JK: Hatutaki Rais mzee 2015

Sababu za kushusha umri zimeelezwa vizuri sana na kaka yetu January Makamba. Amesema wazee wameshindwa kuleta mabadiliko na wameishia kuleta uchawi tu Ikulu. Hapo labda alikuwa anamlenga Baba Mwanaasha.
Baba Mwanaasha, Zitto Kabwa, January Makamba......lao mja tuna jua wanacho kitaka....
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Does it make sense?kwanza ningeomba kujuzwa uzee unaanzia age gani?pili kuna umuhimu gani wa kukataa rais mzee na kung'ang'ania rais kijana wakati si mtendaji?mfano wa rais mzee mtendaji ni Satta wa Zambia,tatu Kikwete katoa kauli hiyo kama mtazamo wake au mtazamo wa chama chake au mtazamo wa watanzania?
 
Sasa kama ni kweli - alisema hivyo - na anaamini hivyo kwanini yeye mwenyewe na makamu wake wasijiuzulu sasa ili kutuondolea kutawaliwa na RAis Mzee?

Mm huwa naheshimu sana michango ya Mzee Mwanakijiji...lkn ktk hili nahisi hajamuelewa jk,kila zama zina kitabu chake mwaka 1995 na 2005 kwetu jk alikuwa kijana lkn kwa mwaka 2005 watu wa umri wake hatuwahitaji sana...Tunahitaji mawazo mapya ya kina January,Zitto,Mnyika,Nyalandu,Dr.Kigangwalla n.k
Sio tu mawazo mapya lkn pia muelekeo mpya wa Taifa letu.NAMUUNGA MKONO SANA J.K...yupo sahihi.
 
Katiba yetu imempa RAISI madaraka makubwa, kama haitabadilishwa kabla ya 2015, basi JK ana mwanya mkubwa wa kufanikisha atakacho si kwa faida ya TANZANIA kama nchi bali kwa faida azijuazo yeye mwenyewe. Nyerere alimkataa JK na ikawa, JK alitaka Spika mwanamke na ikawa, nk..........hii ndio TZ yetu.
Si aruhusiwe Mtanzania yeyote tu mwenye akili timamu ili agombee URAISI, sisi ndio tutaamua yupi anafaa - majority wins na ndio demokrasia. KATIBA ya CCM pia lazima iangalie watanzania wote kwa UJUMLA maana isije ikawa kama KATIBA ya MAKABURU - ohoo sijui sisi katiba yetu Makaburu inaruhusu mgombea kua MZUNGU TU na awe na Phd.
 
Watu hivi kikwete haruhusiwi kutoa maoni yake kama mtanzania?tuache kuwa na fixed minds......The Logic is,ni kwa nini umri wa kugombea urais uanzie miaka 40? Haya ni matusi kwa walio na umri chini ya miaka 40,ni matusi kwa watanzania kwamba busara za kuongoza zinaanzia umria wa miaka 40?

Halafu funny enough,sijui ni kwa nini watu wana-feel insecure statement ya kushusha umri wa urais inapotolewa.


Naunga mkono katika kujenga imani kwa vijana wenye uwezo sawa na kujenga imani kwa wazee wenye uwezo !
 
JK alipata URAISI akiwa kijana, kazeekea humohumo, hivi kaona katuletea maendeleo gani? Naamini kaona raisi wa nchi anazotembelea sana kama kwa CAMERON na kwa OBAMA - muda umefika sasa wa JK kutembelea BEIJING ili kuona makali ya RAISI wazee. Ujana ama Uzee si hoja, tunataka RAISI anayeweza KAZI.
 
Binafsi naamini katika kutumia kigezo kinachomfanya mtu aweze kupigiwa kura kuwa Mbunge ndio hichoo hicho kitumike kumpima anayetaka kuwa Rais. Miaka 18, anajua kusoma na kuandika, hajawahi kufungwa kwa muda uliowekwa na ana akili timamu. Wananchi wataamua wenyewe hayo mambo mengine. Kama tunaruhusu watu wa miaka 18 kuwa wabunge kwanini wasiweze kuwa Rais?


Fikra yako ya leo Mzee HAPANA
 
Ben kwanini basi iwe ni miaka 35? Hiyo siyo dharau kwa walio chini ya miaka hiyo? Kwanini tusiondoe tu minimum age requirement?

