JK: Hatutaki Rais mzee 2015

Nteko Vano

JF-Expert Member
Feb 28, 2012
434
111
JK: Hatutaki Rais mzee 2015

Na Nasra Abdallah

amka2.gif
WAKATI makundi ya urais yakijipanga kuwania kiti hicho mwaka 2015, bila kuyajali, Rais Jakaya Kikwete amesema wanaota urais wakiwa na umri kama wake, wasahau, Tanzania Daima Jumatano limedokezwa.

Kikwete alitoa kauli hiyo wakati wa kikao cha Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM), kilichokutana juzi, pamoja na mambo mengine, kupitisha jina la mgombea ubunge katika jimbo la Arumeru Mashariki.

Habari kutoka ndani ya kikao hicho zilisema kuwa Rais Kikwete alitoa kauli hiyo wakati akifungua kikao hicho.

Kwa mujibu wa habari hizo, Rais Kikwete alisema kuwa kinachotokea Arumeru Mashariki ni makundi yanayotaka urais na kusisitiza kuwa kama kuna mtu mwenye umri kama wake na anataka urais mwaka 2015, asahau kupata kiti hicho.

Alisisitiza kuwa wanaotajwa kutaka urais wakiwa na umri kama wake na hata kuzidi, huu si wakati wao bali wa vijana.

Mtoa habari wetu kutoka ndani ya kikao hicho, alisema kauli hiyo ya Rais Kikwete iliwanyong'onyeza baadhi ya makada wanaotajwa kutaka nafasi hiyo wakiwa tayari na umri mkubwa.

Katika hatua nyingine, Mbunge wa Bombuli, Januari Makamba (CCM), amependekeza kuwa umri wa kugombea urais, ushushwe kutoka miaka 40 ya sasa hadi 35.

Ushauri huo uliungwa mkono pia na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, ambaye alihoji kuwa kama Uganda wameweza kwa nini Tanzania mabadiliko hayo hayawezekani.

Makamba alitoa kauli hiyo jana katika kongamano la Femina HIP la vijana walio nje ya shule, lilioandaliwa na Jukwaa la Femina, huku likiwa limebeba mada kuu ya ushiriki wa vijana katika uundwaji wa Katiba mpya na kufanyika katika Ukumbi wa British Council, jijini Dar es Salaam.

Wabunge hao wawili pia walitaka umri wa mtu kuruhusiwa kupiga kura uwe miaka 16 badala ya 18 kama ilivyo sasa.

Akifafanua pendekezo hilo, Makamba alisema Tanzania inapaswa kuiga mfano wa nchi jirani kama Uganda, Burundi na Rwanda ambao tayari wanafuata mfumo huo.

Alisema asilimia kubwa ya wananchi wa taifa hili ni vijana hivyo haoni ni kwa nini hawapewi fursa kugombea nafasi hiyo kwa kisingizio cha umri.

Kuhusu kupiga kura, mbunge huyo alisema anaamini kwamba umri wa miaka 16 alionao kijana wa karne hii ana uwezo wa kuchambua mambo na kumchagua kiongozi anayeona anafaa.

Kwa upande wake Zitto alisema hata yeye anaunga mkono hoja hiyo na kudai kwamba linawezekana kabisa huku akitolea mfano kwamba kipindi cha nyuma wanawake walikuwa hawashiriki katika kupiga kura.

Kama vile haitoshi alisema miaka ya kupiga kura ilikuwa ni kuanzia 21 lakini kadri muda ulivyozidi kwenda na kuonekana kwamba kuna haja ya sheria hiyo kufanyiwa marekebisho, ndipo ikafika miaka 18 hivyo ni wakati sasa muafaka kwa vijana kudai haki hiyo ya kupiga kura wakiwa na miaka 16.

Hata hivyo Zitto aliwataka vijana katika mchakato huu wa Katiba kutokubali mjadala huo utawaliwe na wanasiasa kwa kuwa wengi wanajadili kwa maslahi yao.

Kwa mujibu wa Zitto tayari ameshaona wanasiasa hao wameanza kuutumia mjadala huo kwa manufaa yao huku wakilenga katika kugawana madaraka na kuacha kujadili mambo muhimu kama ajira kwa vijana na namna gani wataweza kulipwa kutokana na kazi wanazozifanya.

Pia mbunge huyo aliwaonya vijana wasije wakafikiri Katiba mpya ndiyo itakuwa suluhu ya matatizo yanayowakabili na badala yake kuwataka wafanye kazi kwa bidii.

