Elections 2010 JK atangaza kumaliza tatizo la maji umasaini

Zak Malang

JF-Expert Member
Dec 30, 2008
5,404
233
JK atangaza kumaliza tatizo la maji umasaini

Kizitto Noya, Simanjiro

MGOMBEA urais kwa tiketi ya CCM, Jakaya Kikwete jana aliendelea na kampeni katika Jimbo la Simanjaro ambako pamoja na mambo mengine, aliahidi kutafuta Sh30 bilioni kwa ajili ya kumaliza tatizo la maji kwenye jamii hiyo ya wafugaji.

Akizungumza kwenye viwanja vya Orkesumet, makao makuu ya Wilaya ya Simanjiro, Kikwete alisema mbali na kumaliza tatizo hilo, serikali yake ijayo pia itatoa ruzuku ya dawa ya josho za ng’ombe kwa wafugaji.

“Jitihada za awali za tatizo la maji tayari zimeelezwa na mbunge wenu (Ole Sendeka) lakini serikali inajipanga kumaliza kabisa tatizo hilo," alisema Kikwete.

“Tunahitaji kuwa na Sh30 bilioni kwa ajili ya kuvuta maji kutoka Mto Ruvu na huu ni mradi mkubwa ambao mipango ya awali ya kuomba fedha imeshaanza.”
Kwa mujibu wa Kikwete, wakati serikali inaendelea kusubiri Sh30 bilioni, jitihada za awali zimeanza kwa kutenga Sh1.8 bilioni kwa ajili ya kuchimba visima virefu vya maji.

“Tutachimba visima hivyo kwa awamu. Tutaanza na vijiji 12 na baadaye vijiji vingine vilivyobaki,” alisema Kikwete ambaye pia alieleza kuwa lengo la serikali yake ijao ni kumaliza kabisa tatizo la maji nchini.
Kikwete alisema maelekezo ya CCM kwa serikali ijayo, ni kuhakikisha inatengeneza mipango ya kuendeleza sekta za maji, mifugo na kilimo na yeye kama msimamizi mkuu wa maelekezo hayo, amejipanga ipasavyo kuhakikisha hilo linafanikiwa.

“Tuchagueni tuendelee kustawisha nchi yetu. Tutahakikisha kila mfugaji anakuwa na maji yake katika kipindi chote cha mwaka ili kuondokana na tatizo la kuhamahama,” alisema

Awali kabla ya Kikwete kuanza kuhutubia, mbunge anayetetea nafasi yake kwa tiketi ya CCM jimboni humo, Christopher Ole Sendeka alimkabidhi rungu na mgolole kama ishara ya ushindi na uongozi.

Baadaye mbunge huyo mteule alisema CCM ni chama kinachostahili kuendelea kuongoza nchi kwani kimefanya mengi katika kipindi kifupi cha miaka mitano iliyopita chini ya uongozi wa Kikwete.
“Katika kipindi hicho cha miaka mitano, makao makuu ya Simanjiro ya Orkesumet hayakuwa na umeme, lakini sasa tumefanikiwa kusambaza umeme,” alisema Ole Sendeka.

“Katika kipindi hicho pia tumechimba visima 55 virefu vya maji na kuongeza idadi ya wanafunzi wa sekondari kutoka 180 hadi 2,300. Tumeongeza pia shule kutoka tatu hadi 16 na kufanikiwa kutengeneza barabara ya Simanjiro hadi Arusha,” alisema
Rais Kikwete jana alifanya kampeni katika majimbo ya Kiteto, Simanjiro na Karatu kwa mpinzani wake wa urais, Dk Willibrod Slaa.

Tathimini inaonyesha kuwa Kikwete atapata kura nyingi zaidi kuliko wagombea wengine wa vyama vya upinzani katika jimbo la Simanjiro hasa baada ya ole Sendeka kupita bila kupingwa huku CCM ikipita pia bila kupingwa katika kata 16 kati ya kata 18 za jimbo hilo.

Chanzo: Mwananchi




My take: Hivi sasa bado siku tano ndo JK analiona tatizo hilo? Alikuwa wapi ktk miaka mitano iliyopita? Ama kweli jamaa huyu anachekesha!!
 