Itakuwa sarakasi! Kijana wa miaka kumi na tano hayaaaa, miaka saba hayaaaa.

Mkuu nadhani kuna hoja. Kama age limit basi iwe yule mwenye haki ya kupiga kura awe pia na haki ya kupigiwa kura katika maeneo yote kuanzia uenyekiti wa serikali za mtaa hadi Urais; hii itakuwa fair. Lakini pia ingekuwa vyema kuweka maximum limit ili kuepuka wale wazee ambao wakionja utamu wa ikulu kwenye umri mkubwa (excluding Mandela) huwa wanatamani wafie Ikulu (Wade). Maximum age ya kukutwa ikulu ingekuwa miaka 70 basi kwa maana nyingine maximum ya kugombea ingekuwa miaka 65.
 
watu hivi kikwete haruhusiwi kutoa maoni yake kama mtanzania?tuache kuwa na fixed minds......the logic is,ni kwa nini umri wa kugombea urais uanzie miaka 40? Haya ni matusi kwa walio na umri chini ya miaka 40,ni matusi kwa watanzania kwamba busara za kuongoza zinaanzia umria wa miaka 40?

Halafu funny enough,sijui ni kwa nini watu wana-feel insecure statement ya kushusha umri wa urais inapotolewa.


naunga mkono katika kujenga imani kwa vijana wenye uwezo sawa na kujenga imani kwa wazee wenye uwezo !

ukisema ni matusi kwa watanzania kwamba busara za kuongoza zinaanzia umri wa miaka 40 utakuwa umekosea. Je kama tukisema umri uwe ni miaka 35, wale wa chini ya 35 nao watasema ni matusi vile vile.
Kitu cha msingi hapa ni watanzania kukubaliana ni upi uwe umri wa mtu kuongembea urais. Tukishakubaliana kwenye katiba basi kila mtu atapibidi afuate hivyo.

Lakini lazima kuwa na sababu za msingi za kuchagua ni umri gani unafaa kwa mtu kuogombea urais. Kutoa tu hoja ya kuwa umri wa kugombea urais uwe miaka 35 au vipi bila sababu zenye mshiko itakuwa ni kama kupiga debe tu.

Kusuhu umri wa kupiga kura kuwa miaka 16, mimi hili napinga. Tunajua hapa tanzania mtu anatarajia kuwa na uwezo wa kufanya maamuzi ya kiutu uzima anapokuwa na miaka 18. Labda tubalishile hii sheria ya jumla kwanza kuhusu umri wa mtu kufanya maamuzi ya kiutu uzima. Lakini tunajua nini itakuwa madhara yake. Umri wa miaka 16 bado ni umri wa kitoto, na inajulikana hivyo sehemu nyingi dunia.

 
Nitampongeza Kikwete akiongoza vizuri mchakato wa Katiba Mpya. Haya ya umri wa mtu gani awe Rais wataamua Watanzania kwa kuangalia rekodi ya uchapa kazi,uzalendo wake kwa Tanzania na uwezo wa kuongoza. Kigezo cha umri ni hila za watu wanaotafuta uongozi kwa malengo binafsi.
 
Nina wasiwasi na ww kuna nini kati ya ww naEl. huyo ni mwizi

huyu radhia sweety ni kilaza wa kupitiliza,yaani kila post yake ni utumbo tu,kwanza anajua umri wa mwandosya na Lowassa?stupidity
 
Zitto Kabwe is presidential material. Watch this space

Yes he is ! He can totally change the attitudes,he can inspire and more importantly.......he can be the best Commander-in-chief ever.Zitto is a great leader with superb courage and deep sense of commitment and love for his people.

It's Only sickening the pathetic, lazy and backward mentality ...... JK ana haki ya kutoa mawazo yake.Kuna watu wanakosa kujiamini inapokuja suala la kuweka proper age na kupanua wigo wa kidemokrasia kuhusiana na umri wa kugombea urais.

