JK awashangaa viongozi CCM kupenda anasa

sulphadoxine

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
2,257
644
WENYEKITI wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, amewashangaa baadhi ya viongozi wa chama hicho, akisema hawajituma, wamesahau wajibu wao na wanapenda anasa. Alisema tabia hiyo imejijenga kwa viongozi hao kiasi cha kusahau majukumu yao ambayo ni pamoja na kudumisha umoja na moyo wa kujituma. Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Rais Kikwete alisema ni ajabu kuona viongozi hao wanashindwa kutekeleza majukumu yaliyoasisiwa na TANU, hata baada ya kuwezeshwa kwa rasilimali nyingi.

Kikwete alisema hayo wakati akizungumza na wanachama wa CCM katika maadhimisho ya kumbukumbu ya TANU na miaka 50 ya uhuru. Kwa mujibu wa Rais Kikwete, viongozi wa sasa wa CCM wamekosa moyo wa kujituma kiasi cha kusahau wajibu wao, licha ya kuwa na rasilimali nyingi ikilinganishwa na enzi za TANU.
“Sasa tumewapa magari, lakini hawaendi vijijini kuwatembelea wanachama. Wengine hata matawi hawayajui yanavyoendelea. Tusipokuwa na moyo wa kujituma, ndiyo utaona mambo yaliyopo sasa," alisema Rais Kikwete huku akishangiliwa na wanachama waliokuwa wamefurika katika Ukumbi wa Ubungo Plaza, jijini Dar es Salaam.
Rais Kikwete aliendelea: “Awali tuliwauliza, wana shida gani? Wakasema wanataka vipando (magari). Tukawapa Mahindra, wakaona hazitoshi. Siku hizi wana Land Cruiser. Lakini baadhi yao hawaonekani.

Kingunge alikuwa Katibu Mkuu wa TANU alifanya kazi kwa bidii bila gari. Leo wewe una shangingi unashindwa nini?” Akitoa mfano wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, Rais Kikwete alisema msingi wa TANU, ni umoja na moyo wa kujituma. Alisema TANU ilishinda vikwazo vingi licha ya kutokuwa na rasilimali nyingi kama walizokuwanazo wakoloni, kwa kuwa walitegemea umoja wa wanachama waliokuwa masikini.

“TANU ilikuwa na uwezo mdogo wa rasilimali hivyo ilitegemea michango ya wanachama waliokuwa masikini. Siri ilikuwa ni umoja na mashikamano wa wanachama wake. Mwalimu Nyerere alisisitiza kitu hicho hadi anakufa, Umoja ni nguvu, utengano ni udhaifu,” alisema Kikwete Rais Kikwete alieleza kuwa kupitia umoja na moyo wa kujitolea, TANU ilishinda pia changamoto ya kuwaondoa wakoloni waliokuwa waking’ang’ania madarakani.
 
chama cha mapindunduzi kurudisha sherehe za tanu, je kupitia sherehe hizo tanu itaweza kuimarisha chama hicho, hii ni kutokana na watanzania wengi kukipenda chama hiki kilichodai uhuru kutoka kwa mkoloni.
 
WENYEKITI wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, amewashangaa baadhi ya viongozi wa chama hicho, akisema hawajituma, wamesahau wajibu wao na wanapenda anasa. Alisema tabia hiyo imejijenga kwa viongozi hao kiasi cha kusahau majukumu yao ambayo ni pamoja na kudumisha umoja na moyo wa kujituma. Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Rais Kikwete alisema ni ajabu kuona viongozi hao wanashindwa kutekeleza majukumu yaliyoasisiwa na TANU, hata baada ya kuwezeshwa kwa rasilimali nyingi.

Kikwete alisema hayo wakati akizungumza na wanachama wa CCM katika maadhimisho ya kumbukumbu ya TANU na miaka 50 ya uhuru. Kwa mujibu wa Rais Kikwete, viongozi wa sasa wa CCM wamekosa moyo wa kujituma kiasi cha kusahau wajibu wao, licha ya kuwa na rasilimali nyingi ikilinganishwa na enzi za TANU.
"Sasa tumewapa magari, lakini hawaendi vijijini kuwatembelea wanachama. Wengine hata matawi hawayajui yanavyoendelea. Tusipokuwa na moyo wa kujituma, ndiyo utaona mambo yaliyopo sasa," alisema Rais Kikwete huku akishangiliwa na wanachama waliokuwa wamefurika katika Ukumbi wa Ubungo Plaza, jijini Dar es Salaam.
Rais Kikwete aliendelea: "Awali tuliwauliza, wana shida gani? Wakasema wanataka vipando (magari). Tukawapa Mahindra, wakaona hazitoshi. Siku hizi wana Land Cruiser. Lakini baadhi yao hawaonekani.

