Elections 2010 JK anagawa pesa wakati wa kampeni!

Mwanamayu

JF-Expert Member
May 7, 2010
11,349
6,476
Hivi NEC na Tendwa mko wapi? JK amekuwa anagawa pesa huko Tunduma kwa wapiga kura kwa kisingizio cha kusaidia walemavu, je huku sio kununua kura za hao walemavu? Sheria ya gharama za uchaguzi inasemaje kuhusu ili? (Source: Raia Mwema, 8 - 14 Septemba, uk. 6 picha).
 
Mkuu ukizungumza NEC unazungumza Kikwete.....

Ili mambo yaende Tanzania Tunahitaji mabadiliko ya kikatiba!!
 
Wanadai anatoa misaada!! Huku akitumia ule mfumo wake wa "Kubali kuliwa kidogo ili nawewe ule saaaana".
 
TAKUKURU mpo au? kweli mbio za sakafuni uishia ukingoni mbwembwe kibao wakati wa kura za maoni leo muajiri wenu JK ameanza kuchakachua na kuikanyaga sheria ya gharama za uchaguzi mpo kimyaa kama mmelala vile. Si TENDWA wala TAKUKURU wote WAMESHIKWA NA UPOFU NA UKIZIWI kulinda ajira unaweza ukatoa mke au mume sadaka ili ajira iwepo. TAKUKURU WEeeeeeeeeeeeeeeeeeeee AMKA kumekucha mkubwa kaanza kuchakachua
 
Kumfunga paka kengele, tangu lini ikawezekana?...Hamkuona jinsi Tendwa alivyojikanyaga?
 
Sheria si alisaini yeye sasa hana haja ya kuifuata hivyo hakuna wa kumsumbua ndio maana unaona kila kitu kibaya hata iweze kitapita tu.
 
Mkiona shina la UHARIBIFU limesimama PATAKATIFU ndipo mjue ule mwisho umekuja
 
Akamatwe na kufunguliwa mashitaka yule mzee wa mufindi Mungai ,alihonga elfu Kumi tuu kesi yake iko mahakamani sasa hizo KIKWETE alizozigawa kote alikopita si ni zaidi ya zile za Mwakalebela (100,000) Jino kwa JIno Akamatwe apelekwe mahakamani period.
 
Hivi NEC na Tendwa mko wapi? JK amekuwa anagawa pesa huko Tunduma kwa wapiga kura kwa kisingizio cha kusaidia walemavu, je huku sio kununua kura za hao walemavu? Sheria ya gharama za uchaguzi inasemaje kuhusu ili? (Source: Raia Mwema, 8 - 14 Septemba, uk. 6 picha).

mwanamayu na raia mwema tunataka ushaidi na longolongo za magazeti upo apo vyombo vya dola aviwezi kufanya kazi kwa kufuata gazeti limeandka nini!we need evidence to take action!
 
mwanamayu na raia mwema tunataka ushaidi na longolongo za magazeti upo apo vyombo vya dola aviwezi kufanya kazi kwa kufuata gazeti limeandka nini!we need evidence to take action!
Mind your kiswahili! ushaidi, apo, aviwezi! Ni kwamba urudi darasani kwanza ndipo utaweza kufuzu lugha ya kiswahili na pia kujua uozo wa CCM!
 
Back
Top Bottom