JK aziba nafasi iliyokuwa ya Balozi Ombeni

Indume Yene

Platinum Member
Mar 17, 2008
2,950
711
Rais JK amemteua balozi T. Manongi kuziba nafasi iliyokuwa ya balozi Ombeni Umoja wa Mataifa. Ninakuwa na wasiwasi na huu uteuzi hasa baada ya Mama Migiro kutembelea ikulu juzi tu halafu msaidizi wake anapelekwa tena huko...just curious.

attachment.php
 
Attachments

  • Manongi.JPG
    Manongi.JPG
    74.3 KB · Views: 990
Mh.Rais mbona mimi ni mwanadiplomasia niliyekomaa na Mh.Nanii alikupenyezea jina langu afu huyo kaniwahi? VP MIMI NI LINI?
 
WEDNESDAY, JULY 25, 2012

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Balozi Tuvako Manongi kuwa Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, New York.

Taarifa iliyotolewa leo, Jumatano, Julai 25, 2012 na Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi, Bwana Peniel Lyimo kupitia Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Dar es Salaam imesema kuwa uteuzi huo ulianza jana, Julai 24, 2012.

Kabla ya uteuzi wake, Balozi Manongi ambaye ni ofisa wa miaka mingi wa masuala ya nchi za nje, alikuwa Mshauri Mwandamizi katika Ofisi ya Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, New York.

Balozi Manongi anachukua nafasi ya Balozi Ombeni Y. Sefue ambaye aliteuliwa kuwa Katibu Mkuu Kiongozi Desemba 30, mwaka jana, 2011.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
25 Julai, 2012

Rais JK amemteua balozi T. Manongi kuziba nafasi iliyokuwa ya balozi Ombeni Umoja wa Mataifa. Ninakuwa na wasiwasi na huu uteuzi hasa baada ya Mama Migiro kutembelea ikulu juzi tu halafu msaidizi wake anapelekwa tena huko...just curious.

attachment.php

mimi naamini balozi manongi anaweza kujisimamia mwenyewe bila kubebwa kuipata hiyo nafasi.
hongera zake sana na natumaini atazidi kuwajibika vilivyo.
 
Mie sijaelewa hapo panaposema Mwakilishi wa kudumu!!!Ina maana hadi kifo kimtenganishe na hicho cheo?
 
Mie sijaelewa hapo panaposema Mwakilishi wa kudumu!!!Ina maana hadi kifo kimtenganishe na hicho cheo?

Huyu Balozi kateuliwa kuwa "Mwakilishi wa Kudumu" U.N. Kwa kawaida cheo hiki ni cha kibalozi (ndio maana wanapewa watu waliopata ubalozi) lakini si ubalozi kwa sababu ili uwe balozi inabidi upeleke credentials kwa "Head of State", sasa kwa sababu unapoteuliwa kuwakilisha nchi yako Umoja wa Mataifa hupeleki credentials kwa "Head of State", huwi "Tanzania's Ambassador to the UN" bali unakuwa "Tanzania's Permanent Representative to the UN". Wengine, kama Dr. Mahiga, wanakuwa "and Minister Plenipotential"

Ndiyo maana hatuna Embassy UN, tuna "Permanent Mission of the United Republic of Tanzania to the United Nations".

Mwakilishi wa kudumu ana mamlaka ya kiserikali kutoa matamshi na kufanya maamuzi ya kiserikali bila kupata maagizo kama itabidi kufanya hivyo.

Ni ulimbwende wa itifaki za diplomasia.
 
Mie sijaelewa hapo panaposema Mwakilishi wa kudumu!!!Ina maana hadi kifo kimtenganishe na hicho cheo?

Hata mimi najiulizaga hivyo hivyo!

Kwa nini aitwe "mwakilishi wa kudumu"? Picha ninayopata mimi ni kwamba atadumu huko UN mpaka atakapokufa!!

Anaweza kabisa kuitwa 'mwakilishi wa Tanzania kwenye/katika umoja wa mataifa' bila kuweka hiyo "kudumu" na ikaeleweka vizuri kabisa pasipo na utata wowote ule.
 