Kingunge alikuwa Katibu Mkuu wa TANU alifanya kazi kwa bidii bila gari. Leo wewe una shangingi unashindwa nini?" Akitoa mfano wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, Rais Kikwete alisema msingi wa TANU, ni umoja na moyo wa kujituma. Alisema TANU ilishinda vikwazo vingi licha ya kutokuwa na rasilimali nyingi kama walizokuwanazo wakoloni, kwa kuwa walitegemea umoja wa wanachama waliokuwa masikini.

"TANU ilikuwa na uwezo mdogo wa rasilimali hivyo ilitegemea michango ya wanachama waliokuwa masikini. Siri ilikuwa ni umoja na mashikamano wa wanachama wake. Mwalimu Nyerere alisisitiza kitu hicho hadi anakufa, Umoja ni nguvu, utengano ni udhaifu," alisema Kikwete Rais Kikwete alieleza kuwa kupitia umoja na moyo wa kujitolea, TANU ilishinda pia changamoto ya kuwaondoa wakoloni waliokuwa waking'ang'ania madarakani.
The known propensity of a democracy is to licentiousness which the ambitious call and the ignorant believe to be liberty
 
Juzi, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kilisheherekea miaka 57 ya kuzaliwa kwa TANU kwa mbwembwe na chereko. TANU ilimaliza muda wake wa kuishi baada ya kuungana na ASP mwaka 1977.

Hii inafanana na kufanya birthday ya marehemu mzazi wako! Kuna kituko kimoja kilifanyika Moshi cha mtu kufanya jubilei ya ndoa yake wakati mwenzi wake alishakufa miaka kumi iliyopita.

Ukitazama kwa makini inaonyesha kuwa CCM wameshaona kuwa hawana ushawishi wala haiba kwa wananchi na ikapelekea kukumbuka marehemu mzazi wake na kumfanyia birthday party ili walau kupata mapokeo mazuri ya wananchi.

Kulikuwa na ulazima gani wa kufanya sherehe hiyo? Kwa kizazi cha sasa ambacho kina muamko tofauti (rejea matokeo halisi ya uchaguzi mkuu uliopita), wala hawajui TANU ni nini! Labda wale wenye udadisi wa historia. Na hata wakiijua, haina mantiki yeyote kwao.

Nasubiri kwa hamu kufanywa kwa birthday party ya ASP. Tena basi mwakani ifanyike sherehe za kuzaliwa kwa TAA maana bila hiyo, TANU isingezaliwa! Halafu tena na sherehe ya kuzaliwa HIZBU. Ushanifahamu?
 
Mbinu walioitumia kurejesha sherehe za TANU ni mbinu fikirika ya kurejesha heshima ya chama chao kitu ambacho hakiendani na fikra na matendo yao.Wanaotaka mabadiliko ni vijana waliozaliwa baada ya uhuru, hawana sababu wala haja ya kurudi nyuma na kuwaza namna uhuru ulivyopatikana.Ni jambo lisilona shaka wanatwanga maji kwenye kinu.Matunda yake ni madogo sana.wananchi wanahitaji hali ya maisha na uchumi wao uboreshwe na si bra! Bra! wanazoleta!!!!!!!!!!
 
jamani mkuu wa kaya anatafuta sehemu nzur ya kupmzika au bado umwelewa@nngu007
 
hana jipya mbaya zaidi kasema ngeleja na mhando hawana kosa tatizo ni maji, anyway mi nilisikia kwenye nukuu za magazeti ya jana, mwenye full story anijuze.
 
Anashangaa? Mbona hajishangai yy mwenyewe na misafara ya BMW? Mkuu inabidi aache visingizio!
 
kuwashangaa tu haitoshi...kama mtu hatimizi wajibu wake fukuzia mbali waajiriwe wenye uchungu na kazi.
 
Rais Kikwete amedhihirisha kuwa yeye ni mtu safi asiye na doa, lakini wanaomuangusha ni watendaji wake.
 