It's very obvious uwezo wa mtu unapewa first priority na incase kuwe na watu wawili wenye uwezo sawa provided that all other factors are constant except age,then i will vote for the youngest candidate.People dont quote me wrong kama ilivyokuwa kwenye ile thread nyingine tena.
 
jk: Hatutaki rais mzee 2015

na nasra abdallah


amka2.gif

wakati makundi ya urais yakijipanga kuwania kiti hicho mwaka 2015, bila kuyajali, rais jakaya kikwete amesema wanaota urais wakiwa na umri kama wake, wasahau, tanzania daima jumatano limedokezwa.

Kikwete alitoa kauli hiyo wakati wa kikao cha kamati kuu ya chama cha mapinduzi (ccm), kilichokutana juzi, pamoja na mambo mengine, kupitisha jina la mgombea ubunge katika jimbo la arumeru mashariki.

Habari kutoka ndani ya kikao hicho zilisema kuwa rais kikwete alitoa kauli hiyo wakati akifungua kikao hicho.

Kwa mujibu wa habari hizo, rais kikwete alisema kuwa kinachotokea arumeru mashariki ni makundi yanayotaka urais na kusisitiza kuwa kama kuna mtu mwenye umri kama wake na anataka urais mwaka 2015, asahau kupata kiti hicho.

Alisisitiza kuwa wanaotajwa kutaka urais wakiwa na umri kama wake na hata kuzidi, huu si wakati wao bali wa vijana.

Mtoa habari wetu kutoka ndani ya kikao hicho, alisema kauli hiyo ya rais kikwete iliwanyong'onyeza baadhi ya makada wanaotajwa kutaka nafasi hiyo wakiwa tayari na umri mkubwa.

Katika hatua nyingine, mbunge wa bombuli, januari makamba (ccm), amependekeza kuwa umri wa kugombea urais, ushushwe kutoka miaka 40 ya sasa hadi 35.

Ushauri huo uliungwa mkono pia na mbunge wa kigoma kaskazini, zitto kabwe, ambaye alihoji kuwa kama uganda wameweza kwa nini tanzania mabadiliko hayo hayawezekani.

Makamba alitoa kauli hiyo jana katika kongamano la femina hip la vijana walio nje ya shule, lilioandaliwa na jukwaa la femina, huku likiwa limebeba mada kuu ya ushiriki wa vijana katika uundwaji wa katiba mpya na kufanyika katika ukumbi wa british council, jijini dar es salaam.

Wabunge hao wawili pia walitaka umri wa mtu kuruhusiwa kupiga kura uwe miaka 16 badala ya 18 kama ilivyo sasa.

Akifafanua pendekezo hilo, makamba alisema tanzania inapaswa kuiga mfano wa nchi jirani kama uganda, burundi na rwanda ambao tayari wanafuata mfumo huo.

Alisema asilimia kubwa ya wananchi wa taifa hili ni vijana hivyo haoni ni kwa nini hawapewi fursa kugombea nafasi hiyo kwa kisingizio cha umri.

Kuhusu kupiga kura, mbunge huyo alisema anaamini kwamba umri wa miaka 16 alionao kijana wa karne hii ana uwezo wa kuchambua mambo na kumchagua kiongozi anayeona anafaa.

Kwa upande wake zitto alisema hata yeye anaunga mkono hoja hiyo na kudai kwamba linawezekana kabisa huku akitolea mfano kwamba kipindi cha nyuma wanawake walikuwa hawashiriki katika kupiga kura.

Kama vile haitoshi alisema miaka ya kupiga kura ilikuwa ni kuanzia 21 lakini kadri muda ulivyozidi kwenda na kuonekana kwamba kuna haja ya sheria hiyo kufanyiwa marekebisho, ndipo ikafika miaka 18 hivyo ni wakati sasa muafaka kwa vijana kudai haki hiyo ya kupiga kura wakiwa na miaka 16.

Hata hivyo zitto aliwataka vijana katika mchakato huu wa katiba kutokubali mjadala huo utawaliwe na wanasiasa kwa kuwa wengi wanajadili kwa maslahi yao.

Kwa mujibu wa zitto tayari ameshaona wanasiasa hao wameanza kuutumia mjadala huo kwa manufaa yao huku wakilenga katika kugawana madaraka na kuacha kujadili mambo muhimu kama ajira kwa vijana na namna gani wataweza kulipwa kutokana na kazi wanazozifanya.

