Jk azidi kuandika historia

Lilombe

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
242
39
Rais Jakaya Kikwete amezidi kuandika historia katika kipindi chake cha uongozi kwa kuhitimisha kesi ya EPA ambayo kada wa CCM, Rajabu Maranda na \mshirika wake, Farijala wamepewa hukumu ya miaka 21 ambapo watatumikia jela miaka 5. Pia wakitoka jela itatakiwa walipe fedha walizoiba kupitia akaunti ya EPA.

Wananchi wa Tanzania pasipo kujali itikadi inatubidi kupongeza Rais wetu ili tumpe moyo ili aweze kuwashughulikia mafisadi na maovu mengine yanayofanyika nchini mwetu.

Tujikumbushe baadhi ya hatua ambazo JK amethubutu kuchukua katika uongozi wake:-
1. Kuvunja Baraza la Mawaziri ikiwa ni kujiuzulu kwa Waziri Mkuu
2. Kuwafikisha mahakamani viongozi wandamizi wa serikali; Mramba, Yona na Mgonja
3. Kuwapeleka watuhumiwa wa EPA mahakamani
4. Kuwa na moyo wa uvumilivu kwa vyombo vya habari
5. Kutoa vibali vya maandamano kwa vyama vya siasa pasiipo mkomo

NAWAKILISHA

Ukitumia bange shurti ule kwanza!!!!!!
 
Lilombe,

Wakili wa Washtakiwa masaa nane yaliyopita amesema kwamba bado hajasoma/hajaipitia ile hukumu maana ni ndefu sana, sasa wewe umeipitia saa ngapi na kuanza kutoa "sifa"?

Pili, inakuwaje unamhusisha JK na kazi za Mahakama?
 
Hayo amefanya kikwete sasa na aliyo fanya Slaa ni yapi zaidi ya kupiga domo?
 
Slaa atapongezwa kwa kuratibu maandamano yasiyo na kikomo HATAHIVYO inabidi ampongeze JK kwa kumpa uhuru wa kuandamana
 
Naona hawa walioshindwa kulivua gamba wamemwaga kwa wingi leo hapa kama kumbikumbi! ili kuja kuandika upupu wa Chama Cha Mafisadi.
 
Lilombe a.k.a Tamu unaboa na inaelekea wewe ni mwanamagamba. Acha kutuudhi kwa mizaha afanyayo mwanamagamba mwenzio JK. Hao waliohukumiwa ni danganya toto tu...alitakiwa ahukumiwe kikwete na chama cha magamba kwa kuiba hela hizo kwa ajili ya uchaguzi.
 
Historia ipi? hiyo hela waliyoiba si ndio ilizunguka kumweka JK madarakani na chenji iliobaki mgao wake ukagoma na dili kubumburuka? wadangayika kweli tuna akili za kuku hakyanani.
 
Na wewe umetumwa na nani? waiba kodi?

Nakuonea huruma sana kuja hapa na kutetea ufisadi na dhuluma kubwa zinazofanywa dhidi ya Watanzania. Inaelekea nawe ama ni fisadi au unanufaika kwa namna moja au nyingine na ufisadi huo ndio unaandika upupu wako kutetea chama cha mafisadi, lakini ukae ukijua kila jambo lina mwisho wake. Na mwisho wa chama cha mafisadi wala hauko mbali.
 
JK no at all
i reserve my comment on this stupid prezidaa isije ikawa
Una uhuru wa kutumia demokrasia utakavyo, UKWELI unabaki pale pale JK kapaisha demokrasia TZ na vyombo vya dola amewapa uhuru wa kutekeleza majukumu yake
 
Nakuonea huruma sana kuja hapa na kutetea ufisadi na dhuluma kubwa zinazofanywa dhidi ya Watanzania. Inaelekea nawe ama ni fisadi au unanufaika kwa namna moja au nyingine na ufisadi huo ndio unaandika upupu wako kutetea chama cha mafisadi, lakini ukae ukijua kila jambo lina mwisho wake. Na mwisho wa chama cha mafisadi wala hauko mbali.
Sasa kama kila kitu kina mwisho wake basi kwanini iwe CCM na sio chadema? l bora mafisadi kuliko chama chenye nia ya kuchafua nchi.
 
Bora nchi ichafuke tujue moja kuliko masultan wachache kudhania hii nchi wamerithishwa wao na Mungu na sisi wengine ni watumwa wao. Hapana, kama soo na iwe soo tu.
 
Una uhuru wa kutumia demokrasia utakavyo, UKWELI unabaki pale pale JK kapaisha demokrasia TZ na vyombo vya dola amewapa uhuru wa kutekeleza majukumu yake

Kama unapumba kiasi hiki usijibu post zangu nitokee tafadhali
 
Back
Top Bottom