"Msidhani kwamba eti Katiba mpya ikiwepo ndipo matatizo ya ajira yatakwisha au uibwaji wa rasilimali za nchi utaisha la hasha kwani matatizo haya yanaweza kuendelea kuwepo; kinachotakiwa ni kuchapa kazi na kujenga hoja pale mambo wanapoyaona yanaenda sivyo," alisema.

Hata hivyo wabunge hao walipoulizwa swali na mmoja wa washiriki wa kongamano hilo, Humphrey Polepole, kama wangependa kuwa kwenye Bunge Maalum la Katiba, walisema ndiyo kwa madai kwamba wanaamini watakuwa na mchango mkubwa kuwepo kwao katika tume hiyo.

Kwa pamoja wabunge hao walisema kwamba wanataka kuonyesha siasa za tofauti katika kuondoa matatizo ya vijana na wananchi kwa jumla bila kujali vyama wanavyotoka.

Katika kongamano hilo la siku mbili ambapo mgeni rasmi alikuwa Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa, linalenga kupata maoni ya vijana wa Tanzania kuhusu Katiba mpya kwani takwimu zinaonyesha kwamba Tanzania ina watu milioni 44 na kati ya hao asilimia 65 ni watu walio chini ya umri wa miaka 25.

Source: Tanzania Daima. 29/Feb/2012

Waandishi wa kibongo article nzima haina direct quote kuonyesha alivyosema Kikwete verbatim kuhusiana na main topic.

Makala inatuacha tunauliza kama kweli Kikwete kasema hivyo, na kwa context gani.

Kama kasema kweli.

Kikwete kaambiwa na nani kwamba Watanzania hawataki rais "Mzee"?

Au yeye ndiye anataka kuwachagulia Watanzania rais?

Rais haoni kwamba anawagawanya Watanzania katika makundi, vijana na wazee, badala ya kuwaunganisha wote?

Rais haoni kwamba anataka kuwanyima wazee haki yao ya kikatiba ya kugombea uongozi?

Rais haoni kwamba anawavunjia wazee heshima kinyume na mila za kiafrika zinazoheshimu wazee?
 
Katika historia ya Tanzania huru hakuna wakati ambapo wanawake walikuwa hawashiriki kupiga kura; na hakuna sababu ya msingi ya kushusha umri wa kuanza kupiga kura kuja miaka 16. Upigaji kura ni uamuzi wa mtu mzima na tunayo universal suffrage. Kama tunaamini mtoto wa miaka 16 anaweza kufanya uamuzi mkubwa wa kupiga kura basi tushushe universal suffrage ije kwenye 16 ili wenye umri huo waweze kufanya maamuzi mengine ya watu wazima - kuoa, kushtakiwa kama watu wazima, n.k n.k kwanini tushushe tu kwenye kupiga kura?

Hili la kushusha umri wa kugombea Urais kutoka 40 kuja 35 kunaweza kuwa kuzuri lakini kusihusu uchaguzi wa 2015 liwe kwa ajili ya uchaguzi wa 2020. Lakini wakiamua kuondoa hilo waondoe pia ulazima wa kuwa na shahada ya kwanza kwa mgombea wa Urais! Kwanini ni lazima mtu awe na shahada kuwa rais? kwani Urais ni kazi ya usomi?
 
tatizo ni kuwa kipimo hicho kinachotumiwa sana siku hizi cha "uzee" tukikileta kwake yeye mwenyewe atang'aka. Kama mzee hawezi kuwa rais 2015 kwanini mzee awe rais 2012? Na tatizo la uongozi Tanzania halijawahi kuwa umri!
 
Katika historia ya Tanzania huru hakuna wakati ambapo wanawake walikuwa hawashiriki kupiga kura; na hakuna sababu ya msingi ya kushusha umri wa kuanza kupiga kura kuja miaka 16. Upigaji kura ni uamuzi wa mtu mzima na tunayo universal suffrage. Kama tunaamini mtoto wa miaka 16 anaweza kufanya uamuzi mkubwa wa kupiga kura basi tushushe universal suffrage ije kwenye 16 ili wenye umri huo waweze kufanya maamuzi mengine ya watu wazima - kuoa, kushtakiwa kama watu wazima, n.k n.k kwanini tushushe tu kwenye kupiga kura?