Pia mbunge huyo aliwaonya vijana wasije wakafikiri katiba mpya ndiyo itakuwa suluhu ya matatizo yanayowakabili na badala yake kuwataka wafanye kazi kwa bidii.

"msidhani kwamba eti katiba mpya ikiwepo ndipo matatizo ya ajira yatakwisha au uibwaji wa rasilimali za nchi utaisha la hasha kwani matatizo haya yanaweza kuendelea kuwepo; kinachotakiwa ni kuchapa kazi na kujenga hoja pale mambo wanapoyaona yanaenda sivyo," alisema.

Hata hivyo wabunge hao walipoulizwa swali na mmoja wa washiriki wa kongamano hilo, humphrey polepole, kama wangependa kuwa kwenye bunge maalum la katiba, walisema ndiyo kwa madai kwamba wanaamini watakuwa na mchango mkubwa kuwepo kwao katika tume hiyo.

Kwa pamoja wabunge hao walisema kwamba wanataka kuonyesha siasa za tofauti katika kuondoa matatizo ya vijana na wananchi kwa jumla bila kujali vyama wanavyotoka.

Katika kongamano hilo la siku mbili ambapo mgeni rasmi alikuwa meya wa manispaa ya ilala, jerry silaa, linalenga kupata maoni ya vijana wa tanzania kuhusu katiba mpya kwani takwimu zinaonyesha kwamba tanzania ina watu milioni 44 na kati ya hao asilimia 65 ni watu walio chini ya umri wa miaka 25.

Source: Tanzania daima. 29/feb/2012




kama kweli kikwete kasema wanataka urais wakiwa na umri kama wake basi wasahau, atakuwa anakiuka katiba ya nchi ambayo yeye aliapa kuilinda. Katiba ya jmt imeweka tu umri wa chini na haijaweka umri wa juu. Hivyo basi hata kama mtu ana miaka 100 ana haki ya kugombea kuwa rais wa jmt.

Haya mambo ya kutoa kauli za kibaguzi yanatakiwa yakome kabisa. Lazima tufuate sheria za nchi.

 
ukisema ni matusi kwa watanzania kwamba busara za kuongoza zinaanzia umri wa miaka 40 utakuwa umekosea. Je kama tukisema umri uwe ni miaka 35, wale wa chini ya 35 nao watasema ni matusi vile vile.
Kitu cha msingi hapa ni watanzania kukubaliana ni upi uwe umri wa mtu kuongembea urais. Tukishakubaliana kwenye katiba basi kila mtu atapibidi afuate hivyo.

Lakini lazima kuwa na sababu za msingi za kuchagua ni umri gani unafaa kwa mtu kuogombea urais. Kutoa tu hoja ya kuwa umri wa kugombea urais uwe miaka 35 au vipi bila sababu zenye mshiko itakuwa ni kama kupiga debe tu.

Kusuhu umri wa kupiga kura kuwa miaka 16, mimi hili napinga. Tunajua hapa tanzania mtu anatarajia kuwa na uwezo wa kufanya maamuzi ya kiutu uzima anapokuwa na miaka 18. Labda tubalishile hii sheria ya jumla kwanza kuhusu umri wa mtu kufanya maamuzi ya kiutu uzima. Lakini tunajua nini itakuwa madhara yake. Umri wa miaka 16 bado ni umri wa kitoto, na inajulikana hivyo sehemu nyingi dunia.


Mkuu hilo suala la kushusha voting age nakubaliana nalo...naamini mtanzania aanweza kufanya maamuzi sahihi hata akiwa na 15 years.To be safe,tushushe umri wa kum-define mtu mzima constitutionally.

Nataka vigezo vilivyotumika kuweka umri wa mgombea urais kuwa 40 ili tufanye very health debate.Pia naona ni vizuri tuka-review umri wa mtu kuwa mtu mzima!
 
To me age doesnt matter as long as ni mtu mzima mwenye proven records za utendaji mzuri na afya iliyosimama anafaa kuwa raisi.
Nsije sahau asiwe na kashfa yoyote ile!
 
Mkishusha umri wa kugombea urais hadi miaka 35 itakuwa ni dharau kubwa sana kwa sisi wenye miaka 25.
 
Back
Top Bottom