JK anaharibu hadhi ya elimu kwa kujiita Dr. wakati siyo, pamoja na wanasiasa wengine

Tuanzishe utaratibu au hata Sheria kuwa mtu ataitwa Dr pale tu atakapokuwa na elimu ya PhD au Dr.as in law etc au Udaktari wa binadamu,meno au wanyama.Nje ya hapo isiruhusiwe kwa yeyote kutumia title ya Dr. hata kama amepewa hizo Honoris Causa.Vinginevyo hadhi ya hii title itachuja na haitakuwa na maana tena kusotea darasani.Imagine Dr Augustine Lyatonga Mrema!

Too late dear, waliotunga hiki cheo, ndio waliopanga matumizi yake, sidhani kama utaitwa kwenye jopo la kupanga matumizi ya hiki cheo.
JK hajiiti Dr, ila ni watu wanaothamini mchango wake na ambao wanapenda kukumbusha wengine kuwa mchango ule una thamani,
pia ili kukupa myo na wewe utoe mchango wa kujenga ili dunia ikukumbuke.
Katika mambo ambayo tumsifie Huyu babu, ni kuwa mwanadiplomasia.
Kipaji anacho ila tulidhani utaalamu huo utaisaidia Tanzania.
Naombeni tusimkatishe tamaa sana JK, kumtwika udaifu wote kuwa ndio YEYE KWA UJUMLA.
Tusiache kuziona strengths zake ambazo pia zipo tu nyingi.

Ila tu URAIS wa nchi kama Tanzania haumfai (maoni yangu)
 
Honoris causa zinauzwa, halali kabisa duniani kote, dole 5000 tu.
lakini wao ni watu wakubwa, wakiendelea kutamani kuitwa madokta ni kujidharau na kuchekesha kutamani ya walioko bado chini, watake nini tena kuitwa rais mstaafu kama JK au Amani kalume?
 
Back
Top Bottom