JK Kuhudhulia ufunguzi wa Kibo Palace & Snow Crest Hotel Arusha

JK mbona hata kwenye birthday ya mwanao unamleta, kidau tu kwenye uchaguzi, hata ukitaka kuifanyia Ikulu unaweza.
 
Acha uhuni hotel ya Kibo Palace ni ya Swai mwenye Bureau de change Moshi

what is a different? hata Arusha nasikia ana Bureau De Change pia, hapo pia rais atadanganywa kuwa ajira zitakuwepo nyingi sana ila cha ajabu Experts wako wengi kuzidi watanzania na wanachekelea rudi nyuma tizama ilani ya CCM kuhusu ajira kwa watanzania utacheka na kusikitika sana.

Wafanya kazi mishahara ni midogo sana, ila experts wanapewa nyumba(italipiwa maji umeme hadi mlinzi),usafiri nahadi kusomeshewa watoto, nenda kauulize Front Office Manager na ni mzawa kama anapata vyote hivyo?

tuchukulie mfano watanzania tutafaidika na uwekezaji haya basi eg katika Hotel moja wafanyakazi wamesota 5 yrs kwa salary ya 70,000/Tsh ni majuzi tu serikali ilipotoa tamko mishahara iongezwe na kufikia 150,000/=Tsh kima cha chini, njoo kwa ma experts its more than 700$ na huyo ni Housekeeping au stores manager jamani hata ivyo vyeo vyahitaji mtu kutoka India?? maaana wahindi ndio nasikia wamejaaa sana hotel za Arusha.

Sasa mwategemea mfanyakazin mwenye kiwango cha chini kama hicho kujenga maisha yake Arusha na Mji wenyewe wa kitaliii na haujapangika kitalii na kuan gap kubwa kati ya maskini na matajiri, nasikia Arusha ni kiboko kwa kodi za nyumba sasa je kiwanja itakuwa bei gani na huyo mfanyakazi atanunua lini hicho kiwanja cha millioni 7??

Rais huambiwa haya mambo wakati anafanya funguzi katika hizi hotel au??

 
Owner of Kibo palace is MRAMBA though there is rumours that he made a transfer to Raila Pm of kenya,the other one I have no clue.
On those two days,president must be in Arusha region because on 19th Dec he has the task as stipulated in our constitution of granting commission to people who are doing military training at Tanzania Military Academy-Monduli which will make them to be Officers in Tanzania Peoples Defence Forces. There is no delegation in that commission ceremony

Kama Kibo Palace hotel belongs to Pesambili , most likely the money used to build the hotel must have been the commission he received for facilitating the dubious ALEX STEWART deal which is the cause of his criminal prosecution!! It may not surprise me that in spite of all this information the president has the audacity to officiate the opening of such a hotel!! Mungu ibariki Danganyika.
 
Wadau, mmezungumza sana kuhusu Kilimanjaro Hoteli, Mount Meru, 77, Naura Springs, Impala na nyinginezo. Mbona nasikia tena Ijumaa hii Muungwana anakwenda kuzindua hoteli nyingine Arusha. Ni ya nani hii? au ni ya mafisadi wengine?

Ni sahihi kwake kuhusishwa na rasilimali za mafisadi - ikiwa ni kweli - hasa katika kipindi hiki ambacho mwenyewe amesema bayana kwamba watu wanapaswa kuwa makini na 'zawadi'? Ni haki pia kwake 'kubariki' rasilimali za watendaji wake ambao wanajificha kwa majina ya wengine, hasa kwa vile ameshasema kwamba mwakani watu wanapaswa kutenganisha siasa na bizinez?

NAOMBA MAONI YENU WADAU, NA MWENYE FUNUNU KUHUSU HOTELI HIYO, AMBAYO NIMEISAHAU JINA, TAFADHALI AMWAGE DATA HAPA.
 
Ni ya nani hii? au ni ya mafisadi wengine?

sasa kama haujui ni ya nani, kwanini kichwa cha habari kinasema ni ya mafisadi?
 
Ni ya nani hii? au ni ya mafisadi wengine?

sasa kama haujui ni ya nani, kwanini kichwa cha habari kinasema ni ya mafisadi?

Jamaa kaweka mtego. Si kwamba hajui ila hataki ijulikane kwamba yeye ndiye kaleta mada.
 
sasa humu ndani mna-distort nia ya forum hii kuna watu humu ndani wanajaribu kupotosha ukweli from the rivality nature the two hotels are about to pose in the general hospitality industry in Arusha! Pull up your soxs dudes, accept competition!
 
