JK asifiwa kuhusu OBAMA

Kwa taarifa yenu, niliwahi kumsikia hata Nyerere akichapia; Mkapa, Mbeki, Obasanjo, Moi, Museveni na wengine wengi tu!!!!!
 
Rais wa Tanzania anatakiwa atoke among the best of our minds.Mimi nakataa kuwa the best of our minds hawajui hata Kiingereza.

Pundit,

Nafikiri ukoloni umekutawala kweli kweli. Unafikiri elimu ni kiingereza?

Prove kwetu hapa kwanini unafiri wewe ni bora kuliko JK?

Mambo mengine ni ushamba uliozidi kiasi. Unataka Mtanzania aongee English kama Mwingereza au Mmarekani, je itasaidia nini?

Hata Waingereza wenyewe tena watu kama waandishi wa habari, bado wanafanya makosa hasa hilo la kutumia he huku kuna possibility ya kuwa she. Hiyo ni matokeo ya mazoea kwani marais wengi ni wanaume.

Give us a break! na huo ujuzi wenu wa Kiingereza, tuambie angalau hata umeandika vitabu vingapi basi vya kiingereza ili wanetu wafaidike.

Watu wanashindwa hata kuja na mambo ya maana bado wanadharau wenzao kwasababu tu wanaongea kiingereza cha Kibantu?
 
Yes, he should!! Do you always speak good (grammatically correct)English? I will give a pass to anyone whom English is their third or fourth language. It's not easy. Not easy at all. I am around native English speakers everyday who don't always speak grammatically correct English...Hata sisi wenyewe hatuzungumzi Kiswahili fasaha kila siku. Msikilize hata Mwanakijiji kwenye matangazo yake. Saa ingine ana-stumble (sijui Kiswahili chake) akitafuta (ma)neno. Au msikilize yule dada mwenye kipindi cha mapenzi bongoradio....saa ingine hata maneno ya kiswahili hayajui na matokeo anakuwa anachanganya kiswahili na kiingereza.

Its true Nyani Ngabu!
 
Kiingereza cha kuongea na kuandika ni vitu viwili tofauti. Katika kuongea, kila mwongeaji hufanya makosa ya kifasihi na kisarufi(Grammatical and Syntactical errors(?)). Hata katika lugha ya kiswahili ambayo wengi wetu tunajidai kuifahamu tunaongea na hata kuandika makosa mengi tu ya kisarufi na kifasihi. Mara nyingi katika kuongea, kinachotakiwa ni ujumbe ufike kwa yule aliyekusudiwa, na mara nyingi makosa ya kifasihi na kisarufi ni vitu visivyoepukika.

Hata hivyo, katika kuandika kuna nafasi ya kupitia mara kwa mara kile unachoandika na kurekebisha makosa(japo bado yanaweza kuwepo), hivyo kupunguza hayo makosa.

Hata kule uingereza/Marekani watu (wengi) hufanya makosa katika kuongea kwa maana ya kisarufi na kifasihi. Hivyo basi, asilaumiwe JK,Bush au yeyote kwani hayo hayaepukiki kwa mtu yeyote yule.
 
Kwa taarifa yenu, niliwahi kumsikia hata Nyerere akichapia; Mkapa, Mbeki, Obasanjo, Moi, Museveni na wengine wengi tu!!!!!

Na mimi nilishawahi kumsikia Ahmed Tejan Kabbah akiwa so eloquent nilitamani siku moja rais wa Tanzania aweze kuongea vile.

Clearly you are not equating Kikwete to Mkapa,Mbeki or Obasanjo in that department, are you? Toa reference, two wrongs do not make a right.Even if the said president's did bungle a verb or two, still it doesn't make it right for Kikwete to do the same.We demand the best in every aspect from all our leaders.

If just expressing themselves is a problem what do you expect in international negotiations which involve 3d chess underwater with no gas masks while swimming with sharks without being eaten alive?

English is the least qualifications, and we are dismissing even that!
 
Nyani Ngabu,

..kwenye mkutano wa Davos mwanamama waziri wa mambo ya nje wa Nigeria alikuwa anashuka pointi kuliko Raisi wetu Jakaya Kikwete.

..mbona Dr.Asha Rose Migiro anazungumza vizuri na kupangua maswali kuliko huyu mheshimiwa sana Jakaya Kikwete?

..alichoboronga Kikwete siyo grammar na matamshi tu, ameboronga mpaka content.

Jakaya Kikwete said:
well, our excitement is that President Bush is at the end of his term, and the U.S. is going to get a new President, whoever that one is.

