RealMan
JF-Expert Member
- Nov 9, 2010
- 2,367
- 1,388
As usual, CIVIC UNITED FRONT walking the walk while Chonga Domo Milele keep talking the talk. Jitihada hizi za wanamapinduzi hawa wa CUF zimeshaionyesha Dunia nzima kwamba Tanzania mambo siyo mambo. Wakati phd's Chonga Domo Milele wao wanaendelea kunywa pombe tuu na kudai katiba mpya kwenye kompyuta.
Nancy!!!
Tusishangilie kwa kitu ambacho hakipo bado. Maandamano kuonyeshwa EuroNews ni mwanzo mzuri lakini kusudio si kuonekana huko wala CNN bali kupata katiba mpya. Na wala hakuna mwenye kusema mwisho wa siku kwamba yeye ndo ameleta mabadiliko haya. Kwa kadri tunavyotaka kupata ujiko wa nani mwanaume ndio kwa kiwango hicho pia tunapoteza lengo la uhitaji wetu.
Kina Mvungi waliwahi kutengeneza rasimu ya Katiba kama ambavyo CUF wameandaa rasimu, Waislam pia wanataraji kufanya hivyo, tumesikia Tahliso wako mbioni pia, Mnyika na hoja binafsi, Prof Shivji aliandika sana juu ya katiba tokea 1995. Hakuna katika hawa anaweza kusema yeye ndio injini ya harakati hizi.
Wengi wetu hapa tumekwisha sema, haijalishi nani anaunga mkono harakati hizi (Mkapa, Chiligati, Samatta, Bomani etc) na kwa mbinu gani, sie tunaangalia end result. Na kwamba kila mmoja wetu kwa nafasi yake anatakiwa kusababisha/kuleta/kueneza elimu hii kwa mwenzake. What we need is a New Constitution!!!
Tuacheni hii tabia ya kuzodoana kana kwamba kundi moja ndio litaleta mabadiliko haya, tunahitajiana sasa kuliko wakati mwingine wowote. Harakati hizi zinahusu wanazuoni, viongozi wa dini, vyama vya siasa, NGOs, makundi ya wafanyakazi, wanafunzi, wakulima, wanaharakati n.k.
Nancy naamini hukuwa mmoja wa waandamanaji, kwa msingi huo hukupigwa na pengine hujawahi pigwa mabomu ya mchozi na maji washa. Na hata kama umewahi kuandamana bado huna haki ya kubeza mchango wa anayehubiri kanisani/msikitini au kutumia komputa kudai katiba mpya.
Au unataka CDM nao waseme CUF hawakuwa "wanaume" kiasi cha kushindwa kushinikiza wabunge wao walioporwa ushindi kutangazwa washindi ktk mikoa ya Lindi na Mtwara tofauti na wenzao CDM walivyofanya/komaa Kawe, Ubungo, Mbeya, Mwanza, Arusha etc
Nachukia tunapotukuza u-CDM au u-CUF juu ya madai yetu ya msingi ambayo ni New Constitution na New NEC.
Pamoja tutafika!!!!!