Elections 2010 JK auza nchi kwa magaidi?

''''Katika mitambo yetu tumenasa mazungumzo ya ndani ya shirika hilo la ujasusi na inavyoonekana lengo kubwa siyo Uranium peke yake bali ni kufanya undumilakuwili(double crossing) kwa kusaidia JK halafu mlango wa nyuma maadui zake ili kuliingiza taifa hili kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe. Inasemekana kuwa nchi hiyo imefanya ujasusi wa kutosha wa kiuchumi na kugundua kuwa nchi yao itafaidika sana kama Tanzania ikiwa vitani kuliko hali ikiwa ya amani. Wanahitaji Uranium lakini baadaye wanataka waipate kwa njia za panya, halafu wauze silaha na mengineyo'''.
guuuuud....
mnajiandaa kuleta vurugu na uvunjifu wa amani ili mje msingizie mashirika ya kijasusi????
kwa kipindi tulicho nacho, habari shallow kama yako haiwezi kutisha watu hata kidogo,na isitoshe, wengi wenu hamna taaluma ya uaskari na mnafikiri jeshini kuna unafiki na uzandiki kama kwenye siasa na uswazi kwenu!!! unajaribu kuligawa jeshi letu kwa kusema kuna JWTZ B??
JESHI letu linasifika kwa nidhamu na kujituma kwa mujibu wa sheria hivyo jipe moyo kuwa watawaunga mkono katika upumbavu mnaotarajia kuufanya,,
najua kuwa mnajua kuwa ushindi haupo hata mkandamana uchi. na ukweli unajulikana kwamba hata mkileta vurugu na jeshi likaamua kukaa pembeni, mko wachache kiasi kwamba hatutahitaji nguvu kuuuubwa kusafisha virus kutoka kwenye nchi yetu, wewe na wenzako jidanganyeni na umati mnaouona kwenye mikutano ya kibaraka wa MBOWE(SLAA) MDHANI KUWA WOTE NI WAFUASI WA chadema. mtashangazwa na matokeo ya kura na hapo ndipo mtakapojua kuwa nguvu ya umma ipo pande ipi
 
Habari za uhakika tulizozipata masaa machache yaliyopita ni kwamba JK ameingia mkataba na nchi moja kubwa ili shirika la ujasusi la nchi hiyo liweze kumsaidia kupata ushindi kwa wizi bila kuhatarisha amani nchini. Hii ni baada ya balozi wa nchi hiyo kubwa kumpa ripoti ya kijasusi inayoonyesha kuwa bila usaidizi wa nchi hiyo nchi ni lazima itaingia kwenye vita ndani ya Mwezi Novemba.

Katika ripoti ya shirika hilo la kijasusi imeonyesha kwamba Taasisi ya kijasusi ya Tanzania ama 'idara ya usalama' ukiondoa mkuu wake OR hawana mapenzi kabisa na JK japo kuna wenye mapenzi na CCM. Ripoti hiyo pia imeonyesha kuwa ndani ya vyombo vya usalama na ulinzi ikiwemo JWTZ wana chuki kubwa na JK na wanamdharau kutokana na namna alivyoendesha nchi kwa miaka 5 iliyopita.

Ripoti pia inaonyesha kuwa wanamtandao wa 2005 tayari wanaendesha kwa siri kubwa mchakato wa kijasusi utakaomfanya JK apate 'suprise' kwa kujikuta ameshindwa kabisa kiti cha urais japo mikakati yote ya kuchakachua matokeo imeonekana kufanikiwa. Hili ni kundi lililokuwa nyuma ya uanzishwaji wa CCJ kwa usiri na kwa kujificha.

Ripoti imemtaja EL ambaye majuzi alisifiwa na JK na kutambulishwa kwa wapiga kura huko kaskazini mwa Tanzania kuwa ni mmoja kati ya viongozi wa mkakati huu na ambaye tayari amejiandaa kuhakikisha hata jimboni kwake tu ni yeye peke yake anayepita kwa kushinda kiti cha ubunge lakini JK katu hapiti.

