JK apangua makatibu wakuu

HIVI DR. KOMBA ATAUWEZA UFISADI NDANI YA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII?

Tumwombee mwenzetu, maana ufisadi uliopo Wizara hiyo unaojumuisha mtandao wa viongozi wa Wizara hiyo na wa Chama kama akina Mulla, unahitaji moyo kweli kweli!
 
je aliwahi kuwapa ukweli wakuu wake wa kazi? kama sikosei dada huyo alishawahi kuwa idara inayohusika pia na pesa za nje pale hazina na hakuwa mtu mdogo sana je huko alikokuwa mambo yalikuwa shwari? au aliwahi kupiga kelele lakini kwa vile alikuwa mtu "mdogo" sauti yake haikusikika.

- Ukweli ni kwamba sielewi maana ya swali, labda niwaachie wengine wanaoelewa zaidi yangu.

Thanxs!
 
Kumuweka Dr. Turuka pale Utamaduni na michezo ni matusi kwa elimu ya huyu mtu.......similar to what happened to Mh Sarungi........hivi hawa washauri wa JK wanaangalia kweli CV za watu au basi tu ili kumpandisha mtu cheo.........!!

Ogan kuna hesabu nyingi sana zinapigwa wanapochaguliwa makatibu wakuu wa wizara mbalimbali, elimu ni moja tu kati ya vigezo. Kuna siasa nyingi inakuwa involved, Unajua mtu kama Prefesa Sarungi kutokana na profession yake hakutakiwa hata kuingia kwenye siasa. Lakini ni kuwa taaluma ya Siasa Tanzania ndio inalipa zaidi kuliko taaluma nyingine kwa hiyo tusiwalaumu sana.
 
Katika mchuano na mpambano huu wa hoja hapa JF naona kati ya kina Mchundo na FMES bado umo...Ila naona FMES amebadili tactics kwa ghafla na hivyo kumchanganya Fundi Mchundo kiaina..At least kwa wakati huu...Kwasababu FMES alishasema habari isiyokuwa na uhakika, na FM akaikosoa habari hiyo bila kutilia maanani kauli ya mwanzo ya habari hiyo kutokuwa na uhakika.
All in all hapa JF tuna uwezo wa kusoma katikati ya mistari na kwahiyo mambo hayawezi kuharibika provided tunaeleweshana pasi na matusi.

Lakini kaka kuna watu humu ndani wamezidii, utadhani mtu anakaa siku nzima kuangalia kama fulani kaandika kitu ili apinge, yaani badala ya kupinga na hoja anachambua maneno, kwamba hili neno au hili hayajakaa vizuri yaani utadhani mwanasheria ambaye anataka kushinda kesi kwa kupindisha maneno, na mara nyingine huwa hawaangalii maneno yaliyoandikwa na kuanza kubisha upuuzi, kama hapo mtu kashasema na yeye hana uhakika lakini bado wanataka kumhukumu na maneno yake (utadhani sio watu wenye akili zao na kuweza kuchambua kilichoandikwa). Wanakuwa kama watoto sasa.

Kasomeni kwanza niliyoandika ndiyo mhukumu. Mimi nilikuwa ninatia shaka na habari iliyoletwa. Sikumhukumu mjumbe. Kwa kuonyesha kuwa hata nilielewa hata yeye habari alikuwa anaitilia shaka, nika-bold alivyosema hivyo. Sasa haya ya upuuzi, kutokuwa na akili, utoto yametoka wapi? Nimepinga mtazamo kuwa kwa vile Mramba amefanya vikao kwenye hoteli inayosemekana ni ya baba wa mkwe mtarajiwa wake basi ni lazima vilikuwa ni vikao vya kufanya hujuma dhidi ya utawala uliopo. Kwamba vikao hivyo vilikuwa vya kupanga urais wa EL. Halafu kuwa kwa sababu mwenye hoteli amemuoza mtoto wake kwa mtoto wa Mramba, basi huo ni uthibitisho wa haya yote! Sasa maneno gani nimechambua badala ya hoja?

