"JK anaona matatizo halafu anakaa kimya, wapinzani wakisema mnasema wanapiga kelele" by Kinana

Si walisema umaarufu wa JK utaongezeka 2012?
Nadhani umeshaanza kuongezeka, hauoni sasa hivi wagonjwa wanavyoteseka kwenye mawodi, kwa nini hapo asifahamike kwa kutojali wananchi wake kinyume chake anajali kutalii.
 
Maneno ya Kinana mwenyewe kama ilivyoripotiwa na Mwananchi, 31/01/2012

"’Nitamwambia Rais kuwa wananchi wanakubaliana na utendaji wako ila uongeze ukali...Hili suala la kuonea aibu la chama cha CCM ndilo linalosababisha wapinzani wapate nguvu, haiwezekani Kiongozi wa CCM anaona matatizo halafu anakaa kimya, wapinzani wakisema mnasema wanapiga kelele”.

Huyu msomali ana akili nyingi sana miongoni mwa viongozi wa ccm
 
Hivi kwanini jamaaa hakipewa hata ka ubunge ka kuteuliwa wakati walifanya kazi ngumu sana ya ukampeni manager? Au alikuwa ni chaguo la ccm si la JK wakati wa uchaguzi? Ila jamaa anajua kupiga propaganda ambazo kidogo zinaakili ukilinganisha na wengine huko maga,bani!
 
Zitto pesa anazopokea kutoka kwa wafadhili wake zinamtosha, Makamba ile mihela aliyochukuw Nasdaq USA inamtosha sana, Kigwangwala ni muhongo na mnafki, na ni member humu JF natafuta post zake humu JF alizokuwa anapigia upatu miposho, alichofanya Kigwangala ni kucheza na akili za Watanzania kupata Political credilbity, kwani alijuwa wazi kwamba posho ni lazima zipande, kwahiyo alitaka kuonesha yupo upande wa Wananchi. huyu ni mnafki.

Mkuu una akili kama ya huyu Msomali kinana .Maneno ya mpuuzi mmoja unayaleta hapa ? Zitto anapokea pesa za wafadhili kama ni kweli kuna ubaya gani kupokea kuliko kuwakamaua wananchi? Kwa hiyo kwa utetezi wako huu unasema posho ni sawa ? Kweli nawe ni thinker karibu tupo hapa .
 
He is a soldier and as an officer, has assessed the field performance and come up with facts! He knowd the danger of operating in vacuum!
 
Hivi kwanini jamaaa hakipewa hata ka ubunge ka kuteuliwa wakati walifanya kazi ngumu sana ya ukampeni manager? Au alikuwa ni chaguo la ccm si la JK wakati wa uchaguzi? Ila jamaa anajua kupiga propaganda ambazo kidogo zinaakili ukilinganisha na wengine huko maga,bani!

Jk alitaka awe speaker kumrithi sitta akakataa badae jk akataka awe katibu mkuu wa ccm kumrithi makamba pia akakataa,jamaa ni mtu wa ukweli anajua jk hana msimamo ukifanya nae kazi atakuyumbisha utaonekana kiongozi mbovu ndio maana kaamua kujiweka pembeni na kubaki tu kuwa mjumbe wa kamati kuu ambako huwa anawapasha ukweli ccm wapi wanapokosea na kwanini wamefika hapo,lakini huwa anawaambia ni uamuzi wao kuchukua ama kutochukua ushauri wake,mfano issue ya kutowashirikisha kina lowassa kwenye serikali ni yeye ndie aliyemshauri kikwete hata ile ya kikwete kwenda igunga na monduli kuwashika mikono jamaa wakati wa kampeni 2010 aliipinga na kumwambia jk waziwazi kwamba hakukua na ulazima kwa yeye kwenda huko kama ilikua lazima basi angeenda hata Dr Bilali mgombea mwenza,tatizo la jk ni ukaidi.
 
Kulikuwa na sababu yoyote ya kusema maneno haya "huyu msomali"

Au ubaguzi umekukaa akilini zaidi ya ubinadamu..binadamu wote ni sawa mkuu
mimi ndio huwa ninavyomwita hata yeye mwenyewe anajua hivyo mzee,but kama nimekukwaza niwie radhi.all in all jamaa kichwa.
 
Zitto pesa anazopokea kutoka kwa wafadhili wake zinamtosha, Makamba ile mihela aliyochukuw Nasdaq USA inamtosha sana, Kigwangwala ni muhongo na mnafki, na ni member humu JF natafuta post zake humu JF alizokuwa anapigia upatu miposho, alichofanya Kigwangala ni kucheza na akili za Watanzania kupata Political credilbity, kwani alijuwa wazi kwamba posho ni lazima zipande, kwahiyo alitaka kuonesha yupo upande wa Wananchi. huyu ni mnafki.

