JK hali hii mpaka lini?

Fidel80

JF-Expert Member
May 3, 2008
21,947
4,444
_hamnamadawati.jpg

Mwalimu mkuu msaidizi wa shule ya msingi Kunzugu iliyopo tarafa ya Serengeti, wilayani Bunda , Seus Mogasa akiwafundisha wanafunzi wa darasa la sita wakiwa wamekaa chini. Zaidi wanafunzi 400 wa shule hiyo hawana madawati.
 
Inasikitisha sana kuona watoto wa wapiga kura wako wanakaa chini huku wakiendelea kusubili Maisha bora kwa kila Mtanzania ndo kama hivi sasa imekuwa ni ndoto za mchana bora ya hawa darasa limepakwa rangi ila wale wa shule ya Namtumbo ya nyasi ni aibu sana kwa Taifa. Kama imeshindikana basi tembezeni bakuri kwa ajili ya kusaidia shule hizi hiki ni kizazi ni nguvu kazi ya Taifa la kesho.
Punguzeni blah blah nyiiingi tunataka matendo mnatulostisha kwakweli.
 
Elimu ikiendelewa kuchukuliwa kirahisi rahisi kwenye level ya University, huku shule za chini lazima waonje joto ya jiwe.Hakuna mpango endelevu wa kuongeza idadi ya wasomi watakao add value kwenye jamii yetu. Tunasoma soma tu ili mradi tunasoma na sishangai kuona tukijisifu kuingiza idadi kubwa ya wanafunzi shuleni, bila kujari wanasomaje na wanasoma nini.
Bado suala la elimu linaenda kimtindo mtindo tu. Tunasahau kuwa dunia tuliyonayo bila elimu ya kutosha tutaendelea kuburuzwa mpaka tukome.
 
Inasikitisha sana kuona watoto wa wapiga kura wako wanakaa chini huku wakiendelea kusubili Maisha bora kwa kila Mtanzania ndo kama hivi sasa imekuwa ni ndoto za mchana bora ya hawa darasa limepakwa rangi ila wale wa shule ya Namtumbo ya nyasi ni aibu sana kwa Taifa. Kama imeshindikana basi tembezeni bakuri kwa ajili ya kusaidia shule hizi hiki ni kizazi ni nguvu kazi ya Taifa la kesho.
Punguzeni blah blah nyiiingi tunataka matendo mnatulostisha kwakweli.
Tatizo ni baba na mama za hao watoto ikifika wanapigiwa makelele kila siku wachague viongozi wanaojali maendeleo yao lakini ikifika wakati wa uchaguzi mbio...wanapeleka kura zao kwa mafisadi...wanavuna walichopanda and as long as the mentality in this country remains like this such schools will never cease to be present and we will keep on hearing and seeing the same or even worse situations......
 
Tatizo ni baba na mama za hao watoto ikifika wanapigiwa makelele kila siku wachague viongozi wanaojali maendeleo yao lakini ikifika wakati wa uchaguzi mbio...wanapeleka kura zao kwa mafisadi...wanavuna walichopanda..

Sasa mkuu hapo nini kifanyike? Tuwaache wazazi wa hawa watoto waendelee kufanya wanavyo fanya au tuwasaidieje?
 
Kuna jambo moja ambalo mimi huwa nalishangaa sana na sipati jibu kabisa! Sijui priorities za serikali zetu huwa ni nini?? Sitaki kuilaumu serikali ya JK peke yake, hata ya Mkapa, Mwinyi na hata Nyerere. Inakuwaje ni vigumu kutengeneza madawati ya kutosheleza nchi nzima? Hivi yanaweza kugharimu shilingi ngapi za Kitanzania!! Mbona tunaweza kutengeneza mabarabara hata yasiyozalisha kitu. Embu iangalie masaki na oysterbay, si imejaa barabara za lami! walikuwa wanahitaji hizo barabara za lami kwa maisha yao kweli? lakini hawa watoto wa watanganyika wanaokaa chini wanahitaji elimu kwa ajili ya maisha yao. Leo mifuko yote ya pensheni inaidai serikali kwa ajili ya kujenga university of Dodoma, kwanini serikali isidaiwe na mifuko hiyo kwa ajili ya ku supply madawati mashuleni. kama mifuko ya pensheni imechoka basi mabenki!! Ni jambo la kushangaza sana na utakuwa wilaya ina madiwani, mwenyekiti wa halmashauri au meya wa mji au jiji lakini kuna wanafunzi wanakaa chini. Kuna wakurugenzi wenye digrii lakini hawawezi kubuni njia za kuzipatia halmashauri mapato zaidi ya makusanyo kutoka kwa wananchi. Sijui tuchapwe viboko kidogo
 
Matokeo ya UFISADI na matumizi mabaya ya fedha za umma! nenda hospitalini ingia wodini utafikiri wagonjwa wametupwa! kumbe la, matajiri hupata huduma nzuri za usafiri, tiba, shule n.k. kama kweli BUNGE linajipanga kulinda mafisadi, DHAMBI hii tutaitubu wapi? CCM sasa hivi haileti amani bali inaandaa wananchi kupigana vita, maana mtu mwenye njaa hana NIDHAMU!
 
Haya ndiyo matunda ya UFISADI, nenda pia hospitali utadhani wagonjwa wametupwa kumbe wamelazwa sehemu inayoitwa ya huduma ya AFYA!, huduma za maji pamoja na mito mikubwa mingi ambayo ni hazina kubwa kwa taifa! huduma hizi MAFISADI wao huzipata kwa gharama yoyote ili mradi tu kama zipo hapa chini ya jua.

Kama kweli BUNGE linajiandaa kuwalinda MAFISADI hii ni balaa, maana CCM hapa tena haidumishi amani bali inaandaa wananchi kupigana vita, maana kusema kweli sasa hivi hali si shwari, ukiona mabango ya maandamano kuongea na mtu mmoja mmoja utajua kabisa sasa hivi hakuna amani bali kuna utulivu tu, kila mtu kakaa hapigani lakini moyo unauma!

JK kama kweli anapiga vita ufisadi sina hakika maana viashiria vinaonyesha chama kime-nunuliwa.

Tusubiri
 
Back
Top Bottom