JK kukiri hali ya fedha serikalini ni mbaya

Inakuwaje serikali inakuwa na deficit kubwa kiasi cua kutoweza kulioa mishahara au kufubd its various programs? Nini kimetokea tangu bajeti ya mwaka hadi sasa? Haya malimbikizo ya madeni yanalipwa kutoka fedha zisizotengwa kwenye bajeti?
 
umoja wenu ndio silaha yenu......maneno aliyoyatoa huyo rais wenu ni aibu sana kwa taifa ..ninyi ndio mna jukumu la kuhakikisha mnakuwa na taifa lenye ustawi...lakini kwa sasa hakuna.....tafuteni shujaa wenu mwingine mwalimu alishatangulia
mwalimu hawezi kutokea tena
 
Hii maana yake ni nini?

Mbona wengine waliliona mapema na wakalisema wakakaripiwa na kuitwa wazushi?

Je, maelezo ya rais kuwa imetokana na 'hatua ya kulipia malimbikizo ya madeni ya nyuma yana mantiki?

Na kwa maelezo haya bunge la bajeti lina maana gani?

Huenda mimi sijui nchi inavyotakiwa kuendeshwa ila hili haliningii akilini.

Kauli hiyo aliitoa kujibu kilio cha Jaji mkuu kuwa mfuko wa mahakama nchini uliotengewa bil 20 mpaka Dec 31, walitegemea wawe wamepokea bil 10 lakini bil 6.3 tu zilikua zimepokelewa.(mwananchi 4.2.12)

Nasikia kwenye local goverment huko mambo nayo yamesimama hakuna pesa, najua ni maeneo mengi hajapata mgao uliopitishwa na bunge liliopita

sasa tunsemaje kwa hili wakuu? tafakari yenu

Kimsingi bajeti ya Tanzania imekuwa kiini macho kwa muda mrefu!
  1. Kwa miaka kadhaa sasa tangu JK kuingia madarakani hakuna wakati malengo ya bajeti yakatimia kama yalivyoombwa bungeni.
  2. Sehemu kubwa ya makusanyo ya serikali imekuwa ikilipa madeni ya mafisadi waliyoikopesha CC kwa ajili ya kampeni za chaguzi mbalimbali.
  3. Kwa miaka mitatu mfululizo kuanzia mwaka 2009 - 2011 hakuna mradi wo wote wa maendeleo uliokamilika kwa wakati! Miradi yote ambayo imekuwa ikizinduliwa utekelezaji wake umechukua muda mrefu kujiko ilivyokadiriwa kutokana na serikali kushindwa kuwalipa makandarasi kwa wakati.
  4. Kwa mwaka huu wa fedha serikali imekuwa hoi hata kulipa mishahara ya watumishi wake achilia mbali kutoa fedha za maendeleo.
Hivyo si tu serikali inapaswa kukiri kuwa imefilisika bali kutangaza hali ya HATARI ili kufuta mipango mipya ya maendeleo!
 
Hii mambo ya kuendesha mdundiko wa miaka 50 ya uhuru nchi nzima matokeo yake ndo hayoo. inanikumbusha mda fulani nilikuwa bwagamoyo kila nyumba unayopita ngoma za mdundiko kwa kwenda mbele... angalia hali za watu wanaodundika na kula na kunywa wiki nzima particularly baada ya kudundika... hata sukari ya chai taaabu...this is what is called utamadunisho......Nadhani nimeeleweka...
 
de'levis who are you please!Nimesoma comments zako napata shaka kidogo! it seems unasiri kubwa moyoni ambayo ukifunguka inaweza kuwa mshike mshike!who are you please??
 
Ni nini alicholalamika hapo? au mradi tu upakaze?

Nchi ya walalamikaji...kuanzia rais waziri mkuu hadi mwananchi... wote wanalalamika.... Nashauri vasco atulie home ashughulike na uchumi hawa wakoloni hawatusaidii sana. Kama ni exploration of the world si inatosha bana!!
 
Mkulima wa korosho mletee mtaalam wa mazao ya korosho yalipofanikiwa duniani. Unamletea mtu kaenda kusoma miaka miwili chuo cha kilimo Iringa, ambapo hakuna hata mkorosho mmoja halafu unamwambia huyu ndio mtaalam? Leta mtu aliyebobea anajuwa kulima na kuuza korosho. Sio kulima tu.

Mfano leo tunawaambia wakulima wetu waanze kulima kwa umwagiliaji (irrigation) badala ya kwenda kuwachukuwa wataalam wa irrigation kutoka Egypt, ambao wana historia toka zama za kabla ya kina Firauni wao wanafanya irrigation kwa mto wao mmoja tu na wanazalisha na kulisha Egypt yote yenye watu zaidi ya millioni 80 na wanauza mazao yao nje ya Egypt. Sisis tunamchukuwa mtu kutoka wapi sijui ambako hata zana za irrigation na mbinu hazijui ipasavyo ndio awape somo. Bila kutumia wataalaam wa fani zao maweee! Sasa hayo si ya kungoja Serikali. Ni wenyewe wakulima wangekuwa na akili wangetafuta wa Egypt kuja ku volunteer.