..Tumshukuru MUNGU kwamba matamshi hayo ameyatoa magogoni-DSM na siyo White House. Wachekeshaji kama Jay Leno na John Stuart wangeanza kuyatumia matamshi ya JK kwenye vipindi vyao.
 
Na mimi nilishawahi kumsikia Ahmed Tejan Kabbah akiwa so eloquent nilitamani siku moja rais wa Tanzania aweze kuongea vile.

Clearly you are not equating Kikwete to Mkapa,Mbeki or Obasanjo in that department, are you? Toa reference, two wrongs do not make a right.Even if the said president's did bungle a verb or two, still it doesn't make it right for Kikwete to do the same.We demand the best in every aspect from all our leaders.

If just expressing themselves is a problem what do you expect in international negotiations which involve 3d chess underwater with no gas masks while swimming with sharks without being eaten alive?

English is the least qualifications, and we are dismissing even that!

No, I'm not equating Kikwete to any one of them. Each one has their strengths and weaknesses. I mentioned them to highlight the fact that if the language is not your mother tongue, you are bound to make some grammatical errors here and there no matter how fluent you are in that foreign language and in no way am I saying it is okay. However, it is understandable and not such a big deal to ( at least not to me) fuss about!

As for reference, well, that would very tedious for me to go and search the world wide web for African ( or any other) head(s) of states who butcher the English langauge.

For some, it does seem that the mastery of the English language trumps all else including competency and accountability. Not to me sir! I could care less of how well Jakaya Kikwete speaks English than I care about him being a competent leader who puts the interests of his country first and ahead of everything else.
 
Oh by the way, has any one ever noticed that the current U.N. Secy. Gen. Ban Ki-Moon doesn't speak the best English out there...?

And, I've also heard his deputy, Asha Migiro, use tenses that weren't correct. I'm not saying she unknowingly used the wrong tense but she surely used it repeatedly. But I gave her a pass because it doesn't mean that she's not competent at what she's doing.....
 
Mbona siipati, hivi hili swali ni mtu gani anayejua diplomasia au uungwana angeshindwa kulijibu? Labda kama hatukudhani JK angeweza kulijibu kwa uelewo wake. Hii inasikitisha kuwa hatumtegemei Rais mzima wa nchi kujua diplomasia. Haya wanaompongeza wampongeze na kuandamana Bush akiondoka. Ila ajue bado hatujasahau tunasubiri kuendelea na kushughulikia mafisadi.
 
Unajua tatizo letu Watanzania tunadhani kujua lugha ya kingereza ni ishara ya usomi na siku zote mtu akijua kingereza hata kama ni mbumbumbu wa kutupwa basi ataonekana msomi. Ndio maana tunaishia kuajiri illiterate kutoka West wasio na elimu ya kutosha kisa tu wanajua kingereza. Hongera JK umefanya kazi nzuri kwenye Press Conference na Bush.
 
Pundit,

..JK served as a Min' of Foreign Affairs for 10 good years. English, not swahili, is the official language of our government. He should have no excuse for not speaking good english.

Hapana bwana hili kosa ni dogo mno wala sio la kubebea bango. Wakati mwingine watz tunazidi kujishusha; mbona miafrika mienzetu huwa inapuyanga tu kiingereza tena inakosea sana tu lakini sisi tunakuwa too keen ndio maana matokeo yake tunakosa confidence ya kuongea kiingereza mbele za watu. Waangalieni wenzetu wa Nigeria wanakosea sana tu kiingereza tena pronounciation ni zero, lakni hawababaiki wanakwenda tu. Vilevile mbona tukikosea kuongea kiswahili hatu-mind vile lakini ikija kiingereza inakuwa issue, lugha ambayo to some of us ni ya tatu hata ya nne? Hapa napo tunahitaji ukombozi, uzuri wa hili tatizo kulitatua hatuhitaji dola za Bush, ni kubadilika kichwani tu basi!
 
Unajua tatizo letu Watanzania tunadhani kujua lugha ya kingereza ni ishara ya usomi na siku zote mtu akijua kingereza hata kama ni mbumbumbu wa kutupwa basi ataonekana msomi. Ndio maana tunaishia kuajiri illiterate kutoka West wasio na elimu ya kutosha kisa tu wanajua kingereza. Hongera JK umefanya kazi nzuri kwenye Press Conference na Bush.

Kweli kabisa mazee!! Kuongezea tu, kasumba yetu inatufanya si tu kuona mtu ajuaye kiingereza kuwa ni msomi bali mwenye akili pia!! Yaani ukiwa unajua kiingereza unaonekana mwenye akili kama vile wasiojua kiingereza hawana akili!! Tunashangaza sana saa ingine
 
Sasa wale wasioongea Kiingereza kabisa akina Chavez na Hu tunawaweka ktk fungu gani?

Ikiwa bado tunaamini kiingereza kizuri ndio kipimo cha uwezo basi tuna safari ndefu mbeleni... ( By the way Im sorry for my broken swahili)
 
Hapana bwana hili kosa ni dogo mno wala sio la kubebea bango. Wakati mwingine watz tunazidi kujishusha; mbona miafrika mienzetu huwa inapuyanga tu kiingereza tena inakosea sana tu lakini sisi tunakuwa too keen ndio maana matokeo yake tunakosa confidence ya kuongea kiingereza mbele za watu. Waangalieni wenzetu wa Nigeria wanakosea sana tu kiingereza tena pronounciation ni zero, lakni hawababaiki wanakwenda tu. Vilevile mbona tukikosea kuongea kiswahili hatu-mind vile lakini ikija kiingereza inakuwa issue, lugha ambayo to some of us ni ya tatu hata ya nne? Hapa napo tunahitaji ukombozi, uzuri wa hili tatizo kulitatua hatuhitaji dola za Bush, ni kubadilika kichwani tu basi!

Kitila unanifurahisha sana siku hizi...hapa nilipo nacheka kama sina akili nzuri!! Eti Miafrika mienzetu...hahahahaha...kweli sisi Miafrika tuna mambo!!!
 
..jamani kinachogomba ni CONTENT ya kile alichozungumza. hilo ni tatizo kwa mtu aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje kwa miaka 10 mfululizo.

Jakaya Kikwete said:
well, our excitement is that President Bush is at the end of his term, and the U.S. is going to get a new President, whoever that one is.

..Hilo jibu hapo juu ndiyo lina matatizo. Linaonyesha kwamba Raisi wetu, hata baada ya miaka 10 pale Foreign, na miaka 2 ya Uraisi, hajaiva kidiplomasia.
 
Kwa kweli inasikitisha sana kama watu watapima uwezo wa mtu hata kidiplomasia au kiutendaji kwa kujua kiingereza.Mbona basi baba zetu waliosoma darasa la nne la zamani walikuwa wanajua kiingereza sana,lakini bado performance yao serikalini ndio imekuwa mbaya zaidi.Lugha ni kuweza kuitamka,kuiandika na kueleweka na upande wa pili.Hayo mataifa ya magharibi yaliyokuwa yakikosoa ina maana hawakuelewa Kikwete alichozungumza au walitaka fani na sio maudhui?Hata kusema we are excited Bush kuondoka haina maana anamchukia Bush,mtu anapomaliza muda wake wauongozi vizuri lazima tuwe excited.Hii kasumba ya kuutukuza uingereza wakati hata European Union wenyewe wameanza kuondokana na kasumba hiyo inatupeleka pabaya.
Nakubaliana nanyi english ni international language na viongozi wetu wote ikiwa ni pamoja na sisiwa jf tunapaswa kuijua,lakini si kipimo cha maarifa.Unaweza zungumza lugha yoyote ile na bado ukawa kiongozi mzuri tu.Hapa Uk,penyewe pana english tofauti,scottish,Irish nk.Isitoshe lugha ya kiingereza kwa mtu ambaye si lugha yake ya kwanza lazima apate shida,wee herufi "a2 mara inasomwa a,mara e,mara i,kujua yote hayo unapaswa kuwa mzungumzaji sana,sasa maisha yako yote 85% unazungumza kiswahili,15% tu unazungumza kiingereza sekondari,chuoni,mikutano ya kimataifa n.k.unategemea utajua kiingereza kama wao?
Wabongo kwa kujidharau bwana,sijui tutaishia wapi hakuna hata kitu kimoja tunachojithamini wenyewe,na ndio maana utakutana na mijitu pyua mibongo huku nje,inajifanya haijui kiswahili.Basi mtu unacheeeeeka halafu hilohilo kesho linategemea likirudi bongo tulipe ubunge au urais na mikasumba yake ya magharibi.
Acheni hizo.
 
Yes, he should!! Do you always speak good (grammatically correct)English? I will give a pass to anyone whom English is their third or fourth language. It's not easy. Not easy at all. I am around native English speakers everyday who don't always speak grammatically correct English...Hata sisi wenyewe hatuzungumzi Kiswahili fasaha kila siku. Msikilize hata Mwanakijiji kwenye matangazo yake. Saa ingine ana-stumble (sijui Kiswahili chake) akitafuta (ma)neno. Au msikilize yule dada mwenye kipindi cha mapenzi bongoradio....saa ingine hata maneno ya kiswahili hayajui na matokeo anakuwa anachanganya kiswahili na kiingereza.