Kama tatizo la Maji Dar ambako kuna ikulu limeisha basi kumaliza tatizo la maji umasaini ni SIMPLE kama kumsukuma mlevi. Ila kama bado tatizo la maji Dar linampasua kichwa JK basi hili la Umasaini litakuwa ndoto za Alinacha kama siyo za Abunuwasi. Wamasai na makabila ya wafugaji wajue ahadi anazo toa DK Mazishi kwao ni zile za zamani enzi za ujinga na giza kipindi ambacho watu walikuwa na uwezo mdongo wa kupembua mambo.

JK aambiwe wamasai na wafugaji hawadanganyikiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii
 
Sasa kama billion 30 zinaweza kutoa maji Ruvu mpaka umasaini, then Dar peke yake haitahitaji zaidi ya billion 10 lakini maji watu hawayajui. Vilevile haiingii akilini kama CCM wanaweza kutumia Tshs > 50 billion kwenye kampeni za JK pekee iwaje leo waseme 30 billion ni nyingi na wanatafuta mhisani??
 
Hata akikaa ikulu maisha yake yote hawezi kumaliza tatizo la maji. Asubiri kidogo tumwajishe 31 10 2010
 
JK tumekuzoea wewe hujawahi kuwa serious kwenye issue zinazoligusa taifa. Acha porojo za maji jisalimishe yaishe
 
Maji kutoka ruvu hadi UMASAINI??????
LAITI KAMA TZ TUNGEKUA TUNATUMIA KIINGEREZA KAMA NCHI NYINGINE NADHANI MATAIFA YOTE YANGEKUA YANAONA HII NCHI WATU NI WAPUMBAVU NA WASIOJUA HAKI ZAO MILEE.. TUMSHUKURU NYERERE NA KUMUENZI SANA TU MANA ALIPOKAZANIA TUTUMIE KISWAHILI ALIKUA UNAFAAMU NI NINI NA NI WAPI TUNAPOELEKEA BILA KUANGALIA ILI TUSIJE KUWA KITUKO
kama wameshindwa kwa dar,tanga,moshi... je uo umbali wote watauweza??
mfano ni Dar es salaam tu tusiende mbali yan kwel watanzania tunadanganywa sana..
arusha mjini kwenyewe shida na sehemu za nje ya mji, je iwe uko vijijini????
miaka yote alikua wapi hadi awambie kipindi cha uchaguzi
 
Maji kutoka ruvu hadi UMASAINI??????
LAITI KAMA TZ TUNGEKUA TUNATUMIA KIINGEREZA KAMA NCHI NYINGINE NADHANI MATAIFA YOTE YANGEKUA YANAONA HII NCHI WATU NI WAPUMBAVU NA WASIOJUA HAKI ZAO MILEE.. TUMSHUKURU NYERERE NA KUMUENZI SANA TU MANA ALIPOKAZANIA TUTUMIE KISWAHILI ALIKUA UNAFAAMU NI NINI NA NI WAPI TUNAPOELEKEA BILA KUANGALIA ILI TUSIJE KUWA KITUKO
kama wameshindwa kwa dar,tanga,moshi... je uo umbali wote watauweza??
mfano ni Dar es salaam tu tusiende mbali yan kwel watanzania tunadanganywa sana..
arusha mjini kwenyewe shida na sehemu za nje ya mji, je iwe uko vijijini????
miaka yote alikua wapi hadi awambie kipindi cha uchaguzi

Kumbuka pia ni lazima uvuke mto Wami toka Ruvu kwenda Umasaini....illogical
 
Sasa kama billion 30 zinaweza kutoa maji Ruvu mpaka umasaini, then Dar peke yake haitahitaji zaidi ya billion 10 lakini maji watu hawayajui. Vilevile haiingii akilini kama CCM wanaweza kutumia Tshs > 50 billion kwenye kampeni za JK pekee iwaje leo waseme 30 billion ni nyingi na wanatafuta mhisani??

Duh!!!Mkuu umenigusa sana na comment yako makini na ya ukweli!
 
Huko umasaini si ndo amesema atahimiza ufugaji wa SAMAKI (Tanzania Daima) mie sina mbavu. Mmasai na SAMAKI. mmhhhh jamani yaani mpaka naishiwa na maneno nabaki nsikitika.
 
Back
Top Bottom