JK aongoza kikao cha Kamati kuu ya NEC CCM leo. Ubunge Igunga kujadiliwa

Nape yu karibu kuumbuka...shikeni maneno yangu
Ni kweli Mkuu maana anamwaminisha mwenyekiti wake kuwa mambo yanaenda vizuri kwa kujibu kila kitu cha CDM kumbe siyo hivyo, anakimaliza chama na hii inanikumbusha vita ya Tanzania dhidi ya Uganda 1978, kamanda mmoja wa Idd Amini Maliyamungu kama nakumbuka vizuri alikuwa anampa taarifa Amini kihivyo kuwa mambo yanaenda vizuri kumbe la, ndiyo yanayotokea kwasasa kwa CCM.
 
Hakuna jambo jipya lolote zaidi ya kuja kuambiwa matamko ya kawaida kabisa ya kuunga mkono na kupongezana tu, na haya yanaweza kuwa ni baadhi ya maadhimio;

1/Tutakata rufaa hukumu iliyotengua ubunge wa Dr. Dalali Kafumu .

2/Tunaunga mkono suala la sensa ya watu na makazi kwa kuwa ni muhimu katika maendeleo ya taifa letu.

3/Tunaunga mkono juhudi za majadiliano kati ya Tanzania na Malawi kuhusu mpaka wa ziwa nyasa.

4/Tunapongeza hatua za wabunge kupitisha bajeti na kuunda kamati ya kuchunguza kashfa ya rushwa.

5/Tunapongeza hatua iliyofikiwa katika mchakato uliofikiwa wa kuundwa katiba mpya.
 
Mtachonga sana gwandaz, ikulu mtaiona kwenye picha na mialiko ya chai. Mikutano itafanyika sana tu hapo. Kwani mlikua hamjui hiyo HQ ya ccm na itabaki kua hivyo milele?
 
Hili la Spika wa Bunge kuwa mjumbe kwenye kamati ya chama inaleta walakini kwenye utendaji. Ukizingatia kuwa Bunge linaundwa na vyama mbalimbali. Nafikiri kuna haja ya kutafuta namna ya kuchagua Spika wa Bunge kuondokana na maslahi binafsi kwenye chama na uongozaji wa vikao vya Bunge.
 
View attachment 62769View attachment 62769

Hili ni gazeti la leo la Ijumaa na habari inadokeza hivi:

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete amemuita ikulu mwanamuziki anayefanya vizuri kwa sasa kwenye Bongo Fleva, Nasibu Abdul Jumaa ‘Diamond Platnumz’ na kumpa jukumu maalum, Ijumaa linairusha hewani.

Kwa mujibu wa Diamond, juzikati ‘prezidenti’ alimwita ikulu Magogoni, Dar es Salaam na kumpa shavu la kwenda kufanya shoo kwenye mkutano maalum utakaofanyika Washington DC nchini Marekani hivi karibuni.

“Yaa, rais aliniita akaniambia kuna shoo natakiwa kwenda kufanya Marekani

Labda anataka kumpa Wilaya ya Serengeti
 
watakuwa wanajadili ishu ya sensa na kashkash zake za baadhi ya watu na taasisi kutaka kususia

hapo serikali na CCM wamekamatika ipasavyo.
 
Mile tu sisi tutaendelea kukutana ikulu na Kamwe hamtaingia huko . Mtakuwa mnaiona ikulu kwenye luninga. Kuhusu igunga tumeelewa kuwa yule jajji ni mwanachama wa movement for Chaga M4c katika Hali hiyo ungetegemea hukumu ya namna gani.
 
nauliza tu wajamini
ikulu ni ya CCM au ni ya watanzania wote?
kama jibu ni ndio kwanini afanye mkutano mkuu wa CCM ndani ya Ikulu?
CCM si wana ofisi zao lumumba au dodoma?
 