Hata mimi najiulizaga hivyo hivyo!

Kwa nini aitwe "mwakilishi wa kudumu"? Picha ninayopata mimi ni kwamba atadumu huko UN mpaka atakapokufa!!

I suspect imekuwa convention siku nyingi hata wenyewe ukiwauliza wanaweza kushindwa kukuelezea.

Mi naona wanatofautisha tu kati ya "Balozi" (ambaye naye strangely ni Muwakilishi wa Kudumu) na "Muwakilishi wa Kudumu" (ambaye naye almost always ni balozi by rank) kwa maana ya kwamba balozi anapeleka credentials kwa Head of State na Muwakilishi wa Kudumu ni kwa UN organizations au NATO/EU/AU na kwa hivo hapeleki hati kwa Mkuu wa Nchi.
 
I suspect imekuwa convention siku nyingi hata wenyewe ukiwauliza wanaweza kushindwa kukuelezea.

Mi naona wanatofautisha tu kati ya "Balozi" (ambaye naye strangely ni Muwakilishi wa Kudumu) na "Muwakilishi wa Kudumu" (ambaye naye almost always ni balozi by rank) kwa maana ya kwamba balozi anapeleka credentials kwa Head of State na Muwakilishi wa Kudumu ni kwa UN organizations au NATO/EU na kwa hivo hapeleki hati kwa Mkuu wa Nchi.

Tatizo ni neno "kudumu" linapotumika kwa huyo mwakilishi.

Kudumu maana yake ni kuendelea kuishi au kuwepo kwa muda wote.

Katika umoja wa mataifa nadhani uanachama wetu labda ndiyo wa kudumu lakini si hao watu au huyo mtu anayetuwakilisha. Yeye huwa hadumu.

Wanapotumia "mwakilishi wa kudumu" kumuelezea mtu atakayetuwakilisha huko wanazua utata kidogo.

NB: Halafu hiyo "muwakilishi" ni Kiswahili cha wapi hicho? Maana Kamusi ya Kiswahili Sanifu ya Oxford toleo la pili iliyochapishwa mwaka 2012 na kamusi ya TUKI chapa ya tano iliyotolewa mwaka 2010 zote zina "mwakilishi"....
 
Muwakilishi cha kwetu Mrima, mwakilishi cha Unguja.

Ukienda Mayotte huko utasikia kingine cha ajabu zaidi utasema si Kiswahili hiki.

Hiyo habari ya "Muwakilishi wa Kudumu" inazama katika historia ya diplomasia.Kulikuwa na wawakilishi wa kutumwa mara moja.Rais/ mfalme anamtuma muwakilishi kwenda kwenye nchi fulani kwa sababu maalum, ama kutuma ujumbe fulani ama kuhudhuria kikao fulani.

Zilipokuja habari za kuwa na haja ya kuwa na ubalozi, na kuwa na balozi ambaye badala ya kutumwa kwa mara moja, anakaa kabisa katika mji wa nchi ya kigeni kama muwakilishi wa serikali yake, hapo ndipo pakatokea habari ya "muwakilishi wa kudumu".

Muwakilishi wa kudumu haina maana kwamba hatoki mpaka kifo.
 
Basi kama hatoki mpaka kifo huyo si mwakilishi wa kudumu. Ni mwakilishi tu huko Umoja wa Mataifa.

Au ni bora hata angeitwa mwakilishi mkazi (resident representative) kuliko mwakilishi wa kudumu maana anakaa kabisa huko alikoenda kuiwakilisha nchi yake na si kwamba katumwa mara moja tu.
 
Hivi Ikulu bado inatumia email ya yahoo tu jamani?

Hivi kuna mtu anajali hili kama swala la national security?

​Kuna mtu mmoja aliwahi kusema huko nyuma kuwa watanzania tumelogwa na aliyetuloga alishakufa. Hayo ndo madhara yake.
 
Back
Top Bottom