Sasa, Lusajo, wewe unaamini kipi? Kuwa habari ni sahihi, kwa hiyo FMeS asiwe na wasiwasi na taarifa yenyewe au kuwa habari si sahihi, kwa hiyo FMeS ana haki ya kuwa na wasiwasi? Au ni hoja gani unayoizungumzia ambayo mimi mtoto sijaielewa?

Lakini kwa nini najisumbua kujielezea? Aminini mnachotaka kuamini. Ndiyo uzuri wa www. Wote tuko huru kufanya tupendalo. Hata kama tunakuwa kama hatuna akili. Pengine kweli hatuna akili!

Nilikuwepo.......
 
Nimepinga mtazamo kuwa kwa vile Mramba amefanya vikao kwenye hoteli inayosemekana ni ya baba wa mkwe mtarajiwa wake basi ni lazima vilikuwa ni vikao vya kufanya hujuma dhidi ya utawala uliopo. Kwamba vikao hivyo vilikuwa vya kupanga urais wa EL.

- The point missed ni kwamba ndio maana akanyimwa dhamana makusudi ili akose harusi, kuwakomoa ndege wawili kwa jiwe moja.

Otherwise big deal for nothing! na waste of time and space kwa wananchi.
 
pamoja na Blandina Nyoni anayekwenda Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii akitokea Maliasili na Utalii.

- Another kichwa, saafi sana maana huko Afya kumeoza sana, kunahitaji kusafishwa. na huyu atawasafisha wawe clean.
 
- Wananchi angalieni another scenario inayotembea mjini leo sina uhakika na ukweli wake, inasema hivi:-
kulikuwa na vikao vya siri vya kamati za el kugombea urais vilivyokuwa vikifanyika katika hotel ya mzee mmoja mjini anayeitwa Msiba. vikao hivyo vilikuwa vikiongozwa na mramba. na leo mtoto wa mramba ameolewa na mtoto wa huyo msiba. kwamba harakati zimewaka moto za 2010 kwa sababu makubaliano ya mtandao yalikua muungwana atawale term moja tu amuachie el lakini sasa anaonekana kukiuka makubaliano.
Fundi Mchundo
FMES alisema hivyo, kwamba kuna habari inasema hivyo ila hana uhakika, na wewe badala ya kuja na hoja ya kukubali au kupingana wewe unauliza maswali na kutaka majibu ya maswali ya kitu ambacho FMES kauliza, na yeye ameuliza ili kama ilivyo kawaida ya JamiiForum watu wengine wanaongezea data juu yake lakini sio wamuulize maswali, na wewe unamjua vizuri FMES kama ana uhakika na alichokisema huwa anasema hivyo na kama hana uhakika anasema na watu wengine wanachangia kumuambia kilichotokea au kuongezea maneno. Na jamaa unajua kwamba huwa anatoa data hata wakati hata kikao kinaendelea na mara nyingi inakuwa kweli na kesho yake unazikuta kwenye vyombo vya habari. Kwa nini na wewe usije na hoja zako? nilitumia neno kama watoto kwa sababu kama hujaelewa hicho nilicho-quote hapo juu basiii.
 
Bongolander said:
Unajua mtu kama Prefesa Sarungi kutokana na profession yake hakutakiwa hata kuingia kwenye siasa.

Bongolander,

..Prof.Sarungi alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Muhimbili kabla ya kuingia siasa. Hiyo ilikuwa baada ya kupanda ngazi toka kuwa daktari wa bingwa na mhadhiri mpaka kufikia Proffesor.

..Ukiwa DG pale Muhimbili ni mara chache sana kuwa na clinic na kuona wagonjwa. Majukumu ya DG ni management na administration kuliko utabibu.

..Sarungi alishatoa mchango ni mkubwa tu ktk taalum aliyosomea. kwamba aliamua kushiriki siasa huo nadhani ulikuwa ni uamuzi wake na hatupaswi kuulaumu.

..siyo jambo la ajabu kwa wanasayansi mahiri duniani kujiunga na siasa. Waziri Mkuu wa kwanza wa Israel Prof.Wisemann alikuwa mkemia aliyebobea. Senator.John Glen wa USA ni mwana-anga mashuhuri kabisa duniani. i can go on and on.