View attachment 62769View attachment 62769

Hili ni gazeti la leo la Ijumaa na habari inadokeza hivi:

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete amemuita ikulu mwanamuziki anayefanya vizuri kwa sasa kwenye Bongo Fleva, Nasibu Abdul Jumaa ‘Diamond Platnumz' na kumpa jukumu maalum, Ijumaa linairusha hewani.

Kwa mujibu wa Diamond, juzikati ‘prezidenti' alimwita ikulu Magogoni, Dar es Salaam na kumpa shavu la kwenda kufanya shoo kwenye mkutano maalum utakaofanyika Washington DC nchini Marekani hivi karibuni.

"Yaa, rais aliniita akaniambia kuna shoo natakiwa kwenda kufanya Marekani

Kama hii ni kweli, this is TOO LOW kwa PREZIDAA kumwalika Diamond just kumuomba kwenda kutoa shoo eti kuzindua tawi DMV. Diamond kama watanzania wengine anaweza kutembelea ikulu, lakini sababu ya invitation hiyo haiendani kabisa na hadhi ya presidential responsibilities. Anyway, huyu ndiye Rais wetu na priorities azionazo.
 
Jamani hicho kikao kitapunguza bei ya umeme,vyakula,mafuta na mengineyo so saa mbili leteni habari za hicho kikao kama ww ni mhusika

Wakuu,
Mie na mashaka kama mnimkulu (Afisa Mkuu wa Itifaki) huwa anaipeleke CCM hati ya madai (bill) kwa kutumia
  • umeme
  • mapochopocho
  • ukumbi
  • wahudumu
  • n.k
Sababu kikao hiki ni cha ki-chama zaidi na siyo masuala ya kiserikali. Anyway hii nayo tutaipeleka Mahakamani, Msajili wa Vyama na Tume ya Uchanguzi juu ya CCM kutumia vibaya ofis za umma hususan kwa ajili ya kukatia rufaa ubunge waliopoteza na mikakati ya uchaguzi.

Hali hii inaonesha kuwa bado mentaliti ya 'Chama- Kushika- Hatamu' kama vile hakuna vyama vingi. Je vyama vingine vikiomba kutumia ukumbi wa Ikulu kwa masuala kisiasa vitapewa hiyo nafasi na Mnimkulu?
 
Kuna jamaa humu jf aliwahisema kwamba rais wetu kazi anayoweza kufanya kwa ufanisi ni usanii. Sasa kama anataka kumpromote diamond kwa kumpatia fursa ya kupiga show kwa nini nisiamini maneno ya jamaa!
 
Kwa mara nyingine tena naomba niseme kitendo cha Spika wa bunge kuwa mjumbe wa CC ya CCM kinatia doa kiti cha Spika. Kuwa mjumbe wa NEC ni sawa lakini sio CC. Bunge limeharibika kabisa, kageuza bunge kuwa idara ya serikali na sasa bunge linanuka rushwa kama ilivyo serikalini.

Hili la Spika wa Bunge kuwa mjumbe kwenye kamati ya chama inaleta walakini kwenye utendaji. Ukizingatia kuwa Bunge linaundwa na vyama mbalimbali. Nafikiri kuna haja ya kutafuta namna ya kuchagua Spika wa Bunge kuondokana na maslahi binafsi kwenye chama na uongozaji wa vikao vya Bunge.

Kwani chama gani hakimjumuishi spika kuwa mjumbe wa kamati kuu? Soma katiba ya Chadema sura ya saba 7.7.14 (r).
 
Kwani chama gani hakimjumuishi spika kuwa mjumbe wa kamati kuu? Soma katiba ya Chadema sura ya saba 7.7.14 (r).
Kama umesoma vizuri comment yangu sijaspecify chama chochote. Ndio maana nikasema kuna haja ya kutafuta njia nzuri ya kupata spika ambaye hayupo ndani ujumbe wa chama chake.
 
Back
Top Bottom