Ni sahihi kwake kuhusishwa na rasilimali za mafisadi...
Hata kama sio ya fisadi, kwani kuna lazima gani kwa JK kufungua hiyo Hotel?
- Urais umekuwa 'low' namna hiyo?
- Kwanini hasihusishwe Director wa Idara ndani ya Wizara ya Utalii?
- Hatujui gharama zinazoambatana na safari za Rais?
- Ni sahihi kwa Watanzania kubeba mzigo huo kwa Rais kwenda kufungua Hotel?
- Hivi Rais ana washauri wa Uchumi?

mmh, swali linazaa swali! Sijui washauri wa Rais kama wanazo kichwani!:rolleyes:
 
Hivi hamuoni kwamba suala zima la kuzungumzia MAFISADI na UFISADI limewekwa ili kupotosha maana nzima ya dhana hii? Tutakaa kuzungumza ufisadi na mafisadi huku wenyewe wanajichukulia kana kwamba ni nyumbani kwao.

Walipoanza kuchota - TENA ZAMANI, enzi zile za mashirika ya umma (SU) - mbona hatukusema? Kwani ule ulikuwa ni nini? Watu walichota mpaka mashirika yakafilisika na kufa kabisa. Sisi KIMYA!

Leo hii ndio TUNAAMKA, kana kwamba tumezinduliwa usingizini? Wa kulaumiwa ni SISI WENYEWE! Tuliwapa ruksa ya kuchota, kwa kusingizia kwamba hao ni WAKUBWA, wako juu ya Sheria? Hivi kweli sisi tuna akili nzuri? NANI yuko juu ya Sheria, kama sisi wenyewe hatujawaruhusu?

Nawapeni mfano. Basi linatembea mwendo wa kasi kupitiliza. Lina abiria 65! Hakuna abiria hata mmoja anayediriki kusema lolote. Anatokea kijana, jasiri - MIMI - na kwenda mbele kwa dereva, kumwambia aendeshe kwa mwendo unaoruhusiwa, kwani tunataka kufika sio kuishia MORTUARY!

Unajua kinachotokea? Naanza kupigiwa kelele, tena kwa matusi ya nguoni - siwezi kuyataja hapa - na watu wazima wenye akili zao. Wanadai wana haraka. Haraka ya kufika au kufa?

Bahati nzuri tunafika, ninaomba dua kumshukuru Mola.

MARA NGAPI tumeona abiria wanaonusurika kufa kwenye ajali lukuki wakisema "Dereva alikuwa akiendesha kwa mwendo mkali kweli!" Enhe? Na ninyi mlifanya nini?

Unapokataa kumwajibisha mtu anayefanya makosa - kuendesha mwendo wa kasi kupitiliza ni KOSA, kwani anahatarisha usalama wako na wa wenzako - nawe pia unakuwa unashiriki katika kosa. Ni sawa na kumwona mwizi akivunja nyumba ya jirani yako, ukamwona na hukumzuia, kwa kusema "Si kazi yangu!" Kama kuna ambaye alikuona ukishuhudia, unaweza kuhusishwa kwenye uhalifu huo, kwani, kutokuzuia kosa kufanyika ni kushiriki kwenye kosa... accessory to the crime!

Sasa, kama sisi tunaendelea - tena wengine kuwahimiza madereva kwenda mwendokasi kupitiliza - kufanya hayo, huu nao si ufisadi?

Kabla hujamtoa mwenzako boriti jichoni mwake, angalia la kwako!

Tusilalamike UFISADI na MAFISADI wakati sisi tunashiriki katika yote hayo. Huko BOT na Hazina, Grey Mgonja hakupitisha hizo barua za kuitetea Alex Stewarts Assayers PEKE YAKE! Kulikuwa na makarani, wahasibu, wakurugenzi, makamishna! Walikuwa wapi wasiseme wakiona MKUU WAO WA KAZI akiharibu? NAO WALISHIRIKI! Wasisimame mbele ya Pilato na kusema "Nilimwona fulani akifanya hivi, na hivi, na hivi!" Wewe ULIKUWA WAPI?

Mnawalenga wenzenu kidole kimoja, viwili vinawalenga ninyi wenyewe!

Atakayekerwa na maoni haya, basi yeye ndiye FISADI NAMBARI WANI!

./Mwana wa Haki

P.S. TUACHE UNAFIKI!
 
...just a whiff of wishful thinking that the muungwana choice ya GOD ALMIGHTY is going to use the hotel opening platform to announce his RESIGNATION from the POLITICS of this country as a ROLE MODEL ya UWAJIBIKAJI. He is alleged to have ascended into the PRESIDENCY vide CORRUPT pathways! As an example of the kind of ethical and moral codes desired of Tanzanians if we are to make tangible progress and burst out of our present ABYSS, the PRESIDENT should set a much needed precedence, an example ya kuwajibika from the TOP so that others can follow! ....ONLY and I repeat ONLY if the tuhumas we come across daily, yaani yale mambo ya mahela ya chaguzi na harufu yake yote, NI KWELI. Not otherwise.

....afterwards lets dwell on matters of LAW and order. Strict adherence to that once we have set adherence to proper set of ethics and morality! watu hawawezi kuendelea kufanya madudu, madudu tu forever.
 