Yako mambo mengi kwenye ripoti hiyo ambayo yalimfanya JK ashindwe kutoa jibu mara baada ya kukabidhiwa ripoti ya mwisho ya REDET na mwanamke mmoja BK wa REDET ambapo hii ilikuwa mara ya pili, kwani mara ya kwanza ilionyesha kuwa JK anaongoza kwa asilimia 81.3 na ndipo baada ya kuangalia upepo akawarudishia ili wairekebishe kwani Dk.alionekana kupata asilimia 6.8 tu jambo lililomfanya JK ang'ake 'wewe unataka kuniharibia wewe, ukimpa asilimia sita si itaonekana uongo wa wazi, kabadilisheni haraka'

Safari hii ilipoletwa alikuwa tayari ameshachanganywa na ripoti ya shirika lile la ujasusi na hivyo baada ya kumgandisha kwa muda mrefu mama huyo ambaye inasemekana ni girlfriend wake wa muda mrefu na ameshaahidiwa ukatibu mkuu wa wizara ya elimu, JK alimwambia tu 'haya kaitoeni' bila kuiangalia kiundani.

Habari zinasema kuwa nchi hiyo kubwa ina uchu mkubwa wa madini yetu ya Uranium na haiko tayari kuona nchi nyingine yeyote inayakamata. Hivyo tayari wamekwisha sambaza NGO zao sehemu kubwa ya Tanzania wakijifanya kushughulikia HIV, kumbe wanafanya ujasusi kuhusu rasilimali zetu. Hawa ni magaidi ambao hupenda kuita nchi nyingine magaidi huku wakiwaibia rasilimali zao.

Hivi sasa wameleta na wanaendelea kuleta majasusi wa shirika lao japo wana utaifa wa nchi mbalimbali kama waangalizi wa kimataifa wa uchaguzi huu ikiwa ni moja kati ya mkakati wa shirika hilo la ujasusi kuhakikisha linatimiza makubaliano ya mkataba, yaani kazi imeanza. Hivyo hata uchaguzi uchakachuliwe mpaka mtoto mchanga mwenyewe aone waziwazi kuwa umechakachuliwa bado waangalizi hao watasema ulikuwa huru na wa haki.

Hivi sasa shughuli za saidia JK ashinde zimeanza pole pole kuchukuliwa na shirika hilo kutoka kwa mtandao mpya wa JK unaoongozwa na RK, na shughuli za kampeni zinazoongozwa na AK. 'we are taking over from here gentlemen' wanasema majasusi hao.

Katika mitambo yetu tumenasa mazungumzo ya ndani ya shirika hilo la ujasusi na inavyoonekana lengo kubwa siyo Uranium peke yake bali ni kufanya undumilakuwili(double crossing) kwa kusaidia JK halafu mlango wa nyuma maadui zake ili kuliingiza taifa hili kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe. Inasemekana kuwa nchi hiyo imefanya ujasusi wa kutosha wa kiuchumi na kugundua kuwa nchi yao itafaidika sana kama Tanzania ikiwa vitani kuliko hali ikiwa ya amani. Wanahitaji Uranium lakini baadaye wanataka waipate kwa njia za panya, halafu wauze silaha na mengineyo.

Nchi hii kubwa inaamini kuwa hakuna biashara inayolipa duniani kama vita. Lakini hawakubali asilani vita kwenye ardhi yao.

Mtaji wao mkubwa kutokana na habari za uhakika kutokwa kwa mmoja wa makatibu wa kwanza wa ubalozi huo ni kwa uchakachuaji wa matokeo.

WATANZANIA TUAMKE, JWTZ, TISS NA WENGINEO KUMBE SIYO WALINZI KWENYE UCHAGUZI HUU BALI NDIO WATAKAO TUMIWA NA NCHI HII KUBWA KULETA MACHAFUKO NCHINI. HAITAKUWA VITA KATI YA WANANCHI NA WANANCHI, ITAKUWA VITA KATI YA JWTZ A NA JWTZ B LAKINI WATAKAOUMIA NI WANANCHI WA TANZANIA KWA FAIDA YA WAGENI.

KAMA UNAIPENDA NCHI HII, ZUIA UCHAKACHUAJI WA MATOKEO AMBAO UMESHAANZA KWA MATOKEO YA TAFITI ZA KISHENZI. VINGINEVYO MUDA SI MREFU........ TANZANIA PIA TUTAITWA NCHI YA KIGAIDI, HUKU JAMAA WAKIBEBA URANIUM, TANZANITE, DHAHABU, ALMASI, WANYAMA WETU, HALAFU HAWATOKI NG'O WAKIDAI KULINDA AMANI MPAKA WAMALIZE KABISA KWA FAIDA YA NCHI ZAO.

JAMANI EBU TUKUBALI MABADILIKO, TUKUBALI SAUTI YA UMMA, VINGINEVYO TUTAJUTA.
tuwekee mawasiliano mliyoyanasa juu kwa juu kama unavyodai,la sivyo wewe hautakuwa tofauti na shimbo kutisha wapiga kura.
 
Mtoa hoja tusaidie kwa kuwa muwazi zaidi, ninaona kama unazungumzia USA na kama ndivyo basi useme hivyo na kama kweli ripoti hii ipo basi ing'aze hapa CIA wataipata tu na wataifanyia kazi.
 
[

Ripoti pia inaonyesha kuwa wanamtandao wa 2005 tayari wanaendesha kwa siri kubwa mchakato wa kijasusi utakaomfanya JK apate 'suprise' kwa kujikuta ameshindwa kabisa kiti cha urais japo mikakati yote ya kuchakachua matokeo imeonekana kufanikiwa. Hili ni kundi lililokuwa nyuma ya uanzishwaji wa CCJ kwa usiri na kwa kujificha.

Ripoti imemtaja EL ambaye majuzi alisifiwa na JK na kutambulishwa kwa wapiga kura huko kaskazini mwa Tanzania kuwa ni mmoja kati ya viongozi wa mkakati huu na ambaye tayari amejiandaa kuhakikisha hata jimboni kwake tu ni yeye peke yake anayepita kwa kushinda kiti cha ubunge lakini JK katu hapiti.

Hapo kwenye red baba ,umechapia.
Katika watu wote watakao taka JK asirejee madarakani, Lowasaa hawezi kuwa mmoja wao. Lowasa needs JK now ,More than Ever!
 
Katika ripoti ya shirika hilo la kijasusi imeonyesha kwamba Taasisi ya kijasusi ya Tanzania ama 'idara ya usalama' ukiondoa mkuu wake OR hawana mapenzi kabisa na JK japo kuna wenye mapenzi na CCM. Ripoti hiyo pia imeonyesha kuwa ndani ya vyombo vya usalama na ulinzi ikiwemo JWTZ wana chuki kubwa na JK na wanamdharau kutokana na namna alivyoendesha nchi kwa miaka 5 iliyopita.

akashube na Ndege ya Uchumi,
Mimi pia hivi juzi tu nilipata wasaa wa kukutana na "Kijana" mida ya Happy Hawaz maeneo karibu na Jengo Jipya la Ubia kati ya Jk, Rostam na Karamagi. Alinithibitishia suala hili pamoja na lile la pesa (3 Billion) iliyokuwa mbioni KUONGEZWA na Ikulu kusaidia Kampeni jk na ikanusuriwa na mkwara wa Dr. Slaa. Ni kweli kuwa JK alipewa taarifa za mwenendo wa kampeni na upepo wa matokeo yanayobashiriwa kwa ujumla. Na hazikuwa nzuri hata kidogo kwa JK. Inawezekana alipandikizwa woga maksudi ili Majasusi wapate nafasi ya kuonyesha umuhimu wa kazi yao. Na kwa mujibu wa "Kijana" Wanazidi kufanikiwa katika lengo lao. Jk anazidi kuona kwamba wao ndiyo wanashikiria mustakabali wa matokeo ya Urais.

