Zak Malang
JF-Expert Member
- Dec 30, 2008
- 5,404
- 233
Ukifuatiliua vizuri historia ya Thailand utaona kuwa hali iliyofikiwa sasa hivi inatokana na uminywaji wa haki wa muda mrefu uliofanywa na watawala mbali mbali, hali ya rushwa kubwa (grand corruption) iliyoshamiri kutokana na vyombo husika kuchukua hatua stahili.
Hali hii imeleta tofauti kubwa ya maisha kati ya 'walionacho' na 'wasionacho', huku 'walionacho' ndiyo wameendelea kushika dola kwa kutumia wakala (aka vibaraka) wao waliowaweka madarakani.
Kinachoendelea sasa hivi ni upande wa 'wasionacho' kuona 'sasa imetosha' kwani kujikomboa kwa njia za halali za kidemokrasia imekuwa vigumu kutokana na ukweli kwamba dempokrasia hiyo imekuwa ni uharamia tu kwani hufanyika katika mazingira ya rushwa kubwa kutoka kwa wachache 'walionacho' hivyo kujinyakulia ushindi kila mara.
Mazingira haya ya demokrasia ndiyo yanaonekana hapa Tz ingawa pengine itachukua muda mrefu hadi nchi kupata 'Red Shirts' wake. Nina hakika kuna baadhi katika utawala wa CCm wanaelewa hivyo ingawa wengi bado hawaoni mbali -- wanaona mwisho wa pua zao tu.
Ninachojiuliza ni kwamba hivi utawala wa JK, na hasa JK mwenyewe anawaonaje wale Red Shirts? Anawaona ni kundi dogo tu la wahuni ambali haliwawakilkishi watu wowote?