JK apaa kwenda Paris leo...

Natamani Mh. Dr. Slaa achukue nchi ili awe rais wa kwanza kutosafiri nje ya nchi, awe rais asiyeomba msaada nje ya nchi, asiyekopa, hakutakuwa na rushwa, mahosipitali yote yatajaa dawa na vifaa, shule zitakuwa na madawati bila kuchangisha wafanyabiashara na wananchi, hakutakuwa na wakwepa kodi, machinga hawatalipa kodi na watafanyia umachinga popote wanapotaka hata kama ni katikati ya barabara na airport, kariakoo igeuke taipei, mfumuko wa bei soko la dunia hautaikumba nchi yetu nzuri, madini tutachimba wenyewe bila kutegemea nchi au makampuni ya kilaghai, vijana tutakua huru kuandamana kufurahia au kulaani jambo bila kuhitaji polisi. Polisi na majeshi yatakuwa katika hali nzuri, mabomuu hayatalipuka hata kwa bahati mbaya/ajali, umeme utawafikia watu wote ndani ya miaka mitano nk.

Ushindwe na Ulegeee. Ebbo!

Hiyo ni ndoto ya mchana kweupeeeeeeeeeee.

Huyo tena ni fisadi namba moja. Ataanza kazi ya kuwanyanganya watu wake zao kwa kutumia nguvu atayopewa ya urais.
 
Yuko anasubiri huruma, kulia kwake hakutusaidii la msingi a-adress issue zinazodaiwa kumshinda!
 
....baada ya kuongea pumba za jana ..tuko hapa airport ..tunaona JK Anaondoka kwenda nje ya nchi ...anaagana na viongozi wote wakuu pale...sijui kwa nini safari hii kimya kimya......

Mtasema sana lakini Uzi ni ule ule.Msituletee balaa la Vita nchini kwetu nyie wapenda shari.
 
Hivi kila anaepita Dar aiport anaenda nje ya Bongo?

Mzee protocal ya rais wa Tanzania anapoenda nje ya nchi ..huwa anasindikizwa na waziri mkuu na makamu...[kama wapo mjini] au na viongozi wa ulinzi na usalama ....ukiona kati ya hao yupo kumuaga basi ujuwe mkuu anaenda nje.....kama anaenda mikoani huwa yeye na walinzi wake tu!!..hope umeelewa mambo yanavyokuwa....

MARA ZOTE akisafiri idara ya mawasiliano IKULU hutoa taarifa ya vyombo vya habari ...kipindi hiki kimya...sijui anaogopa nini?? anafikiri waandamanaji wakijua hayupo wataenda kukalia IKULU?? AU anaogopa wafanyakazi na wanajeshi ambao mishahara inasuasua ..wataziba anga asirudi........mwaka huu kazi ipo.

Hata kama ni kutibiwa idara ya mawasiliano na daktari wake huwajibika kutoa taarifa.....hivi huyu ataweza kukaa nje miezi mitatu kwa matibabu kama mkapa alivyokaa SWITZERLAND na nchi ikawa inaenda?????....mkapa hakuwa na wasiwasi kwa kuwa hazina yake ilikuwa na pesa za kutosha kuendesha nchi hata kwa miezi 10 bila kutetereka.....sasa hivi kila kitu mpaka kungoja kodi ya ikusanywe ...hakuna akiba!!
 
Ushindwe na Ulegeee. Ebbo!

Hiyo ni ndoto ya mchana kweupeeeeeeeeeee.

Huyo tena ni fisadi namba moja. Ataanza kazi ya kuwanyanganya watu wake zao kwa kutumia nguvu atayopewa ya urais.

kama babu yako alivyomnyanganya babu seya demu wake..
 
Hivi kwenye houba hamkuona halivyokuwa dhaifu? Jamaa anaenda kukarabati afya
 
kazi ipo kama anapenda kuishi nchi za watu si aondoke na familia yake nani anamtaka,kazi kudandia tu shughuli za mawaziri kwani hakuna waziri husika yaani kwa kupenda kupanda ndege
 
cha kushangaza nini wakubwa? Alisema asipopaa tutakufa kwa njaa. C mnajua mungu anakaa juu? Na mkumbuke ameacha wasaidizi. Najua akirudi tu atakuwa na kontena la majenereta, kwani jana kumbe wengi aliwakatia umeme kisha akahutumibia, nilistukia kwenye manuezi pepa! Kumbe mkulu alimwaga hisia zake kwa woga!
 
Mtasema sana lakini Uzi ni ule ule.Msituletee balaa la Vita nchini kwetu nyie wapenda shari.

...hasidi hakosi sababu...mara dini ..mara damu kumwagika..., wananchi hawadanganyiki tunataka aongelee chanzo sio matokeo...! alah!!

hayo maandamano yameenda hadi butiama...zaidi ya wale watu waliokufa kwa uzembe wa polisi Arusha....maandamano ya amani yaliyofuatia ...hakuna hata mtu aliyesukumwa ..sembuse kutoka damu?
 
Isije ikawa ndio anatoroka hivyo baada ya nchi kumshinda. Nimeambiwa anaenda Ufaransa, sijui kufanya nini. Hata wasaidizi wake anaosafiri nao nasikia wanalalamika safari zimezidi. Ila kuna taarifa kwamba jamaa alianguka tena hivi karibuni na alizimia kwa muda mrefu. Waliokuwa karibu naye wanasema walihofia huenda alikuwa amezimika moja kwa moja. Labda anaenda kushughulikia masuala ya afya yake.
 
kazi ipo kama anapenda kuishi nchi za watu si aondoke na familia yake nani anamtaka,kazi kudandia tu shughuli za mawaziri kwani hakuna waziri husika yaani kwa kupenda kupanda ndege

kweli amepaa juu, lakini atatua tena bongo mda si mrefu, walikubaliana kuendelea na usuluhishi wa ivory coast 3days baada kile kikao cha juzi, so ndo keshago, vile aenda meet na maprezda wenzake kunyorosha mambo pande ile, zen atakam hom kumalizana na mbowe/slaa, mambo yakienda kama alivyoagiza awakute korokoroni waking'ang'ania maandamano yao, na kesi ya arusha wafutiwe dhamana inji hii itawalike! Kama umenisoma gonga tano, teh teh!
 
Anaenda wapi? Tuwekee taarifa kamili hapa,isije kuwa kaamua kwenda kwao msoga kwa ndege halafu wewe unasema anaenda nje ya nchi!
 
kasoma alama za nyakati, harudi tena

mkuu vp tena,ID yako ni jina la rais wangu tunavomuita hapa jamvini kulikoni umelibeba? Najua madokta wengi ila apa naona umenpa utata,anyway tuyaache ayo. Nami nko apa Quality Plaza nimemwona Msafiri dr dr dr jk anapelekwa uwanja wa ndege,na magari yamerudi baada ya dakika chache alipopanda pipa. Uyo ndo mkwere a.k.a traveller.
 
Hivi kila anaepita Dar aiport anaenda nje ya Bongo?

Ajabu sana!! Hata miye niliposoma tu hii, haikuingia akilini kwamba akipita airport tu anakwenda majuu?? Vipi kama anakwenda Mtwara au Bukoba? Hawa eti ndiyo great thinkers wetu!! Mnatia aibu sana. Hata comments zenyewe ukisoma ni mipasho na umbea tu, hakuna mantiki yoyote.
 
Back
Top Bottom