Wana JF,

Habari nilizo zipata to mjini Arusha ni kuwa Rais JK ataudhulia ufunguzi wa Snowcrest hotel(The Peak of Perfection) na Kibo Palace Hotel(Five Star) hapo mjini Arusha mnamo tarehe 18 na 19 December 2009,

Maswali yangu ni kuwa sasa kamekuwa ni system kusikia Rais wa nchi kuudhulia funguzi nyingi za hotel, Last time nilisikia Rais kamtuma mwakirishi katika ufunguzi wa Seliani Hospital iliofunguliwa Arusha Mjini yeye hakuja, Siku nyingine akaja mwenyewe katika ufunguzi wa bank ndogo ni branch ya FBME opposite na East African Hotel, this time ana kuja kwa ufunguzi wa hizo hotel mbili.

IKULU inatuambia hakuna mtu mwingine(mwakirishi) wa ufunguzi wa hizo hotel??

Rais Hana kazi za msingi sana ni mpaka aje kwa ufunguzi wa hotel?

Je kuna Interest zipi katika hizo hotel kutoka IKULU?

Snockrest Hotel kwanza last time nilipita Arusha nikakuta imesogelea eneo la barabara ya Arusha - Moshi which means eneo lote la parking pale mbele ya Hotel latakiwa kubomolewa.

Watu wanaopanga safari za Rais wanajua hayaaaa?

Ufunguzi wa Seliani Hospital kwanini Rais hakujaa??


Thanx for the facts lakini napenda kutoa angalizo mkuu..... kuhusu matumizi ya L na R unaonekana kuyachanganya....

Mwisho napenda kuwaambia kuwa mnatunisha misuli yenu ya vichwa bure mzeeke siku si zenu, kwani hamjui kuwa raisi wenu ni rais wa watu na chaguo la mungu, we kama una kajistationery yako au kakibanda cha cm kama sio sherehe ya mtoto kuota meno mwite aje atakuja tuuu kwani unafikiri ana tatizo... sasa kama yote muhimu ya nchi hayawezi hata haya asifanye aaah jamani mje mseme hajafanya kitu kabisa, c bora apate la kujitetea kuwa alikuwa anakuja kwenye basidei zenu,,,, NI hayo tu

NB: DO NOT LET PEOPLE DRIVE YOU CRAZY WHEN U KNW ITS A LONG DISTANCE....
 
Hivi kuna tatizo gani kwa Rais kufungua iwe hoteli au hospitali au shughuli nyingine yoyote? Siyo siri nyie watu ambao mnahojihoji kwa kweli mwakera sana nyien ati. Alaa!!Ebo!!Mna matatizo sana nyie.
 
Kila hoteli Arusha inamilikiwa na Mafisadi? Hivi zile za Sumaye tulikuwa tunasikia zimeishia wapi?

Nimesikia kwamba zile za sumaye zimerudishwa serikalini halafu si unakumbuka jamaa aliondoka nchini kwenda kusoma ili kutupotezea.
 
Wakuu kwa hiyo Bongo kila mwenye pesa ni fisadi, si mchezo ,ila suala la kufungua hotel kwa raisi si jambo la kushangaza, au mngeuliza kwa nini amekataa kufungua hotel za wazalendo kaenda kufungua siku ya mauzo kwenye soko la hisa nje ya nchi?.tujadili mambo kwa ajili ya ujenzi wa nchi lakini sio kwa msukumo wa jealous
 
nadhani hatasahau kuwapitia na Watanzania wenzetu walio poromokewa na Miamba huko same,akisha fungua hiyo hotel
 
Wadau,

Hakuna hata mtu mmoja kati yenu aliyemtaja mmiliki sahihi wa hiyo hoteli. Binafsi namfahamu, wala sio mtu "mkubwa", kama hao mliowataja - Pesambili na Swai!

Hivi, ili Rais aje kuzindua hoteli yako lazima uwe mtu "mkubwa" na "fisadi"? Huwezi kuwa mtu wa kawaida kama watu wengine?

Hizi dhana potofu hazijengi, zinabomoa. Mwenyewe akisoma - bahati nzuri si mwenzetu humu ndani - atazimia kwa kicheko! Mnampa sifa ambazo sio zake.

Nawahakikishieni, mwenye hoteli hiyo ni mtu wa kawaida sana, hana makuu. Lakini nyie mnajifanya kama vile mnajua kila kitu! Kwani akina Mramba na swai ndio wenye ukiritimba wa kuwa na hoteli za nyota tano wao peke yao?

UNAFIKI MKUBWA!

./Mwana wa Haki
 
katika kuonyesha yeye na mafisadi damu damu mh rais akiwa njiani kwenda monduli majuzi alifungua hotel nyingine ya fisadi mramba basil akimshirikisha bw mmoja kivuli william,...iitwayo "SNOW CREST" iliofunguliw a kwa mbwe mbwe na vifijo huku arusha nzima ikiwa hoi kujua nini kinaendelea,,..
anyway ni moja ya fadhila lakini hatudhan rais anaitaji kuwa cheap kihivi kwa washenzi kama hawa na hivyo kutufanya kukosa imani na haya makesi yasiyoisha....
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom