Jk aunda kamati okoa maisha somalia

KABAVAKO

JF-Expert Member
Apr 5, 2011
229
32
Rais wa Tanzania, mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ameunda kamati ya matajiri wa nchi hii kwa ajiri ya kukusanya michango ya watanzania kwa ajili ya kuwasaidia wasomali wanakufa kwa nja. Mwenyekiti wa kamati hiyo akiwa ni Bwaba Reginald Mengi na wajumbe kadhaa akiwemo Haruna Zakaria, Said Bakhresa na Mohammed Dewji. Takribani tan 200 za vyakula mbali mbali zimechangwa na matajiri hao. Mheshimiwa Rais amewaomba watanzania kuwachangia wasomali kupitia kamati hiyo.
 
Kiteto wanakufaa njaa, rais anakimbilia Somali?!: well, wamarekani wanatutafuna kimyakimya.
 
Wengine kati ya hao aliowateua kumsaidia kuchangisha hicho chakula kwa ajili ya wasomali wanashukiwa kuhusika na biashara haramu ya madawa ya kulevya, Je Mkweree anaweza kuwathibiti kwa biashara yao hiyo haramu inayowangizia kipato anachowaomba wakitumie kuthibiti njaa ya wasomali?
 
Okoa Maisha Tanzania ameshindwa..ndio ataweza huko somalia kwa maharamia.
 
Nadhani ni jambo bora sana, kwa sababu kuna hatari ya hao Wasomali wakavuka mipaka na kuja Tanzania kutafuta ifadhi na vyakula, sasa ni bora wasaidiwe ili waweze kujitegemea.
 
Nadhani ni jambo bora sana, kwa sababu kuna hatari ya hao Wasomali wakavuka mipaka na kuja Tanzania kutafuta ifadhi na vyakula, sasa ni bora wasaidiwe ili waweze kujitegemea.
&lt;br /&gt;<br />
&lt;br /&gt;<br />
Naungana na wee, yaani hata kama wasomali hawatakuja pana haja ya sie pia kujitolea na sio kusubiri wazungu tu. Mtu hawezi akasema Tanzania kuna njaa, tatizo la TZ ni usambazaji mbovu kutoka wanakozalisha sana kwenda kuliko na uhaba. Lazima tujue pia kuwa kutoa sio lazima iwe ziada iliyotushinda kuitumia, mbona wazungu wanatoa misaada lkn wao wanalipa kodi mno kuliko sie tunaopewa. Ktk hilo big up Kikwete umetuondolea aibu maana nasikia kwenye harambee ya somalia huko Addis Ababa kuna mwanafunzi wa kighana ametoa dolla za US 4000 wakati serikali ya Lesotho imetoa dolla 2000 na nchi nyingine wala hazikutokea kupledge.
 
Kiteto wanakufaa njaa, rais anakimbilia Somali?!: well, wamarekani wanatutafuna kimyakimya.

Haya kibwagizo cha kila kitu Marekani/Wamarekani tena!!!!? hata njaa zetu na za wa al shabab?
 
ili waweze kujitegemea.
us.jpg
seo1.jpg

seo.jpg

uk.jpg
 
Back
Top Bottom