SHIME WAZALENDO TUSIPUUZE TAARIFA YA akashube
 
JF ni sehemu ambayo hata magazeti yote ya bongo wanakuja kuchukua news hapa. Hii taarifa sipingani nayo hata kidogo kwani mengi ambayo yamesemwa hapa yamekuja kuoneka kuwa ni ya ukweli anzia na redet.Marekani wanajipenda wenyewe tu basi hakuna kitu kingine angalia iraq,kongo,angola. Wamarekani wapo huko hata urusi ana rasilimali nyingi lakini kamwe hataki kusikia kitu USA

Wewe kweli nyani! Teh teh teh!
 
Kwa Tanzania hii sitarajii marekani wakitaka Uranium wana haja ya kuanzisha vita... Ninachoweza kurikiri ni kuwa watafanya kila linalowezekana kuhakikisha JK anabaki madarakani, akiwa na upinzani haba bungeni, ili waendelee kuingia mikataba feki za kuzipata hizo raslimali...
 
tangu ilipoanzishwa hii thread jana niliikwepa kuchangia kwa kuwa nilijipa muda wa kutafakari yaliyomo.
Kwa kweli nimestuka na hii ishu.

Nimekuwa nawasoma wamarekani na tricks zao tangu nikiwa mtoto na ninaamini kwamba mtoa taarifa hajazuka hewani au ametunga tu. Tukubali kwamba USALAMA wa nchi upo kwenye hali tete sasa na ni sisi wananchi tunaopaswa kujiweka dhamana kwa amani yetu nchini. tusithubutu kuruhusu mtu kumtoa jicho jirani yake wala jamii dhidi ya jamii. Cha msingi ni kukaaa chini, na kutafakari how to dodge hii trap at this very short period. Naamini inawezekana hata in last minute inawezekana.

Natamani ningekuwa UwT walah hawa vidudu mtu kutoka nje wangelijuta kuzaliwa. Naamini tuna mfumo mzuri wa ulinzi lakini viongozi wanauingilia kwa manufaa yao binafsi.

Dawa ni kutoipatia ccm kura na tuone huo moto wao wa kiranga cha uranium utawashwa vipi. Kwanza napinga uuzwaji wa uranium nje maana sisi tunaihitaji sana kwa ajili ya nishati na shughuli nyingine za maendeleo.
Msilale amkeni ninyi wakulima wa tz
 
Hata kama habari yenyewe haiaminiki, Jamani watanzania wenzangu, turudi kwenye nyumba za ibada, kuiombea nchi yetu! Maana vinywa vyetu huumba!
 
du watu mna data!...........kumbe tunaweza kuwa na akina DR.SLAA wengi tu km tukiamua..........
 
Japo sijui mambo ya kiintelijensia lakini unaweza kujua kwamba wamerekani kuna kitu wanataka kwenye nchi yetu baada ya kuona upepo wa kisiasa unamwendea Dr. Slaa kumekuwepo na mikataba mikubwa mikubwa ya misaada iliyosainiwa mwezi wa tisa kutoka kwa wamerekani na waingereza,umoja wa nchi za ulya na makampuni yao,ukiangalia kwa wepesi huwezi kujua maana yake nini lakini ukweli wanataka kuuuthibitishia umma kwamba nchi hizo tajiri na zenye sauti kuu duniani wanaimani na utawala wa kikwete kwa mantiki hiyo tutapenda kumpigia kura kwa sababu tutaamini fedha za misaada zitaleta maeendeleo,vile vile wanalinda uhai wa makampuni yao makubwa kumbuka uingereza ni nchi ya kwanza ikifuatiwa na kenya kwa kuwekeza Tanzania
Nadhani wananchi tumeamka sasa,marekani hawajawahi kushinda vita mahali popote duniani wanachukiwa sana na hadhi yao imeshuka kwa ajili ya uvunjifu wa amani katika nchi wanazolazimisha kujipenyeza nadhani elimu ya uraia iongezwe ili tuweze kukomboa nchi yetu ,kama makampuni wamempa ndege KIkwete unategemea nchi zao zitakaa pembeni thubutu.
 
