JK, iliwezekana, mbona sasa kimya?

Mundali

JF-Expert Member
Sep 16, 2010
749
164
Mheshimiwa JK,

Mnamo mwezi June, 2010 pale Dodoma wakati kikao cha bajeti kikiendelea, ulitutangazia watanzania nia njema ya serikali yako ya kunusuru ulichoita hasara waliyopata wafanyabiashara ya mazao na sekta ya utalii kutokana na mtikisiko wa uchumi duniani. Mpango huo mliupa jina "Stimulus Package".
Serikali yako kwa upendo iliokuwa nao kwa wafanyabiashara wale (na si wakulima) mliamua kuwagawia fedha kwa hasara walizosadikika kuzipata. Makampuni yaliyofaidika yamebaki kuwa siri ya serikali yako.

Kwa angalizo tu kipindi hicho ilikuwa ni miezi minne kabla ya wewe kuingia kwenye kinyang'anyiro cha uchaguzi mkuu. Ulitenga kiasi cha shilingi 1.3 trilioni kwa mpango (zawadi?) huo. Mimi mtanzania raia wa kuzaliwa sina nchi nyingine ninayoifahamu zaidi ya mama Tanzania, nauliza je,

1. Kipi ni muhimu kati ya wafanyabiashara wachache waliopata hasara ya mtikisiko wa uchumi wa dunia, ama watanzania wote wanaopata hasara kutokana na janga la Giza na kupanda kwa bei za mafuta?

2. Serikali yako iliweza vipi kujibana na kupata shilingi trilioni 1.3 katika bajeti ya 2010/2011 ya stimulus package, ikashindwa kujibana katika bajeti ya 2011/2012 kupata pesa kama hizo kununulia mitambo ya umeme?

3. Mbona trilioni 1.3 zilipatikana mapema kabla ya October 2010?

4. Kuna uhusiano wowote kati ya stimulus package na miezi takribani mitatu ya helikopta tatu kupzunguka nawe nchi nzima katika kampeni zako?

5. Uliweza kuajiri askari wapya zaidi ya 5000 na kununua magari ya maji ya kuwasha na zana nyingine za kutushikisha adabu tukipinga matokeo haramu, kwa mwaka huo wa 2010 pekee, uwezo huo uliutoa wapi mheshimiwa sana?

NAOMBA MAJIBU TAFADHALI MR. PRESIDENT
 
Mheshimiwa JK,
Mnamo mwezi June, 2010 pale Dodoma wakati kikao cha bajeti kikiendelea, ulitutangazia watanzania nia njema ya serikali yako ya kunusuru ulichoita hasara waliyopata wafanyabiashara ya mazao na sekta ya utalii kutokana na mtikisiko wa uchumi duniani. Mpango huo mliupa jina "Stimulus Package".
Serikali yako kwa upendo iliokuwa nao kwa wafanyabiashara wale (na si wakulima) mliamua kuwagawia fedha kwa hasara walizosadikika kuzipata. Makampuni yaliyofaidika yamebaki kuwa siri ya serikali yako. Kwa angalizo tu kipindi hicho ilikuwa ni miezi minne kabla ya wewe kuingia kwenye kinyang'anyiro cha uchaguzi mkuu. Ulitenga kiasi cha shilingi 1.3 trilioni kwa mpango (zawadi?) huo. Mimi mtanzania raia wa kuzaliwa sina nchi nyingine ninayoifahamu zaidi ya mama Tanzania, nauliza je,
1. Kipi ni muhimu kati ya wafanyabiashara wachache waliopata hasara ya mtikisiko wa uchumi wa dunia, ama watanzania wote wanaopata hasara kutokana na janga la Giza na kupanda kwa bei za mafuta?
2. Serikali yako iliweza vipi kujibana na kupata shilingi trilioni 1.3 katika bajeti ya 2010/2011 ya stimulus package, ikashindwa kujibana katika bajeti ya 2011/2012 kupata pesa kama hizo kununulia mitambo ya umeme?
3. Mbona trilioni 1.3 zilipatikana mapema kabla ya October 2010?
4. Kuna uhusiano wowote kati ya stimulus package na miezi takribani mitatu ya helikopta tatu kupzunguka nawe nchi nzima katika kampeni zako?
5. Uliweza kuajiri askari wapya zaidi ya 5000 na kununua magari ya maji ya kuwasha na zana nyingine za kutushikisha adabu tukipinga matokeo
haramu, kwa mwaka huo wa 2010 pekee, uwezo huo uliutoa wapi mheshimiwa sana?
NAOMBA MAJIBU TAFADHALI MR. PRESIDENT

Haya ni maswali magumu sana kwa mheshimiwa sana,ila amini nakuambia baada tu ya bunge la bajeti kuisha tutaandamana mwanzo mwisho na majibu yatapatikana-Subiri makamanda warudi toka dodoma
 
Mimi hii thread nimeipenda saaaaaaaaaaaaana. Watanzania wenzangu ukweli ni kwamba hawa CCM kwa kuchezea kodi zetu sio kitu cha ajabu kwao. Walichezea hela na kura zetu waliiba ndio maana mpaka leo matatizo yanatuandama. Ole wenu CCM laana ya Mungu itawafuata mpaka kwa vizazi vyenu.
 
Well written!Hii inaonesha ni jinsi gani alivyokuwa amejipanga kurudi magogoni kwa gharama yoyote ile,matokeo yake uchumi ukayumba na mpaka leo wameshindwa kuubalance tena.Jamani hivi ni nini tunasubiri,hatuna cha kupoteza tena kilichobak ni kuingia barabarani tu.Subira lazima iwe na mwisho!
 
everything it has got an end! and for the CCM their end will not be easy..they will be no mercy.. time is coming soon!
 
Sijajua vizuri kulikuwepo na uhusiano gani wa Kikazi kati yao, lakini tangu mnajimu Sheikh yahaya atutoke ni kama JK Amekosa mwelekeo kabisa????????!!!!!!!!?????????
 
Bahati mbaya JK siyo member humu.........na Salva(member) hatamwambia.......otherwise nice thread and message
 
ccm ni kama joka lenye sumu, wote tuligonge kichwa tuliue, tukishindwa litaendelea kututesa, hivi hamuoni kila leo matatizo lukuki? tunangoja nini? si tuingie bararani? yaani msekwa nae ni fisadi? ndo maana alishindwa kuwapa mapacha 3 barua, anajijua kuwa akiwapa leo kesho nae atapewa barua, watz tuache njaa tuipige chini ccm wote wezi, kvmamazao walah!
 
Well written!Hii inaonesha ni jinsi gani alivyokuwa amejipanga kurudi magogoni kwa gharama yoyote ile,matokeo yake uchumi ukayumba na mpaka leo wameshindwa kuubalance tena.Jamani hivi ni nini tunasubiri,hatuna cha kupoteza tena kilichobak ni kuingia barabarani tu.Subira lazima iwe na mwisho!

natamani watz wote wawe na ari kama hii, jk ana dharau sana!
 
Uongo kwa serikali ya kikwete ni jambo la kawaida na wala siwezi kushanga
 
Back
Top Bottom