JK apata mshituko juu ya ongezeko la bei ya vyakula; aagiza serikali kuingilia kati

Angejaribu kupambanua namna gani serikali itaingilia kati kupunguza bei, isije ikawa kuwakandamiza wafanyabiashara wadogo na kuwaacha mafisadi papa wakipeta tu.
 
Hapana...unaposhusha kodi bei hupungua na watu hufanya manunuzi zaidi....kutokana na unafuu wa bei...watu watanunua zaidi(in terms of volumes) na wigo wa kodi kupanda....simple economics...kwa vile VAT sio production cost
hapana babu.....you need to check how elastic that demand is,we're talking about food here!!!
 
Hivi wachumi wanaomzunguka ****** pale magogoni wana kazi gan? Dah bora BEN kuliko huyu mtu...hata kiberiti kushusha bei hawawezi kweli?????????????:A S 13::A S 13:

Ni mkurupukaji asiye na maana. Mimi namjua huyu rais hakuna gazeti asilosoma mpaka ya udaku. Kinachoendelea mitaani anafahamu vizuri. Leo eti anakurupuka kujifanya anashangaa bei za vyakula ni unafiki mkubwa. Marais wa namna hii ndiyo hawatufai. Hiyo ndiyo tabia ya rais msanii na mpenda sifa zisizo na msingi. Nachojua mimi ataishia kusema hivyo na hakuna hatua itakayochukuliwa.
 
Bei ya petroli iko sh. 2,050/lita...., KASI ZAIDI kwa kwenda mbele!!!!!!
 
Ni wazo ambalo naweza kusema ni linatokana na emotional response and not from a rational one. Ni uamuzi uliotokana na kushtushwa.

a. Wakulima wa Tanzania wanazalisha vipi chakula? Nakumbuka nilikuwa miongoni mwa wakosoaji wa kampeni ya kuzalisha Jatropha ambapo vijiji vilibadilisha kutoka kulima mazao ya chakula na kuanza kulima Jatropha wakiadiwa hela ya haraka haraka;

b. Serikali yake ilitoa Stimulus Package katika sekta ya Uchumi wa zaidi ya Shilingi Trilioni 1.6 ni kwa kiasi gani fedha hizo zilienda kusaidia kilimo cha mazao ya chakula?

c. Kama mtu mwingine alivyoeleza hapo juu; unapotoa chakula cha ziada wakati prospect ya mazao mwaka huu bado inatisha kwa ajili ya lengo la kupunguza bei ya vyakula unajiandaa kwa janga kubwa zaidi. Itakuwaje akifanikiwa kweli kupunguza bei za vyakula (temporarily) kwa kuongeza bidhaa sokoni halafu baadaye mavuno yakawa mabaya na taifa likaanza kuwa na tatizo la njaa; NGR itakuwa haina chakula na kubidi kuagiza kutoka nje. Wale wanaoshangaa Tanzania kula Yanga wakati wa Nyerere, watapigwa na butwaa wakilazimika kula Yanga 2011!

d. Tatizo la chakula Tanzania ni la kujitakia; na linatokana na sera mbovu za Chama cha Mapinduzi.
 
cdm walisema nini kanda ya ziwa na yeye anatimiza tu kiaina na bado atafanya mengine tu pipoz power kumbe noma eh
 
Hana maana vipi kuhusu mfumuko wa mafuta? Coz fuel is everything on inflation rate. Mpaka cdm waandamane ndio atekeleze? Sh*t
 
Kweli jk ni hamnazo kweli!!

Yeye alikuwa wapi wakati chadema wanaandamana kupinga kupanda kwa bei za bidhaa na maisha!!!

Si yeye alisema chadema wanataka afanye mambo ambayo hata maraisi waliopita walishindwa??

Sasa haya maamuzi ya sasa alikuwa anasubiri lini ndiyo atoe!!!
 
Huyu jamaa waliopendekeza awe kiongozi wa nchi sijui waliona nini maana hata wizara alizokuwepo kabla ya hapo ameacha maneno mengi sana

Mkuu usifikiri kuwa Rais wa Tanzania ni sawa na rais kama wa Botswana, Namibia, South Afrika, Ghana, n.k. Rais wa Tanzania can be ANYTHING!!
 
Hivi kuna analoagiza likatekelezwa kweli? zaidi ya polisi tu ndio huwa wanatekeleza....

Bomu la Tumbo
 
Back
Top Bottom