..
 
Huu ni uteuzi unaofaa sana kwa taifa, maana huyu sister hana mchezo ni kazi tu I can't wait siku atakapokuja kuwa waziri mkuu, maana mbingu zitashuka.

Nakumbuka siku moja mkutanoni Paris alivyomshangaza muungwana akiwa waziri, kwa kuiita hoja yake kuhusu uchumi wa bongo kuwa ni nonsense na kwamba anahitaji kwenda kufanya homework, duh! mkulu hakuamini kuwa huyu dada ana huu ubavu!

Na pia ninakumbuka wakati tunasubiri cabinet ya kwanza ya awamu ya nne kutangazwa, nilimuuliza vipi, akasema baada ya ile ya Paris haamini anaweza kupewa anything, huyu sasa anaondoka kumbe muungwana huheshimu wanaoweza kumpa facts usoni bila uoga.

Saafi sana sister Joyce wembe ni ule ule kumkoma nyani usoni tu, najua upo hapa respect na nitakutwangia later!

Mkuu FMES,

According to the data,ni kuwa Bibi Joyce Mapunjo kahamaishwa pale baada ya kuwapo ugomvi wa muda mrefu kati yake na Omari Chambo,Huyu mama ni kiboko na hapendi mambo ya usanii na kuleteana siasa ndani ya kazi.

Uteuzi mwingine wa mama Nyoni kuhamishiwa pale wizara ya Maliasili ni kutokana na yeye kutoelewana kabisa na mama Mwangunga na hadi ilifikia kipindi yule mama alishwahi kumshartaki kwa Mkulu wa Nchi kwamba anamkwamisha.Kumbuka mamama nyoni alitolewa pia wizara ya Fedha baada ya kuwa na Ugomvi na CAG.wanashindwa kumtoa sababu ni mchapa kazi na hawana sabau ya kumwangamiza.

Kuhusu Mgonja,Muda wa kustaafu ulshafika na tulijua muda mrefu tulishajua aytaachia ngazi.Kuhsu kufunguliwa mashtaka sidhani kama itawezekana sababu kuu ni kuwa alikuwa ni mjanja sana katika hizi dili na hakuna hata sehemu moja aliyohusika wazi.

Hata suala la Kagoda yeye hawakuwapo wakati linapitishwa,yey aliletewa tu bada ya kina balali na baadhi ya wakulku flani kulifanyia maamuzi tayari,yawezekana yeye alipewa tu asante.Mgonja alikuwa natoboa bomba tu kupata maji ili hakuwa bomba la kupitishia maji.

 
Haya tumeyazoea kila siku tuu. Ina maana Rais hawezi kuwachagua wataalam wake wenye sifa na uzoefu wa kuongoza au kuratibu kazi za Wizara??? Kuna tatizo katika uteuzi wake. Believe me or not, ukweli ndo huo. Yaani leo Katibu Mku anapewa dhamana ya kuratibu shughuli za Wizara kesho unaona hayuko competent unamhamishia Wizara nyingine, huo tunaweza kuuita uteuzi wa try and error!!!!! Matokeo yake hawa Makatibu Wakuu wanakuwa kwenye Wizara kabla hata hawajamaliza kudesa sera na sheria za Wizara husika na kazi za pale basi wanahamishwa. Hii inakwamisha utendaji maana Katibu Mkuu anahamishwa akishazoea kufanya kazi za Wizara husika then anahamishwa tena akawe kwenye sijui tuite Probation Period, ikimalizika unasikia tena anahamishwa!!!!! Jamani huu si ufanisi wa kazi bali ubomoaji. Inakera.
 