Watanzania by far hatujui lugha, Kiswahili au Kiingereza, mfano ni bodi hii hapa.

Tatizo ni kwamba, ingawa tuna wachache wanaoshine, hatuna system ambayo hairuhusu watu kupanda kwa merit.Rais wa Tanzania anapatikana kwa politiki nyingi kuliko merit.Kikwete hkupanda kwa merit ila kwa politiki. Waliompigia kura wamepata walicho deserve.
 
..jamani kinachogomba ni CONTENT ya kile alichozungumza. hilo ni tatizo kwa mtu aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje kwa miaka 10 mfululizo.

Content can be debated; lakini wenzako wengine hapa wameng'ang'ania Kiingereza, ambacho kwa kweli wengine hatujaona kama ni big deal. Hata hiyo content kwa kiwango cha Rais wetu mimi binafsi naona hii ya jana alijitahidi sana; I think this was his best performance tangu aanze siasa. Kwa wale waliosikiliza mahojiano yake na Shaka Ssali wa VoA pale Dodoma wanaelewa naongea nini. Watanzania tuache ujinga; tusitarajie kuvuna ambacho hatukupanda. Huyu JK uwezo wake unajulikana siku zote tangu akiwa waziri, Lipumba na wengine wengi walituonya kwamba hili la urais ni zito mno kwa JK tukamwona Lipumba kichaa. Halafu ghafla tunataka JK awe kipanga kwa kuwa amekuwa Rais? Kuna tatizo bado tunalo katika ile nchi, watu wanafikiri ukishakuwa kiongozi unaongezewa akili. Ndio maana leo mijitu inamsifia Mizengo Pinda wakati tunajua huyu uwezo wake ni mdogo mno siku zote, sasa sijui kaongezewa akili baada ya kupewa uwaziri mkuu!!??

Tuache uzembe, kama tunataka viongozi vipanga tuwapate wakati wa uchaguzi sio wakishachaguliwa. Kama kweli tulikuwa tunataka mtu wa kutufanya tucheke kwenye ma-forum makubwa kama haya tungemchagua Salim au Lipumba au Mwandosya. Hawa ndio vipanga wa hizo content na lugha yenyewe katika wagombea tuliokuwa nao. Sasa hawa tuliwakataa tukamchagua huyo tuliye naye leo tunashangaa akishindwa kumudu mambo makubwa, ebo sisi vipi?

Binafsi namsifu JK kwa speech yake ya jana maana naona ame-improve sana nikimlinganisha na anapotoka. Ni wazi akina Salva walifanya kazi kubwa. Yes, it's was very low for such an important forum, but quite high compared to his previous performances, yaani alivunja record yake mwenyewe.
 
Kweli lugha ni kitu muhimu. Lakini hata siku moja sijawahi kuona Foreign press (hususan zile kutoka nchi kama Marekani au Uingereza) zikimbeza kiongozi wa taifa jingine kwa kuzungumza kiingereza ambacho si fasaha. Pia vi-grammatical error vidogo vidogo sio nongwa hata kidogo. Hata Waingereza wanavifanya. Kufanya vikosa vidogo vidogo kuwa nongwa tena kwa mtu ambaye si mzungumzaji asili wa lugha ni kuzidisha na kukuza mambo ambayo si muhimu. Ni wapi Afrika (au hata Duniani) ambapo kila kiongozi wa taifa anazungumza kiingereza fasaha mara zote?

nadhani hoja aliyotoa Pundit ni ya muhimu....kwamba mbali na vijikosa vya grammar kama ilivyoonyeshwa kwenye ujumbe tunaouongelea[ambavyo vinaweza kuvumilika]kuna suala la kuchafua ujumbe kwa kutumia neno 'excitement'pasipostahili. sidhani kwamba kikwete angeulizwa swali hilo kwa kiswahili angejibu na kuashiria maana ambayo inasomeka kwenye neno 'excitement'. kwa hiyo si vema tuanze kujipa moyo kwamba mapungufu kama haya si taabu kwa sababu tu eti vyombo vya habari vya nje havijakosoa wazi wazi.
 
Sasa wale wasioongea Kiingereza kabisa akina Chavez na Hu tunawaweka ktk fungu gani?

Ikiwa bado tunaamini kiingereza kizuri ndio kipimo cha uwezo basi tuna safari ndefu mbeleni... ( By the way Im sorry for my broken swahili)

Kama hujiu Kiingereza ongea Kiswahili watu watakuwekea interpreters. Ukishaongea Kiingereza maana yake unajua Kiingereza na ukikosea tunakulima kama kawaida.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom