JK apingwa kortini kugombea urais 2010

Tatizo hapa hamna kesi, hatujaonyeshwa sharti lililovunjwa na huyu bwana akiambiwa ahakikishie mahakama ni jinsi gani safari za JK zinafuja mali ya umma ni vigumu sana kuonyesha, hasa kwa sababu ni vigumu kuchanganua kwa uhalisi safari za raisi zinafanya kazi gani hata zile tangible tu, ukiachilia mbali zile intangible ambazo ndiyo kabisa kuzi quantify ni vigumu.

System yenyewe haina transparency, evidence yote iko classified hata ile isiyostahili, rais yuko juu ya sheria halafu yeye ndiye anayechagua majaji wote na mwenyekiti wa tume ya uchaguzi. Unategemea nini ?

Kesi inaweza kuburudisha watu, kuonyesha watu walivyochoka na kutoa msukumo wa kumpinga JK, lakini haina legal merit.

Legal merit, which is quite different from merit period. The law is an a.s.s.

It is not what happenned, it is what you can prove happenned.
Katika hiyo red ndilo la muhimu. Ni kweli kesi hiyo inaweza isiwe na nguvu yeyote kisheria ila ujumbe huo ni mkuu na unaweza kumharibia sana mkulu kisiasa.
 
Angekuwa Mtikila watu tungesema mzee wa kesi amezidi apuuzwe - mmhh linavyoonekana hili nalo neno mzee Mhozya ameamua anajitoa kwa faida ya vizazi vijavyo.
 
Hivi huyu malaria ana focus kweli? Mbona anaegemea kwenye udini sana?

Ungetaka afungue kesi kwa rais wa dini ipi nyingine?

Aisee unatia kinyaa.

Udini unatoka wapi hapa sasa?

Stop bahaving as if you have never seen the four corners of a classroom!!

grrrrrrrrrrrrrrrrr!!
 
“….ujio wa Jakaya na mtazamo wake wa masuala mbalimbali umeonyesha kuwa ile chachu ya maisha bora kwa kila mtanzania imeshindikana. Ile ndoto tuliyokuwa nayo ya kuipeleka mbele nchi yetu, naamini wakati wake umewadia kwa kuwashukuru watu kama hawa wanaowaza kumtoa Jah-Kaya kwenye urais ili angalau "Dr. Slaa/Nyerere wetu" atuvushe na kutuonyesha njia ya kufika Kanani; maana bado tumepotea porini (lost in the wilderness) na tunatangatanga.
 
Katika hiyo red ndilo la muhimu. Ni kweli kesi hiyo inaweza isiwe na nguvu yeyote kisheria ila ujumbe huo ni mkuu na unaweza kumharibia sana mkulu kisiasa.
Mkuu upo sahihi na hilo ndilo lengo kuu la mfungua kesi.
 
Hakuna haja ya kumharibia Rais wetu, Huko nje nasikia amepata kufahamiana na watu wengi sasa nchi yetu inafahamika sana Marekani, hata Obama ameshatujua Tanzania hivyo ataudhamini Tukienda Kukopa, Hakuna wa kutunyima maana tumeshajitangaza vyakutosha kuwa sisi ni aroro apweche. Sasa kama asingeenda hizo safari tungepata wapi wa kutukopesha? Hata hivyo vyandarua vilivyozua kashfa huko Temeke ni matokeo ya Hizo safari hata Bill klinton kaja mpaka Ntwara kuangalia kama matumizi ya fedha zake yameenda sawia au la japo niliona kile kituo cha afya kama changa la macho vile!!!!!!:bowl::bowl::bowl::bowl::bowl::bowl::bowl::bowl::tape:

Kwenye red: kumbuka vyandarua na millenium challange ($700M0 ni miradi ya Mmmchinga Mkapa. Jamaa hana cha kujivunia ! Sijui ameanzisha mradi gani vile? najua mtasema UDOM
 
Wanaodhani huyu Mzee anacheza wanakosea, alishaandika historia kwa UTHUBUTu na sasa anarudi tena kuandika nyingine.... siwezi tabiri matokeo lakini si wa kum-underestimate...
Mwalimu Paul John Mhozya v. Attorney General (No.1)
High Court (Samatta, J.K.): April 25, 1993
Civil Case No. 206 0f 1993

  • Civil Procedure-injunctions-injunctions against President- no injunction lies against President
  • Civil Procedure-Pleadings-defects-primary concern substance rather than form
  • Constitutional Law-institution of proceedings-protection of Constitution-right may not be used to grant remedy available only through parliamentary procedure
  • Constitutional Law-removal from office-Union President -jurisdiction- jurisdiction lies with Parliament and not courts under Constitution Ss. 42(2), (3), and 46A
 
Naomba kuwasilisha mawazo yangu, kwa heshima na taadhima. Hili swala limenigusa sana. Nampongeza sana Mwl. Paul Mhozya kwa hatua aliyochukua. Nadhani ni wengi tunaonung'unika chini chini tu. Tanzania, nchi ambayo raia tumezingirwa na upepo wa ahadi hewa na maneno ya asali kutoka kwenye vinywa vya miungu watu, eti nchi yetu ina amani na utulivu wakati haki zetu za msingi za kiraia zinaendelea kupuuzwa kila kukicha. Vilio vyetu vinapuuzwa, mbaya zaidi wanatukejeli raia na kutukana bila woga. Sisi sio muhimu, na kura zetu hazina maana? Sio walimu tu, au polisi na wafanyakazi wengine. Ki-mantiki, mlipa kodi yeyote ni mfanyakazi wa serikali. Serikali sio tu Rais, Mawaziri, Wabunge au vyombo vyake vya kutunga sheria na kuzisimamia. Serikali sahihi ni watu. Viongozi wanasimamia tu kwa mamlaka tuliyowapa sisi, au waliyopewa kwa niaba yetu na watu tuliowachagua. Ni waajiriwa wetu. Wanajibu kwetu. Wakiharibu tunawatoa au sio? Hiyo ndio maana halisi ya serikali ya demokrasia! Tatizo ni nini sasa? Mimi nadhani maana ya neno "Serikali" tafsiri yake imehujumiwa na watu wachache. Ni dhahiri kwamba Taifa letu la Tanzania linahitaji mapinduzi ya kweli, hasa ya kifikra. Amani? Utulivu? Mshikamano? Hivi ni vitu muhimu katika kuendeleza Taifa. Lakini hauwezi ukasema nchi ina amani wakati watu wengi tu wanalala na njaa. Sio tu kuwa ni njaa ya chakula, bali njaa ya maendeleo. Njaa ya haki. Hauwezi ukawa na mikakati ya kujenga taifa wakati wasimamizi wa ujenzi huo wanawaza tu kubomoa na kujijenga wao na familia zao. Biashara ndogondogo na ajira zetu zinahujumiwa. Rasilimali zetu muhimu hazitujengei maisha bora. Nenda leo sokoni ongea na muuza nyanya, halafu safiri kamsikilize na mkulima wa hizo nyanya. Nenda kamsikilize mwanafunzi wa shule ya kata, kamsikilize na mwalimu wake. Kamuulize na mfanyakazi yeyote wa umma, au kwa ufupi, mtanzania yeyote wa kawaida aliye karibu nawe. Muulize kama ana furaha. Ukishayatafakari majibu yote utakayoyapata, au ambayo unayo tayari sasa hivi, rejea tena kwenye barua ya Bw. Paul Mhozya hapo juu. Weka kando ushabiki wa kisiasa, urafiki au ubishi tu usio na maana. Jiulize tumetoka wapi na tunakwenda wapi? Nilimsikia Dr. Mohammed Ghalib Bilali juzi kwenye Hamza Kassongo hour, kipindi cha Channel Ten. Alijitahidi sana kujibu maswali tena kwa upeo mkubwa tu, akanivutia nimsikilize. Kuna jambo moja alihoji ambalo nadhani ni la msingi. Kwamba, Tanzania ipo moja tu na ndiyo nchi yetu pekee na wala hatuna pengine pa kwenda. Hivyo basi, na mimi nahoji, kama kweli serikali inaundwa na sisi wananchi, watanzania tunaoongozwa na katiba, sheria na taratibu tulizojiwekea, hatutaweza kuendelea kamwe katika Taifa hili endapo tutaendelea kubweteka tu na kunung'unika chini chini tukamwachia kazi Bw Paul Mhozya na wengine wachache wajaribu peke yao kutetea haki zetu. Tuwaunge mkono sio tu wanaotufaa, bali wanaofaa kwa maendeleo ya kweli ya Taifa hili. Hizi sio nyakati tulizozizoea, Dunia ya leo siyo ya jana. Inabidi tubadilishe mtazamo wetu wa kifikra. Kesi hii nadhani iwe chanzo tu cha mabadiliko hayo. Ahsanteni.
 
hizi ni siasa za kina mtikila tu hizi, huyu jamaa si ndo alimfanyia hata mwinyi kuhusu OIC ile kesi yake kama nakumbuka alishinda...however, hapa anampandisha tu jamaa chart, hakuna chochote hapa, hamna kesi..wanatuzuga tu na kutuchanganya akili na kutaka tuelekeza mawazo yetu hapo na kusahau hoja za msingi ambazo tulitakiwa kufikiria...ni bora kumpuuza tu na mtikila pia...
 
kwannini afungue kesi kwa marais wa dini fulani tu?

Hivi jamani kwa nini kuna watu humu wanashindwa ku 'think outside the box'?

Yaani hawaoni kitu zaidi ya dini kila mjadala unapowekwa hapa.