Katika siku hizi za karibuni Rais Kikwete amehamisha makatibu wakuu na manaibu wao.Sababu iliyotolewa ni kwamba Grey Mgonja na wengine wanastahafu kwahiyo ni katika harakati ya kuziba mapengo.Sawa,lakini kama sababu ni hiyo, kwanini mapengo yasizibwe kwenye zile wizara tu ambazo zina wastahafu na badala yake iwe "mass movements?"Nadhani kuna sababu nyingine ambayo hatujaambiwa.Lakini hasa mabadiliko haya yanalenga nini kuongeza ufanisi?Sidhani, kwasababu kama yangelenga ufanisi Turuka, ambaye ni mtu wa uchumi asingepelekwa Ustawi wa Jamii.Mimi ni mtu ambae ninaamini kwamba ili mtu aweze kuwa na "output" ya maana,haina budi kumpeleka kwenye fani yake.Sasa haya mambo ninayo yaona kwenye serikali yetu yakumweka au kumpeleka mtu mahali ambapo ni tofauti na fani yake kabisa yanashangaza,"how can he perform and have desirable outputs?"Haya ni baadhi ya matatizo.Lakini tatizo lingine ambalo linaweza likafanya kusiwe na ufanisi ni kama hakuna utafiti wa kina uliofanywa kutathmini historia na utendaji wa wahusika.Tumeshasema na kuishauri serikali mara nyingi kwamba uteuzi wa watendaji wakuu wa umma ufanyike kwa uangaifu.Hata ikibidi usalama wa taifa uhusishwe katika tathmini hiyo.Nasema hivyo kwasababu huko nyuma tumeshuhudia teuzi zilizokuwa na dosari nyingi,hata kuliingiza taifa katika matatizo makubwa.Sina shaka kabisa kwamba katika uhamisho Rais alioufanya, tathmini ya kina ya kiutendaji ya kila mhusika imefanyika na hatutashuhudia tena matatizo tuliyoyaona huko nyuma.Kila la heri Rais wetu katika "kasi yako mpya" ya kuwashughulikia mafisadi.
 
Wakuu Joyce Mapunjo and Blandina Nyoni ni wapambanaji, ni wachapa kazi. Kwa mfano huyu Mapunjo haogopi kumkosoa hata bosi wake inapokuja issues za bla bla. Mama anataka kazi ifanyike na pia anajali sana maslahi ya watumishi wake popote pale alipo. Ikumbukwe kuwa alipokuwa Naibu Katibu Muu Fedha, alidumu pale kwa muda mfupi sana akahamishiwa iliyokuwa Wizara ya Mipango, Uchumi na Uwezeshaji. Kwa hiyo dili nyingi za Wizara ya Fedha naweza kusema hakuhusika hata kidogo ukizingatia hakuwa full PS. Pale Mipango alijitahidi kupanyoosha vilivyo, japo alikuwa Naibu Katibu but she did wonders!!! Ukitaka proof jaribu kumpata mutimishi wa Mipango enzi za Mapunjo atakushuhudia, hata Fedha walikuwa wanampenda sana. Alipohamishwa wengi walisikitika kwani walikubali kuwa wamepoteza mchapakzi ma mtetezi wa maslahi ya nchi na watumishi. Kwa Nyoni nasikia tu ni mchapakazi mzuri na huwa hapendi kulea ubadhirifu na inasemekana alitofautiana na bosi wake katika kupitisha mambo fulani fulani ikabidi ahamishwe maana alionekana kikwazo ila wakashindwa tu kumwondoa katika uandamizi wa serikali kwa kuwa wanaheshimu kichwa chake (akili inachemka) na ni mchapakazi.
 
Fundi Mchundo
FMES alisema hivyo, kwamba kuna habari inasema hivyo ila hana uhakika, na wewe badala ya kuja na hoja ya kukubali au kupingana wewe unauliza maswali na kutaka majibu ya maswali ya kitu ambacho FMES kauliza, na yeye ameuliza ili kama ilivyo kawaida ya JamiiForum watu wengine wanaongezea data juu yake lakini sio wamuulize maswali, na wewe unamjua vizuri FMES kama ana uhakika na alichokisema huwa anasema hivyo na kama hana uhakika anasema na watu wengine wanachangia kumuambia kilichotokea au kuongezea maneno. Na jamaa unajua kwamba huwa anatoa data hata wakati hata kikao kinaendelea na mara nyingi inakuwa kweli na kesho yake unazikuta kwenye vyombo vya habari. Kwa nini na wewe usije na hoja zako? nilitumia neno kama watoto kwa sababu kama hujaelewa hicho nilicho-quote hapo juu basiii.

Kumbe tatizo lilikuwa ni kumuuliza swali FMES? kwa mtaji huu, tutafika kweli?

Otherwise big deal for nothing! na waste of time and space kwa wananchi.

Agreed. Wholeheartedly!
 
Mgonja sasa tumsubiri Kisutu,mi naenda kaa pale entrance mpaka wamlete nimwambie SHIMBONY
KARIPU UYANENY!!
Alizoea kunawiri kiwiziwizi tu
 
JK si kweli kuwa hana washauri wazuri nionavyo mimi ni kuwa anapuuza na hasikilizi ushauri anaopewa. HAiwezekani washauri wake wote wakawa wapuuzi kiasi hicho lazima kuna wanaomshauri vema ila yeye tu... si unajua tena ukiitwa mkuu wa nchi how it feels.....................................!!
 
Kumbe tatizo lilikuwa ni kumuuliza swali FMES? kwa mtaji huu, tutafika kweli?

Fundi Mchundo hii ni mara yangu ya mwisho kukuandikia, kwa sababu kuna watu wawili mjinga na mpumbavu (Mods sina ubaya na mtu hapa ni mfano tuu) , kuna mmoja kati ya hao ambaye hata ufanyeje hawezi kukuelewa au hataki kukuelewa so good luck! upo hapa jamvini kutokea Fri Nov 2007 na wewe ni Expert Member humu kwa hiyo kama bado haujaelewa nini kinaendelea basii. Ni kweli nimesema unauliza swali kwa mtu aliyesema hana uhakika na habari aliyoipata sasa wewe unataka nini? tatizo sio kumuuliza FMES angekuwa mtu yeyote humu ndani ungemuuliza ningekushangaa! Kwa hiyo usinifanye nifikirie kwamba wewe ni mmoja katika watu niliowa-difine hapo juu (Samahani kama imekukera ila nauliza tuu) na hauna haja ya kunijibu maana sitaendelea kuandikiana na wewe.
NB: ninavyoona Expert Member huwa ninajua una uelewa mzuri na akili ya kuchambua vitu.
 
- Unajua this is incredible, ndio maana sasa watu wananilipa kuweka jina langu tu la FMES kwenye webb zao,

ahsanteni kwa wale the so called "maadui" zangu maana it could not have happened bila ya msaada wenu, hasa zaidi recently keep it up guys!

Maana I love it!
 
Fundi Mchundo hii ni mara yangu ya mwisho kukuandikia, kwa sababu kuna watu wawili mjinga na mpumbavu (Mods sina ubaya na mtu hapa ni mfano tuu) , kuna mmoja kati ya hao ambaye hata ufanyeje hawezi kukuelewa au hataki kukuelewa so good luck! upo hapa jamvini kutokea Fri Nov 2007 na wewe ni Expert Member humu kwa hiyo kama bado haujaelewa nini kinaendelea basii. Ni kweli nimesema unauliza swali kwa mtu aliyesema hana uhakika na habari aliyoipata sasa wewe unataka nini? tatizo sio kumuuliza FMES angekuwa mtu yeyote humu ndani ungemuuliza ningekushangaa! Kwa hiyo usinifanye nifikirie kwamba wewe ni mmoja katika watu niliowa-difine hapo juu (Samahani kama imekukera ila nauliza tuu) na hauna haja ya kunijibu maana sitaendelea kuandikiana na wewe.
NB: ninavyoona Expert Member huwa ninajua una uelewa mzuri na akili ya kuchambua vitu.

U-expert member haimaanishi kujua, kuelewa au kuwa mahiri wa kuchambua vitu. Hata wewe ukishatuma posting kadhaa utajikuta unaitwa expert. Haina maana yeyote. Kuweko toka mwaka jana na kwenyewe hakumaanishi kitu. Ninachokisema, kasome tena posting yangu. Pengine utaelewa. Kuna neno linaitwa rhetorical question. Ni swali ambalo halihitaji jibu.

