JK: Inakuwaje uko upande wa upinzani?

siyabonga

Senior Member
Jan 25, 2012
125
35
Wakuu, ukiwa ndani ya mtumbwi huwezi kukaa kimya unapoona mmoja wenu yuko busy anatoboa mtumbwi katikati ya mto. Madhara yake wote mnayajua.

Yapo mengi yanayoonyesha kuwa kinachofanyika ni kusaidia upinzani;

1. Inakuwaje matukio makubwa na mazito yanatokea na kiongozi anakaa kimya tu bila ya kutoa kauli yoyote? Inahitaji rasilimali gani? Neno, kauli ina nguvu kubwa kiutawala. Au ni style ya upepo, utapita?

2. Inakuwaje Mawaziri wanaachwa wajipiganie na kudhalilika wakati ungeweza kuepusha haya kwa kuyawekea msimamo mapema: Nchimbi, Mwakyembe na wezi wa mafuta na shaba waliotoroshwa ki-mizengwe.

3. Inakuwaje kilio cha watu wa Nchi yako, kupunguza safari za nje, ukubwa wa misafara, unapuuza?

4. Unapata muda saa ngapi wa kutuliza akili na ku-concentrate kushughulikia matatizo yanayolikabli Taifa wakati muda wote uko safari?

5. Ni kweli imeshindikana kuwashushulikia wezi na wabadhirifu wa mali za umma?

6. Kuna ugumu gani kuzifanyia kazi hoja muhimu, hata kama zimetoka upinzani, iwapo zina maslahi kwa Taifa?

7. Huko Zanzibar, CUF pia ni chama shiriki katika kutawala. Hoja zao zinasikilizwa au mpaka wapande jangwani na kufanya mikutano ya hadhara? Kwa nini wanapuuzwa na kupewa majina ya kudhalilisha?

8. Unamkumbuka muasisi wa Perestroita?

Yapo mengi mengine, unawapa tabu wenzio kujitetea muda wote wakati mengine yangeweza kufanyiwa kazi.
 
Dunia imekuwa kijiji kidogo sio lazima ukae Tandahimba kufahamu kinachotokea Tandahimba.
 
Mkuu pole kwa kupoteza muda wako kumshauri mzee wa totozi, aka dhaifu, aka mzee wa kulipa fadhila aka mzee wa tumbo kwanza nchi badaye, aka mzee wa kulindwa na majini, siku nyingine usipoteze tena muda wako kumashauri huyu dhaifu hata serikali yake.. Wao wanaamini watz wote ni wajinga na hakuna hata siku moja wataelevuka, wako hapo kupiga dili, na kuua yoyote asiye upande wao... Wako hapo ikulu kuhakikisha nchi inauzwa kwa gharama yoyote ile.

So usitegemee majibu au maamuzi magumu toka kwa hii serikali ya kupiga dili.. Hilo sahau, siku nyingine huu muda kahangaikie familia yako... Hakuna mtu aliyewahi kuwa let down watz kama huyu...

Yeye ni mtu wakuhudhulia misiba tu na kusafiri, hana vision wala mission hata ukimtuma nepi( nape) amuulize jk kwanini watz ni maskini yeye jk hajui wala serikali yake haijui kwanini watz wanazidi kuwa maskini.

Wala hawajui kwanini watoto zaidi ya wanafunzi 5000 wanaomaliza shule ya masingi hawajui kusoma na kauandika lakini wanafaulu.
 
mi nilitegemea kwa kua JK ametembelea sana nchi za nje na anajua zinavyojiendesha basi ange adapt na yeye akawa anaendesha nchi kidhungu dhungu lakini mmh mtoto wa mkulima ni mtoto wa mkulima tu hata umpeleka ulaya atabakia kua mtoto wa mkulima
 
Hivi unataka Rais aongoze kizungu watu ambao hawajui ya wazungu? Hukuona juzi Michelle Obama akihutubia Baraza la DEMOCTATIC, Mama SALMA akifanya hivyo mbele ya NEC ya CCM si kule Machame na Karatu wote wataambiwa eh mnaona, tupeni sisi nchi. Mwacheni JK jamani kaona mengi sasa anawapuuza tu.
 
Mkuu pole kwa kupoteza muda wako kumshauri mzee wa totozi, aka dhaifu, aka mzee wa kulipa fadhila aka mzee wa tumbo kwanza nchi badaye, aka mzee wa kulindwa na majini, siku nyingine usipoteze tena muda wako kumashauri huyu dhaifu hata serikali yake.. Wao wanaamini watz wote ni wajinga na hakuna hata siku moja wataelevuka, wako hapo kupiga dili, na kuua yoyote asiye upande wao... Wako hapo ikulu kuhakikisha nchi inauzwa kwa gharama yoyote ile. So usitegemee majibu au maamuzi magumu toka kwa hii serikali ya kupiga dili.. Hilo sahau, siku nyingine huu muda kahangaikie familia yako... Hakuna mtu aliyewahi kuwa let down watz kama huyu... Yeye ni mtu wakuhudhulia misiba tu na kusafiri, hana vision wala mission hata ukimtuma nepi( nape) amuulize jk kwanini watz ni maskini yeye jk hajui wala serikali yake haijui kwanini watz wanazidi kuwa maskini. Wala hawajui kwanini watoto zaidi ya wanafunzi 5000 wanaomaliza shule ya masingi hawajui kusoma na kauandika lakini wanafaulu.