Unajua katika mambo ya utawala grapevine pia ni source ya taarifa.
Na wataalamu huwa wanashauri kuwa hautakiwi kudharau grapevine inaweza kukutokea puani
 
Hizi ni taarifa muhimu mno kwa usalama wa nchi.
hatua zichukuliwe
 
Nchi hiyo kubwa yenye kuhitaji uranium ni Marekani lakini marekani siyo kweli wanapenda vita ziwepo nchi za wengine. Huu uchambuzi una walakini sana. Hoja za kutoyachakachua matokeo ndicho USA wanataka na wanelewa yoyote atakayekuja watafanya naye kazi. Hii siyo nchi ya kislamu na hivyo kufurahia vita vya wenyewe kwa wenyewe na kauli kama hizi zilizochanganywa na ukweli huu zinalenga kutupofua macho:-
MKuu, nakubaliana na wewe na ndo maana nimeitilia mashaka habari hii. Pia tukumbuke kuwa rais wa sasa ni mwislamu na ameonekana ni mdini na amekuwa akigawa ardhi na rasilimali kwa waarabu. Sasa hapo anaweza vipi kuwa 'ally' wao? Hiyo uranium nayo nasikia inashikiwa na RA kupitia Caspian, kwa hiyo probability kubwa ni kuwa waarabu ndo watakuwa na interest na rais huyu kuliko wamarekani.
NImejaribu kutumia logic lakini sipati jibu na siko tayari to go out on a limb on this maana mpaka sasa sijaona evidence yoyote.
Kusafiri sana kwa JK Marekani ni kutokana na business interest ya baadhi ya wawekezaji hapa lakini siyo official US government. Kitu pekee ninachoweza kulink hapa ni akina Tudor Jones na wenzake, na kama ni CIA hawa siyo official inaweza ikawa ni wale 'consultants' lakini hebu tusubiri tuone....
 
Japo sijui mambo ya kiintelijensia lakini unaweza kujua kwamba wamerekani kuna kitu wanataka kwenye nchi yetu baada ya kuona upepo wa kisiasa unamwendea Dr. Slaa kumekuwepo na mikataba mikubwa mikubwa ya misaada iliyosainiwa mwezi wa tisa kutoka kwa wamerekani na waingereza,umoja wa nchi za ulya na makampuni yao,ukiangalia kwa wepesi huwezi kujua maana yake nini lakini ukweli wanataka kuuuthibitishia umma kwamba nchi hizo tajiri na zenye sauti kuu duniani wanaimani na utawala wa kikwete kwa mantiki hiyo tutapenda kumpigia kura kwa sababu tutaamini fedha za misaada zitaleta maeendeleo,vile vile wanalinda uhai wa makampuni yao makubwa kumbuka uingereza ni nchi ya kwanza ikifuatiwa na kenya kwa kuwekeza Tanzania
Nadhani wananchi tumeamka sasa,marekani hawajawahi kushinda vita mahali popote duniani wanachukiwa sana na hadhi yao imeshuka kwa ajili ya uvunjifu wa amani katika nchi wanazolazimisha kujipenyeza nadhani elimu ya uraia iongezwe ili tuweze kukomboa nchi yetu ,kama makampuni wamempa ndege KIkwete unategemea nchi zao zitakaa pembeni thubutu.

If we don't understand the rule of the game, we can simply be reduced to a pure guessing group while the conspiracy goes on without any objection.

Every one of us should be aware that, most of us are just common people and good citizens, there is little we can do in this game.

Pengine mtu anaweza kudhani nguvu yetu ipo kwenye mchezo wa ballot box, lakini ukweli ni kuwa hata huko hatuna nguvu sana kama Farao akigoma kusikia la Musa. Ndio maana nikapendekeza UWT watumie uzalendo kwa nchi yao kwa niaba yetu… (ipo mifano ya uzalendo k.v. Kombe). Hawa wanaweza, wakitaka, wanao uwezo wa kutusaidia.

Bila hivyo tunaendelea kubaki tunalalamika, kutoa mabunio yetu na kujaza mabandiko ya nadharia na kejeli za kila aina.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom