue matatizo yao halisi na sio kuwajengea machinga complex
3. wahakikishe wote wanaowasababishia maisha magumu Watanzania wanashughulikiwa mara moja bila kuacha chembe ya shaka.
4. Lianzishwe jukwaa huru la vijana wasio na hajira ( na sio vijana watoto wa vigogo) hapo pawe ni chumbiko la mijadala ya kupunguza ukosefu wa ajira kwa vijana.
Zipo sababu nyingi nimetoa mawazo yangu tu kwa uchache, lakini kama kuna mpuuzi ambaye anadhani tatizo ni CHADEMA anajidanganya, kwangu mimi Chadema naona ni kama starter tu ya kuamsha hasira za watu waliokata tamaa ya maisha na hambao hawana cha kupoteza, maana duniani hawapo na peponi hawapo, je watu hawa wako wapi? mtu anaota ndoto amekufa kwa wiki mara tatu unadhani mtu mwenye maisha bora huwa anaota ndoto za kufakufa?

Mbona umewasahau waliokua wafanyakazi wa East Africa Community? wazee wawatu mpaka wataisha wote, serikali hii imeshalaaniwa na wengi ndio maana mambo yanawaendea kombo
 
hayo maandamano yamepunguza makali ya maisha? Wahimize wananchi kufanya kazi. Mbona hawaelezi serikali nini cha kufanya maisha yawe bora.Baada ya maandamano na mikutano huko mwz,bukoba,mara,shy, je maisha yamebadilika? Huu si muda wa kampeni,waacheni wananchi wafanye shughuli zao.Slaa anakipeleka vibaya chama watu washamchoka kila siku kasema hili mara lile,utekelezaji zero.
Ndg yangu Slaa hana mamlaka yoyote yeye sio Raisi wa nchi, kama unataka afanye mwambie JK aachie ngazi ili CDM iingie kazini uone mafisadi kama watabaki!!!! Lakini anao uhuru wa kuwaelimisha watu waishinikize serikali itimize wajibu, hasa kuwakamata wezi wa fedha lukuki za umma. Mbona hapo hugusi tukisema wezi????????? Wewe ni nani, kwa mtu mwenye uelewa kama wewe naona kuna kitu unaficha au ni mwajiliwa wa wezi hao!!!!!!!!Wewe huna kabisa uchungu wa nchi kufilisiwa na kuachwa utupu?????????Eti CDM ikae tu ikiangalia, lazima waseme hata ingalau wezi washituke wajue tunawaona kasoro wanalindwana watawala!!!!!!!!
Tukiwapatia mwanya watajua Watanzania ni watu gani??????????
 
No preconditions.

Heshima mbele Mkuu MMKJJ: Mimi nadhani CDM wakatae kabisa kukutana na JK au CCM. Kwa vile wazo hilo la Baraza la demokrasia limedakwa mara moja na Tendwa nadhani hii ni project ya CCM yenyewe -- ya kujitafutia life-line ya kutokea, maana sasa hivi imezidiwa mno na hoja za CDM. CCM wanatafuta ahueni kidogo -- mahala pa kupumzikia -- yaani respite maana chama hicho kimekuwa kinaendeshwa puta kwa kasi sana.

Hoja ya CCM kwamba CDM wanataka kuleta macahfuko haina nguvu sana hasa pale CCM wanashindwa, wanapotakiwa kutoa maelezo ni matamshi gani -- tena kwa nukuu husika -- ambayo viongozi wa CDM wamenena majukwaani yanayoweza kuhatarisha amani.
 
JK Kama Rais, nina hakika anayajua matatizo yote haya. Hivyo basi kwa usalama wa nchi yake na Chama chake sidhani kama amekaa tu ametulia. No! He is doing something, let us give him time after the elections and see what will happen. We learn through misktakes. Give him a second chance. Mpaka amefika hapo alipo (Rais) sidhani kama anaweza kukaa bila kutafuta suluhu ya kero zilizopo. Hiyo Ari ZAIDI, nguvu ZAIDI na kasi ZAIDI ni tofauti na Ari MPYA ....... ipeni muda kidogo hiyo ZAIDI, inaweza ikaleta matunda. Yeyote afanyaye kosa, akishaligundua hulirekebisha. Ukimsakama wakati yuko katika process ya kulirekebisha, unamvunja nguvu na ku-disturb process zake. Mnapowapump wananchi na maneno ya kuichukia Serikali, Je hao watendaji wanapowatembelea kwa ajili ya kufuatilia maendeleo si mnataka wazomewe? Hiyo itawapa nguvu kweli? Mi kwa upande wangu namsupport sana Rais wetu, namwombea afya njema na mafanikio katika jitihada zake. Namhurumia anavyosakamwa. kuongoza nchi sio mchezo jamani.