Suala hili la kuchukua hela Nasdaq ili akazitumie kutekeleza mpango wake wa Bumbuli ya Jana, Leo, Na Kesho, nilidhania ni utani, pamoja na kuambia na mwanamke mmoja mtu wa karibu sana na January, kwani haikuniingia akilini jinsi atakavyoweza zirudisha. Kwahiyo hii ni kweli? Je una taarifa kamili ya mchakato wake wote huu wa Nasdaq umekaa vipi?
 
Jk alitaka awe speaker kumrithi sitta akakataa badae jk akataka awe katibu mkuu wa ccm kumrithi makamba pia akakataa,jamaa ni mtu wa ukweli anajua jk hana msimamo ukifanya nae kazi atakuyumbisha utaonekana kiongozi mbovu ndio maana kaamua kujiweka pembeni na kubaki tu kuwa mjumbe wa kamati kuu ambako huwa anawapasha ukweli ccm wapi wanapokosea na kwanini wamefika hapo,lakini huwa anawaambia ni uamuzi wao kuchukua ama kutochukua ushauri wake,mfano issue ya kutowashirikisha kina lowassa kwenye serikali ni yeye ndie aliyemshauri kikwete hata ile ya kikwete kwenda igunga na monduli kuwashika mikono jamaa wakati wa kampeni 2010 aliipinga na kumwambia jk waziwazi kwamba hakukua na ulazima kwa yeye kwenda huko kama ilikua lazima basi angeenda hata Dr Bilali mgombea mwenza,tatizo la jk ni ukaidi.

Pamoja na kuwa kichwa, ana madudu mengi sana ambayo akiingia tu kwenye siasa yatamwagwa hadharani. Vinginevyo anayapenda sana madaraka kama wengine tu. Utakubalije kuwa spika wa bunge la afrika mashariki lakini ukatae kuwa spika wa bunge la jamhuri kwa sababu za ovyo ovyo tu? Hes very sharp, siasa za CCM level yake ni chini sana ya Kinana kiasi kwamba atavurugana nao na watatoboa siri ya mambo yake mengi tu ya ovyo ovyo, ya tangia akiwa waziri wa ulinzi chini ya Mwinyi.
 
jambo la kwanza lazima ujue kwamba siasa za tanzania hasa ccm zinaendeshwa kwa style ya remote control na genge la lowassa ambalo jamaa siku zote hakubaliani nalo wakati mwenyekiti anaonekana kuwa nalo sambamba kiaina,ndio maana mwenyewe anasema wazi hataki kugombana na watu kwa kuwa yeye ni mtu wa principle akiingia inabidi mambo yaende kwa misingi inayoeleweka jambo ambalo anajua kina lowassa hawatalipenda na kwa kuwa wana ushawishi kwa jk basi yeye atakua anaonekana kituko na kudhalilishwa tu kama kina kina mzee msekwa na mukama au spika wa sasa,ndio maana kaamua kujiweka pembeni,lakini hana uchafu huo unaodhani,sema yeye ni mfanyabiashara na alivyo mbowe,kama rafu zipo ni za kawaida kibiashara sio za kuathiri uchumi wa nchi hii kama ma richmond yenu haya pamoja na ma EPA.Kipindi cha mwinyi kashfa kubwa labda eti sio raia.
 
mmhhh...meneja kampeni wa JK anaweza kuthubutu kusema maneno hayo kweli? isije mwananchi wakaandika tena "KUMRADHI KINANA" kwamba walimnukuu vibaya....
 
Tatizo watu wengi wanapenda utukufu wa kisiasa lakini kusema kweli wanasiasa wengi uwezo wao wa kufikiri ni mdogo sana yaani ukomo wa kufikiri (thinking capacity) umeishia kwa homo habilis, bado hawajafikia homo sapien. Kufumba macho ukitembea uchi sio solution.
 
Mkuu una akili kama ya huyu Msomali kinana .Maneno ya mpuuzi mmoja unayaleta hapa ? Zitto anapokea pesa za wafadhili kama ni kweli kuna ubaya gani kupokea kuliko kuwakamaua wananchi? Kwa hiyo kwa utetezi wako huu unasema posho ni sawa ? Kweli nawe ni thinker karibu tupo hapa .
Pumba Express!!
 
Wagonjwa wanateseka kwa madaktari uchwara kugoma.
Pamoja na mapenzi yako makubwa kwa ccm, huoni kuwa hizi tungo zako zinazidi kuongeza chuki zaidi kwa chama chako?
Je, unathibitisha kuwa mambo yapokwenda mrama kila ufanyacho hata kwa juhudi za kuokoa, matokeo yake yanazidi kuharibu zaidi?
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom