BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,790
- 288,007
Sasa Kikwete amekiri kwamba Serikali ina ukata wa kutisha. Je, kuna hatua zipi ambazo Serikali inachukua ili kuongeza mapato yake na wakati huo huo kupunguza matumizi ya anasa kama vile mashangingi kwa maofisa wengi wa juu Serikalini ambao gharama kubwa za kuyaendesha haya ikiwemo mafuta na matengenezo yanatokana na pesa za walipa kodi? Vipi kuhusu kukata safari za nje kwa kwa kipindi cha miaka mitatu ili kupambana na ukata huu? Vipi kuhusu kufanyia marekebisho ya mikataba ya uchimbaji wa dhahabu ambayo aliahidi kufanya katika kampeni za 2005 ili nchi inufaike na na rasilimali zake? Je haiwezekani kuongeza mrahaba ukafikia hata 205 au zaidi na kuanza kuwatoza kodi ya mapato wachimbaji wote wa madini ili kutunisha mfuko wa hazina? Je kuna mkakati wowote kati ta Serikali na TRA kuongeza idadi ya walipa kodi nchini na kuwabana wale wakwepaji wakubwa wanaokwepa kulipa mabilioni ya kodi kila mwaka? Nasikia nchi yetu pamoja na kuwa population inasemekana ni 40 million lakini idadi ya walipa kodi inadaiwa haifiki hata laki 7!!!! Je kuna mkakati wa kuongeza idadi hii ili miaka mitano ijayo idadi ya walipa kodi iongezeke na kuwa mara 10 au hata zaidi ya hii sasa? Au ndio kishakubali kwamba Serikali ina utata basi yamekwisha wanaendelea kubweteka ili kumsubiri Mungu atuletee neema ya mapato kuongezeka na hivyo kuondoa utata uliokuwepo?
....na haya madeni waliyolipa ni madeni gani hayo!? Nadhani Watanzania wengi tungependa kuyafahamu ni madeni yepi anayoyazungumzia Kikwete na kama nchi iliingia madeni hayo kwa maslahi ya Watanzania au kwa ajili ya kununulia mashangingi?
....na haya madeni waliyolipa ni madeni gani hayo!? Nadhani Watanzania wengi tungependa kuyafahamu ni madeni yepi anayoyazungumzia Kikwete na kama nchi iliingia madeni hayo kwa maslahi ya Watanzania au kwa ajili ya kununulia mashangingi?