Hili la kushusha umri wa kugombea Urais kutoka 40 kuja 35 kunaweza kuwa kuzuri lakini kusihusu uchaguzi wa 2015 liwe kwa ajili ya uchaguzi wa 2020. Lakini wakiamua kuondoa hilo waondoe pia ulazima wa kuwa na shahada ya kwanza kwa mgombea wa Urais! Kwanini ni lazima mtu awe na shahada kuwa rais? kwani Urais ni kazi ya usomi?

Mkuu hayo ni maoni ya Zito na January..halafu umri wa kugombea urais uko kwenye katiba ya nchi,lakini ulazima wa kuwa na shahada ya chuo kikuu au elimu inayofanana na hiyo,uko kwenye katiba ya ccm,kama kumbukumbu zangu ziko sawa na ndiyo maana hata Mbowe aliwahi kugombea urais.Labda January apeleke hii hoja kwenye vikao vyao vya chama.
Halafu kwanini unadhani umri wa kugombea urais wa miaka 35,usihusu uchaguzi ujao,tusubiri mpaka 2020?
 
Kiranga,'
Naona ameisema kwenye context ya mkutano wa CCM. Hiyo ni kauli inayowahusu CCM peke yao. Wasituamulie sisi Watanzania tusio ndani ya CCM ni rais wa aina gani au mwenye umri gani tunayemtaka.
 
Kiranga,'
Naona ameisema kwenye context ya mkutano wa CCM. Hiyo ni kauli inayowahusu CCM peke yao. Wasituamulie sisi Watanzania tusio ndani ya CCM ni rais wa aina gani au mwenye umri gani tunayemtaka.

Nominee wa CCM ndiye mara zote anayekuja kuwa Rais wa Tanzania.
 
Kiranga,'
Naona ameisema kwenye context ya mkutano wa CCM. Hiyo ni kauli inayowahusu CCM peke yao. Wasituamulie sisi Watanzania tusio ndani ya CCM ni rais wa aina gani au mwenye umri gani tunayemtaka.

Wazee wa CCM nao ni raia wa Tanzania wenye haki za kikatiba za Mtanzania, sasahaoni hii kauli ni unconstitutional?

Leo tutasema hatutaki wazee kesho nani? Wachagga?
 
Wazee wa CCM nao ni raia wa Tanzania wenye haki za kikatiba za Mtanzania, sasahaoni hii kauli ni unconstitutional?

Leo tutasema hatutaki wazee kesho nani? Wachagga?
You are right. Lakini haki za kikatiba za wana CCM zisiwe haki za kikatiba za Watanzania wengine.
 
If it takes a 99 years old great grandfather/mother to fix this country let it be. Tatizo lililopo sio umri wa rais, ni uongozi mbovu. Hivyo hizi kauli za uzee na ujana na madharau kwa watanzania.

Hoja ya January Makamba na Zito Kabwe kuhusu kuiga Uganda na kushusha umri wa mgombea urais toka miaka 40 to 35 inaweza kutuletea matatizo. Uganda sio nchi ya kuiga kabisa when it comes to governace system. Museven is a classic example of a 'democratically' elected dictactor, sisi tunataka kuiga nini kwake? Kabadilisha katiba na kuwa rais wa maisha, na watu wanajua sababu kuu iliyomsukuma Museven kushusha umri wa kugombea urais na yeye kuendelea kuwa kwenye hicho kiti ni ili mwanae arithi.

Sababu za kuweka umri wa miaka 40 zinajulika - kukomaa (mawazo, uzoefu etc), sasa sababu za kushusha na kufikia umri wa miaka 35 ni zipi?
 
Nominee wa CCM ndiye mara zote anayekuja kuwa Rais wa Tanzania.

Kwa iliyokuwa ccm,lakini siyo ccm hii ya sasa.Nominee wa ccm 2015,siyo lazima aje kuwa Rais.Chukulia kwa mfano anayeandaliwa mazingira haya ni Mwinyi.Je huko ccm hao wazee wanaotaka kuondolewa kwa zengwe,watakubali kumpisha na kum support?chadema au chama kingine kikipitisha mgombea 'nguli',Mwinyi ana ubavu wa kusimama nae?
Yaliyotokea Kenya(KANU) ndiyo yatakayotokea Tannzania(ccm) mwaka 2015!
 
Hiyo ndiyo imekuwa kawaida. Lakini naamini hali hiyo haitaendelea milele. Uchaguzi wa 2010 umedhihirisha hilo.

Uchaguzi wa 2010 umedhihirisha nini? Tusidanganyane hapa. Ukweli ni kuwa Chadema ina safari isiyo na mwisho kabla ya kuchukua urais.
 
Back
Top Bottom