I really wish that were true. 2005 Kikwete alikampeni kwa ujumbe wa change; kwamba anakuja kubadili CCM toka kuwa chama kisichojali na kinachotumika kama kichaka cha utajirisho haramu kuwa chama cha wananchi kama ilivyokuwa hapo awali. Matendo yake tokea atoe ile hotuba ya matumaini ya kuzindua bunge hadi semina elekezi na ziara za mawizarani yamedhihirisha kwamba aliwapiga changa la macho watanzania. Hakuwa na nia wala uwezo wa kuleta mabadiliko ndani ya CCM.

Kibaya zaidi hata kusimamia tu watendaji serikalini kumemshinda; anafanyia mzaha unyanyaswaji wa wananchi huku akitabasamu kwa kauli kama "jamaa wamechora line pale... wanataka kumtoa mtu upepo". Halafu, anakuja kutuonyesha ukali usio wa kawaida kwa wafanyakazi (hotuba kwa wazee DSM) kwamba watatiwa ngeu na polisi wasipotaka kukubaliana naye "mwajiri mkuu" kwa amani. Haya yote huku akiwa na kigugumizi kikubwa kuhusu ufisadi na mafisadi walioisonga CCM kikamilifu. Hawezi hata kuwatamka majina zaidi ya kutoa kauli za rejareja. Mwishowe anajaribu kuihusisha familia yake na siasa za madaraka. Nani atamtilia maanani mtu wa aina hii?

Na tangu lini serikali yenye mamlaka na nyenzo zote ikafuatilia maendeleo kwa kuzurura na kuishia kutoa kauli za kuonya, kutishia na kuagiza kwenye media! Tunataka kuona sheria na taratibu zikisimamiwa ipasavyo-kuanzia ofisini hadi field. Mtendaji yeyote ajue akikiuka maadili adhabu inamshukia bila simile. Vinginevyo, tunabakia na viongozi na watendaji waliokuwa compromised wasioweza kutumia mamlaka yao ipasavyo kuwajibishana kwa maslahi ya taifa.
 
Mgogoro uliopo ni kati yetu wananchi na watawala. Hii si nchi ya vyama vya siasa; si CCM, CHADEMA, CUF, n.k. wenye kushikilia mustakabali wa nchi hii; ni sisi watanzania wenyewe kwa wingi wetu. kama viongozi wa kisiasa wakiamua kukaa na kupatana (sijui kwa kipi hasa) wajue tu kuwa mapatano hayo hayana maana kabisa kama hayazingatii uoondoaji wa kero kuu za wananchi na ujenzi wa demokrasia ya kweli nchini. Hatuhitaji serikali ya umoja wa kitaifa na wasijaribu kabisa mchezo huo. Yumkini hilo baraza la vyama vya siasa limesha-expire. Haliendani na Tanzania tunayoitumainia. Wao wakae kuangalia maslahi yao wajanja wachache wanaotumia vyama kama makampuni binafsi ya utajirisho.

Niongeze tu kuwa hivi sasa CHADEMA ndio wanaoonekana kusoma vizuri hisia na kuzingatia matakwa yetu watanzania; na wanaonekana kuwa makini kuyapigania kama chama kikuu cha upinzani. Haya ni maendeleo mapya na ya kihistoria katika nchi yetu. Wakilegeza uzi ili kumfurahisha Kikwete na CCM yake basi wajue watakuwa wamepoteza fursa adimu ya kihistoria ya kuleta mabadiliko ya kweli nchini. Kwanza wajiulize tu ni mangapi waliyoibua ambayo CCM inahaha kuyarekebisha hata kwa kubabaika tu: katiba mpya; bei za bidhaa, mawaziri (hata PM) kujifanya wanasimamia maendeleo kwa "dhati". So far, they are on the right track. No need to compromise at all!
 
Back
Top Bottom