Mbona unalalamika tu, husemi mbadala wa JK ni nani na kwa sababu gani, au ndo unataka kutuambia haya magarasha ambayo yanategemea vyanzo kutoka CCM ili kupata uongo wa kuwaambia wananchi? teh teh teh, kazi kweli kweli.

Hakuna Rais kama JK miaka 20 badaa ya 2015 na nina uhakika watanzania wengi tutamkumbuka JK kwa mema yake mengi kwa watanzania.
 
Katika maswali yako hayo hawezi kujibu hata moja
Hayo si majungu tu, hata mimi nisingehangaika na kuyajibu. Endeleeni kuwachangisha watanzania maskini kwenye mikutano yenu ya hadhara huku mkipuliza kuwa watanzania ni maskini.
 
Hivi unataka Rais aongoze kizungu watu ambao hawajui ya wazungu? Hukuona juzi Michelle Obama akihutubia Baraza la DEMOCTATIC, Mama SALMA akifanya hivyo mbele ya NEC ya CCM si kule Machame na Karatu wote wataambiwa eh mnaona, tupeni sisi nchi. Mwacheni JK jamani kaona mengi sasa anawapuuza tu.

:biggrin1:
 
mbona JK mwenyewe alishasema ingelikuwa inawezekana angeiachia nchi wengine waongoze,huyu kachoka jamani ...autopilot:flypig:
 
Dunia imekuwa kijiji kidogo sio lazima ukae Tandahimba kufahamu kinachotokea Tandahimba.

Kwa hiyo kwako unaona kwa mtu kama raisi ata akikaa huko huko nje ya nchi Marekani,Brazili ni sawa kwa sababu atakuwa anasikia yanayotokea huku sio? are you serious? akishasikia then what? kwa ufahamu wako wewe yale unayoyasikia na uhalisia wa kitu ni 100% alike sio? Haya nenda kamwambie Mwangosi ameuawa na jeshi la Polisi tena mbele ya RPC wa Iringa,tuone kama baada ya kumwambia kutakuwa na mabadiliko
 
Wakuu, ukiwa ndani ya mtumbwi huwezi kukaa kimya unapoona mmoja wenu yuko busy anatoboa mtumbwi katikati ya mto. Madhara yake wote mnayajua.

Yapo mengi yanayoonyesha kuwa kinachofanyika ni kusaidia upinzani;

1. Inakuwaje matukio makubwa na mazito yanatokea na kiongozi anakaa kimya tu bila ya kutoa kauli yoyote? Inahitaji rasilimali gani? Neno, kauli ina nguvu kubwa kiutawala. Au ni style ya upepo, utapita?

2. Inakuwaje Mawaziri wanaachwa wajipiganie na kudhalilika wakati ungeweza kuepusha haya kwa kuyawekea msimamo mapema: Nchimbi, Mwakyembe na wezi wa mafuta na shaba waliotoroshwa ki-mizengwe.

3. Inakuwaje kilio cha watu wa Nchi yako, kupunguza safari za nje, ukubwa wa misafara, unapuuza?

4. Unapata muda saa ngapi wa kutuliza akili na ku-concentrate kushughulikia matatizo yanayolikabli Taifa wakati muda wote uko safari?

5. Ni kweli imeshindikana kuwashushulikia wezi na wabadhirifu wa mali za umma?

6. Kuna ugumu gani kuzifanyia kazi hoja muhimu, hata kama zimetoka upinzani, iwapo zina maslahi kwa Taifa?

7. Huko Zanzibar, CUF pia ni chama shiriki katika kutawala. Hoja zao zinasikilizwa au mpaka wapande jangwani na kufanya mikutano ya hadhara? Kwa nini wanapuuzwa na kupewa majina ya kudhalilisha?

8. Unamkumbuka muasisi wa Perestroita?

Yapo mengi mengine, unawapa tabu wenzio kujitetea muda wote wakati mengine yangeweza kufanyiwa kazi.

Nimeipenda analysis yako kiasi kwamba kubofya like nimeona kama haitoshi
 
ke1.jpg
 
Kwa hiyo kwako unaona kwa mtu kama raisi ata akikaa huko huko nje ya nchi Marekani,Brazili ni sawa kwa sababu atakuwa anasikia yanayotokea huku sio? are you serious? akishasikia then what? kwa ufahamu wako wewe yale unayoyasikia na uhalisia wa kitu ni 100% alike sio? Haya nenda kamwambie Mwangosi ameuawa na jeshi la Polisi tena mbele ya RPC wa Iringa,tuone kama baada ya kumwambia kutakuwa na mabadiliko

Hajawahi kukaa huko huko huwa anaenda na kurudi.

Mkumbuke pia kwamba ndege ya rais ni kama ofisi pia.
 
acha hizo,basi aishi huko ughaibuni siku zote kwa kutumia utandawazi,hamna haja ya kuja tz wakati kuna utandawazi.hizo ni akili za kuku.
 
Back
Top Bottom