Si unaona wawekezaji waliofuzu, utakuta pale kuna Mholanzi, kule kuna mfilipino, pale kuna Mhindi. Wewe unafiri wanakuja tu wale? wanaletwa kwa maana yake.

Leo sisi tunamleta Mhindi aendeshe shirika la treni wakati treni za kwao zimejaa tambuu na watu wanajazana mpaka kwenye paa la treni, badala ya kuleta Mjerumani, Mjapani, M Canada. Aliyebobea kwenye usafiri wa treni, ukienda kwao mpaka unaona raha.

Unachafua hewa hapa!! Ni shida kujua unasimamia upande gani. Unaona watu wanaomshutumu JK ni wabaya lakini comments zako hapa zinaonesha kuna makosa kadhaa yanafanywa katika uendeshaji wa shughuli. Uko sahihi kwenye bidii binafsi za kujitafutia maendeleo!!

Tambua kuwa wanaomlaumu JK wanamlaumu kwa kutotoa muongozo na kuhakikisha utekelezwaji wa miongozo ili tuwe na hicho kilimo cha umwagiliahi, tuwe na hizo treni unazosema. Yeye ndio anaongoza serikali hii!! Asiishie kusema "serikali haina fedha", aseme kipi kinafuata. Wakati nchi nyingi hasa zilizoendelea zinajaribu kupunguza au ukubwa wa serikali au gharama za uendeshaji, sisi masikini tuko out of control. Je kwa haya, tumlaumu nani?? Je si yeye alisimama majukwaani na kuahidi miradi mingi? Je si yeye huyu atashindwa kuitekeleza??

Ondoa ushibiki, be objective. That will make ya a better critic!!
 
Mkulima wa korosho mletee mtaalam wa mazao ya korosho yalipofanikiwa duniani. Unamletea mtu kaenda kusoma miaka miwili chuo cha kilimo Iringa, ambapo hakuna hata mkorosho mmoja halafu unamwambia huyu ndio mtaalam? Leta mtu aliyebobea anajuwa kulima na kuuza korosho. Sio kulima tu.

Mfano leo tunawaambia wakulima wetu waanze kulima kwa umwagiliaji (irrigation) badala ya kwenda kuwachukuwa wataalam wa irrigation kutoka Egypt, ambao wana historia toka zama za kabla ya kina Firauni wao wanafanya irrigation kwa mto wao mmoja tu na wanazalisha na kulisha Egypt yote yenye watu zaidi ya millioni 80 na wanauza mazao yao nje ya Egypt. Sisis tunamchukuwa mtu kutoka wapi sijui ambako hata zana za irrigation na mbinu hazijui ipasavyo ndio awape somo. Bila kutumia wataalaam wa fani zao maweee! Sasa hayo si ya kungoja Serikali. Ni wenyewe wakulima wangekuwa na akili wangetafuta wa Egypt kuja ku volunteer.

Si unaona wawekezaji waliofuzu, utakuta pale kuna Mholanzi, kule kuna mfilipino, pale kuna Mhindi. Wewe unafiri wanakuja tu wale? wanaletwa kwa maana yake.

Leo sisi tunamleta Mhindi aendeshe shirika la treni wakati treni za kwao zimejaa tambuu na watu wanajazana mpaka kwenye paa la treni, badala ya kuleta Mjerumani, Mjapani, M Canada. Aliyebobea kwenye usafiri wa treni, ukienda kwao mpaka unaona raha.

Sisis = Sisi

Sasa mama, huoni kama hapo lawama zinarudi kwa rais wako?
Yaani unataka mkulima wa korosho pale Madimba ndiye atafute mtaalamu wa korosho kutoka nchi iliyobobea katika kulima na kuuza korosho?!? Mama mbona unatia aibu mbele za watoto na wajukuu zako?!?Serikali ndiyo inapaswa ifanye kazi ya kutafuta wataalamu; mbona inaleta consultants lukuki kwenye benki kuu na wizara zetu? Inashindwa nini kufanya hivyo unavyosema wewe?!
 
Inakuwaje serikali inakuwa na deficit kubwa kiasi cua kutoweza kulioa mishahara au kufubd its various programs? Nini kimetokea tangu bajeti ya mwaka hadi sasa? Haya malimbikizo ya madeni yanalipwa kutoka fedha zisizotengwa kwenye bajeti?

Labda gharama za maonyesho ya wanajeshi kupasuwa mawe kwa vichwa wakati wa sherehe za miaka 50 uhuni wa TZ Bara?
Labda gharama za uchaguzi wa Igunga na maonyesho yake ya watu kuvuliwa "hijabu" na wengine kumwagiwa tindikali?
 
Back
Top Bottom