Hamna taabu kama utanifikiri mimi ni mmoja wa watu uliowa-define hapo juu.

Kingine. Nielewavyo mimi ni kuwa hatuandikiani kwenye posting. Hii ni public forum na tunajibu kilichoandikwa na si kumjibu mtu. Kwa mfano, si lazima wewe ujibu posting hii. Mtu yeyote anaweza kuandika na kusema kuwa kilichoandikwa humu ni pumba. Ukitaka kumwandikia mtu, unampelekea message. Ukitaka wengine wasome ujumbe wako unamtumia visitor's message. Ukitaka iwe kwa ajili ya macho yake, tuma P.M.

Haujanikera. Najibu posting zako kwa sababu navuta posting zangu zifike 1999. Hamna kingine.

Turudi kwenye hoja.

Mimi ninaamini kuwa makatibu wakuu ni muhimu kuliko mawaziri maana hawa ni technocrats. Hawa ndiyo hasa viongozi wa wizara. Kwa mtazamo hiyo inabidi katibu mkuu awe na particular strnghts ambazo zinaendana na wizara anayoiongoza. Kwa hali hiyo, hii kuwahamisha hamisha inaelekea kuwa wao ni jack of all trades kiasi ambacho hawana umuhimu wa kujua kwa ndani mambo ambayo wizara zao zinasimamia. Mimi, hii inanitia wasiwasi.
 
According to the data,ni kuwa Bibi Joyce Mapunjo kahamaishwa pale baada ya kuwapo ugomvi wa muda mrefu kati yake na Omari Chambo,Huyu mama ni kiboko na hapendi mambo ya usanii na kuleteana siasa ndani ya kazi.

Uteuzi mwingine wa mama Nyoni kuhamishiwa pale wizara ya Maliasili ni kutokana na yeye kutoelewana kabisa na mama Mwangunga na hadi ilifikia kipindi yule mama alishwahi kumshartaki kwa Mkulu wa Nchi kwamba anamkwamisha.Kumbuka mamama nyoni alitolewa pia wizara ya Fedha baada ya kuwa na Ugomvi na CAG.wanashindwa kumtoa sababu ni mchapa kazi na hawana sabau ya kumwangamiza.

- Mkulu Gembe, saaafi sana tupo ukurasa mmoja hapa, wabunge wanam-miss sana Sister Nyoni maana alikuwa na tabia ya kwenda bungeni na kuwapa darasa kuhusu mahesabu ya taifa, anapotokea tu wabunge wote huacha kazi zao na kujipanga ukumbini kumsikiliza akimkoma nyani, niliongea naye jana na kumpa hongera kwa niaba ya wakulu hapa.

- Sister Joyce, huyo sina la kuongeza maana records zipo wazi, jana sikumpata maana alikuwa Milimani upare lakini leo nitampata amerudi mjini tayari, nimekuwa nikimfagilia kuwa bosi kamili kwa muda mrefu sana I can't wait kuongea naye kumpa hongera kwa kuwa bosi kamili.

- Wote wawili Mungu awazidishie na walitumikie taifa letu kwa nguvu zaidi na maarifa.
 
hii ni mara yangu ya mwisho kukuandikia, kwa sababu kuna watu wawili mjinga na mpumbavu (Mods sina ubaya na mtu hapa ni mfano tuu) , kuna mmoja kati ya hao ambaye hata ufanyeje hawezi kukuelewa au hataki kukuelewa so good luck!

- Kijana Lusajo,

Yaani kijana mdogo sana kama wewe unapoweza kuandika maneno mazito na yenye busara kama haya, ni faraja kubwa sana kwa taifa, kwa sababu ni vijana wadogo sana kama wewe wenye busara nzito kama hizi na uelewa mkubwa wa ishus, ndio viongozi wa kesho wa taifa letu,

Na the fact kwamba unaingia hapa kwa jina lako la kweli na ID moja tu, that is powerful kid and I am down, keep it up!
 
Back
Top Bottom