CDM oyeeeeeeeee!!!! mbowe oyeeeeee!! slaaa oyeeeee!!! zitto oyeeeeeee!!! Tundu lissu oyeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee
 
Msajili wa vyama anajua kuwa kuna chama kipya TANU tanzania?maana ccm imekufa sasa waisajili TANU
 
Hivi yeye haoni tofauti kati ya TANU ile ya zamani na CCM yake hii ya sasa?
 
Mimi naamini kuwa hizi shereheni zina lengo la kuweka historia sahihi haa kwa vijana. Tukumbuke kuwa historia ya Tanzania ina uhusiano mkubwa na TANU.
 
Kikwete anakuwa komedia siku hizi mara sio mwaingu ya mvua ya kujaza mtera, sasa awewaambia watendaji wa serikali waache anasa.

Swali linakuja Je yeye ameacha hizo ANASA za KUSAFIRI NJE YA NCHI? mimi naona yeye anafanya anasa kubwa kuliko wengine hapa nchi.

anasema amewapa magari viongozi waende vijijini wakatembelea wananchama sio Wakajue wananchi wana matatizo gani ili serikali iweze kuyatatua.

Ndio nasema hivi Mtawala Jinga, Watanzania tumelala bado hakujakucha
 
Ukizungumzia siasa za TANU unazungumzia miiko ya AZIMIO LA ARUSHA,tena kwa viongozi.....je jk anafuata na ccm yake????
WENYEKITI wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, amewashangaa baadhi ya viongozi wa chama hicho, akisema hawajituma, wamesahau wajibu wao na wanapenda anasa. Alisema tabia hiyo imejijenga kwa viongozi hao kiasi cha kusahau majukumu yao ambayo ni pamoja na kudumisha umoja na moyo wa kujituma. Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Rais Kikwete alisema ni ajabu kuona viongozi hao wanashindwa kutekeleza majukumu yaliyoasisiwa na TANU, hata baada ya kuwezeshwa kwa rasilimali nyingi. Kikwete alisema hayo wakati akizungumza na wanachama wa CCM katika maadhimisho ya kumbukumbu ya TANU na miaka 50 ya uhuru. Kwa mujibu wa Rais Kikwete, viongozi wa sasa wa CCM wamekosa moyo wa kujituma kiasi cha kusahau wajibu wao, licha ya kuwa na rasilimali nyingi ikilinganishwa na enzi za TANU. “Sasa tumewapa magari, lakini hawaendi vijijini kuwatembelea wanachama. Wengine hata matawi hawayajui yanavyoendelea. Tusipokuwa na moyo wa kujituma, ndiyo utaona mambo yaliyopo sasa," alisema Rais Kikwete huku akishangiliwa na wanachama waliokuwa wamefurika katika Ukumbi wa Ubungo Plaza, jijini Dar es Salaam. Rais Kikwete aliendelea: “Awali tuliwauliza, wana shida gani? Wakasema wanataka vipando (magari). Tukawapa Mahindra, wakaona hazitoshi. Siku hizi wana Land Cruiser. Lakini baadhi yao hawaonekani. Kingunge alikuwa Katibu Mkuu wa TANU alifanya kazi kwa bidii bila gari. Leo wewe una shangingi unashindwa nini?” Akitoa mfano wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, Rais Kikwete alisema msingi wa TANU, ni umoja na moyo wa kujituma. Alisema TANU ilishinda vikwazo vingi licha ya kutokuwa na rasilimali nyingi kama walizokuwanazo wakoloni, kwa kuwa walitegemea umoja wa wanachama waliokuwa masikini. “TANU ilikuwa na uwezo mdogo wa rasilimali hivyo ilitegemea michango ya wanachama waliokuwa masikini. Siri ilikuwa ni umoja na mashikamano wa wanachama wake. Mwalimu Nyerere alisisitiza kitu hicho hadi anakufa, Umoja ni nguvu, utengano ni udhaifu,” alisema Kikwete Rais Kikwete alieleza kuwa kupitia umoja na moyo wa kujitolea, TANU ilishinda pia changamoto ya kuwaondoa wakoloni waliokuwa waking’ang’ania madarakani.
 
Dalili nyingine hiyo ya kuvunjika muungano kwani hili likitokea CCM inakufa technically ndio maana jamaa wanafufua TANU. Kwa wasiojua TANU(bara) iliungana na ASP(visiwani) 1977 kuunda CCM baada ya Tanganyika kuungana na Zanzibar Kuunda Tanzania 1964.
 
Back
Top Bottom