JK awashangaa viongozi CCM kupenda anasa

_DSC0512.JPG
 
kweli hata mi kwa hili sijaona logic,, kusherehekea kuzaliwa kwa TANU? what about ASP? au ni ujumbe gani kwa watu wa Visiwani? na hili la "kushangaa" viongozi wa chini yake ndani ya ccm kupenda anasa kwa maana ya kutotimiza majukumu tarajiwa amechukua hatua gani? duuu hii kali
 
WENYEKITI wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, amewashangaa baadhi ya viongozi wa chama hicho, akisema hawajituma, wamesahau wajibu wao na wanapenda anasa. Alisema tabia hiyo imejijenga kwa viongozi hao kiasi cha kusahau majukumu yao ambayo ni pamoja na kudumisha umoja na moyo wa kujituma. Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Rais Kikwete alisema ni ajabu kuona viongozi hao wanashindwa kutekeleza majukumu yaliyoasisiwa na TANU, hata baada ya kuwezeshwa kwa rasilimali nyingi.

Kikwete alisema hayo wakati akizungumza na wanachama wa CCM katika maadhimisho ya kumbukumbu ya TANU na miaka 50 ya uhuru. Kwa mujibu wa Rais Kikwete, viongozi wa sasa wa CCM wamekosa moyo wa kujituma kiasi cha kusahau wajibu wao, licha ya kuwa na rasilimali nyingi ikilinganishwa na enzi za TANU.
“Sasa tumewapa magari, lakini hawaendi vijijini kuwatembelea wanachama. Wengine hata matawi hawayajui yanavyoendelea. Tusipokuwa na moyo wa kujituma, ndiyo utaona mambo yaliyopo sasa," alisema Rais Kikwete huku akishangiliwa na wanachama waliokuwa wamefurika katika Ukumbi wa Ubungo Plaza, jijini Dar es Salaam.
Rais Kikwete aliendelea: “Awali tuliwauliza, wana shida gani? Wakasema wanataka vipando (magari). Tukawapa Mahindra, wakaona hazitoshi. Siku hizi wana Land Cruiser. Lakini baadhi yao hawaonekani.

Kingunge alikuwa Katibu Mkuu wa TANU alifanya kazi kwa bidii bila gari. Leo wewe una shangingi unashindwa nini?” Akitoa mfano wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, Rais Kikwete alisema msingi wa TANU, ni umoja na moyo wa kujituma. Alisema TANU ilishinda vikwazo vingi licha ya kutokuwa na rasilimali nyingi kama walizokuwanazo wakoloni, kwa kuwa walitegemea umoja wa wanachama waliokuwa masikini.

“TANU ilikuwa na uwezo mdogo wa rasilimali hivyo ilitegemea michango ya wanachama waliokuwa masikini. Siri ilikuwa ni umoja na mashikamano wa wanachama wake. Mwalimu Nyerere alisisitiza kitu hicho hadi anakufa, Umoja ni nguvu, utengano ni udhaifu,” alisema Kikwete Rais Kikwete alieleza kuwa kupitia umoja na moyo wa kujitolea, TANU ilishinda pia changamoto ya kuwaondoa wakoloni waliokuwa waking’ang’ania madarakani.
na yeye ni miongoni mwao sasa anashangaa nini? aanze kujishangaa kwanza yeye
 
Wauvunje tu huo muungano na kitachofuata ni unguja na pemba kutengana na pemba wataungana na bara kuwaacha unguja wenyewe!!!!
 
Back
Top Bottom