MS unaudhi!! Huo udini wako utakupeleka pabaya
 
Ofcourse mtoto hawezi kumshinda kesi baba yake ambaye ndiye head of the family, lakini yatosha kwamba message is sent and delivered. Tunajua hakuna mahakama Tanzania itakayokuwa na ubavu wa kumpandisha kizimbani mkuu wao hata kama inakuwaje, kwani wabongo tumejaa unafiki. Angalau mwalimu ametusaidia kumwambia hatupendi anavyotulaza njaa kwa visingizio kibao vya kwenda huko ulaya kutanua na wapambe wake
 
Vizuri kwani kanisa katoliki limejipanga vyema kuhakikisha hasiye rc hatakiwi kushika ukuu wa nchi hii kwa kudhani eti tz ni yao,na ndio maana wakaamua kumuunga mguu padri slaa,hata hivyo aliyepewa kapewa na hajaanza yeye kujaariwa watatu wamejaariwa ambao ni mkatoliki jkn,mjahidina ahm na mkatoliki tena bwm.kumbukeni kuwa lowasa anachukiwa sana kwavile si mkatoliki na ndio maana jmk aliamua kumpa uwaziri mkuu mkatoliki mkpp ili kelele zipungue.sisi wote tunajua kinachoendelea kati ya rc na chadema lakini mwisho wake mtakiona.sisi wakkkt na wengine ambao ndio wengi kuliko nyinyi wadini tumenyamaza kimya tukipiga upatu na tumeshaamua kumpa kura zetu zote jmk.
 
Uneongea nini?? haya sasa mumeanza uKKKT na uRC hivi ni nani aliyewaroga? Msitake kuweka issue ambazo sio ajenda za watanzania kuwa ajenda za kujadiri hapa. Hakuna mtanzania anayona tutaendelea au kurudi nyuma kwasababu ya Ukatoliki au uluteri. mambo ya Richmond hatukuwahi kuyahisha na dini unataka sasa tuanze kungalia kuwa ni nani wapo behind Meremeta? nani wapo behind Deep green? nani wapo Behind EPA? kwa mtindo wa dini?? unatupeleka kusiko. Rudi tafakari kama Tunasonga mbele kimaendeleo au hapana, awe muislam au mkristo, au muRC awe mpentekoste au Mlutheri tunataka bara bara, shule, hospitali, watu walale kwenye vitanda na madogoro, watu wanywe maji safi na salama, watu wale anagali milo 2 kwa siku. Hizo habari za kuwa na maturujia au hamna ubatizo wa maji mengi au kidogo hauna hayana mshiko hapa. Rudini kwenye ajenda nyie mliopotea
 
Hivi jamani kwa nini kuna watu humu wanashindwa ku 'think outside the box'?

Yaani hawaoni kitu zaidi ya dini kila mjadala unapowekwa hapa.

MS unaudhi!! Huo udini wako utakupeleka pabaya

Haya ndio mambo yanayoturudisha nyuma, udini na ukabila. MS anazingua.
 
Huyu kaanza na natumai na wengine watafuata,ila mzee ujiandae kuwakaribisha TAKUKURU,POLISI,USALAMA WA TAIFA nyumbani kwako hivi karibuni na kama una vimeo utakoma nao.
 
Tatizo hapa hamna kesi, hatujaonyeshwa sharti lililovunjwa na huyu bwana akiambiwa ahakikishie mahakama ni jinsi gani safari za JK zinafuja mali ya umma ni vigumu sana kuonyesha, hasa kwa sababu ni vigumu kuchanganua kwa uhalisi safari za raisi zinafanya kazi gani hata zile tangible tu, ukiachilia mbali zile intangible ambazo ndiyo kabisa kuzi quantify ni vigumu.

System yenyewe haina transparency, evidence yote iko classified hata ile isiyostahili, rais yuko juu ya sheria halafu yeye ndiye anayechagua majaji wote na mwenyekiti wa tume ya uchaguzi. Unategemea nini ?

Kesi inaweza kuburudisha watu, kuonyesha watu walivyochoka na kutoa msukumo wa kumpinga JK, lakini haina legal merit.

Legal merit, which is quite different from merit period. The law is an a.s.s.

It is not what happenned, it is what you can prove happenned.

Wacha mahakama watamjibu kisha mambo mengine yatafata.
 
NDG Kiranga ujue sheria haipo juu ya MUNGU, huo ndio mwanzo tu wa mpango wa Mungu kuikomboa nchi hii kutoka kwa utawala huu, MUNGU IBARIKI TANZANIA.

Ukimtegemea mungu utakufa bila kufanya lolote.Nchi kuwa na rais kama Kikwete ni moja ya proof kwamba hakuna mungu.

Hakuna mungu mwenye huruma kuu na uwezo wa yote anayeweza kuwapa watu rais rahisi kama Kikwete.
 
Back
Top Bottom