Rais Kikwete amteua Zitto kamati ya Madini

Kikwete amteua Zitto kwenye kamati ya mikataba ya madini

*Itaongozwa na Jaji Mark Bomani,

* Pia wamo Cheyo, Mwakyembe
* Yapewa miezi mitatu kumaliza kazi
* Zitto asema atafanya kazi kwa maslahi nchi
Na Tausi Mbowe

RAIS Jakaya Kikwete amemteua Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe kuwa miongoni mwa wajumbe wa Kamati ya uangaliaji upya mikataba ya uchimbaji wa madini nchini.
Kamati hiyo yenye jumla ya wajumbe kumi na mmoja itakuwa chini ya uenyekiti wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mstaafu, Jaji Mark Bomani.

Wengine katika Kamati hiyo ni Mbunge wa Bariadi Mashariki (UDP), John Cheyo, Mwanasheria wa Wizara ya Nishati na Madini, Salome Makange, Kamishina wa Sera Wizara ya Fedha, Mugisha Kamugisha, Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Makazi Wizara ya Ardhi, Edward Kihundwa na Mbunge wa Kyela (CCM), Dk. Harrison Mwakyembe.

Wajumbe wengine ni Mbunge wa Msalala (CCM),Ezekiel Maige, Peter Machunde kutoka Soko la Hisa, Dar es Salaam (DSE), Mkaguzi wa Mahesabu kutoka Kampuni ya Kimataifa ya Ukaguzi wa Mahesabu, PriceWater Coopers, David Tarimo ambaye ni mtaalam wa masuala ya kodi na Mkurugenzi wa Madai na Sheria za Kimataifa, Wizara ya Katiba na Sheria, Maria Kejo.

Taarifa ya Ikulu iliyosainiwa na Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo ilisema kuwa pamoja na mambo mengine, kamati hiyo pia itakuwa na kazi ya kuchambua mfumo wa kodi unaotumika katika sekta ya madini na kupitia mfumo wa usimamizi wa shughuli za uchimbaji mkubwa unaofanywa na serikali. Kamati hiyo iliyopewa kipindi cha miezi mitatu kukamilisha kazi yake pia inajukumu la kukutana na taasisi zinazosimamia madini na wadau wengine na kutakiwa kutoa taarifa yenye mapendekezo.

Pia Kamati hiyo itakuwa na jukumu la kupitia mikataba ya madini na nyaraka nyingine zitakazohusu migodi ya mikubwa nchini. Kuundwa kwa Kamati hiyo kunafuatia hoja binafsi ya Zitto Kabwe aliyoitoa bungeni kutaka kuundwa kwa Kamati Teule yakuchunguza mazingira ya kusainiwa kwa mkataba wa mgodi wa dhahabu wa Buzwagi huko Uingereza na Waziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi Februari mwaka huu. Baada ya kuwasilisha hoja hiyo, Kabwe alifungiwa kuhudhuria vikao vya Bunge hadi hapo Januari mwakani. Hatua hiyo ya Bunge iliibua mjadala mkubwa miongoni mwa makundi mbalimbali wakihoji sababu za kumfungia mbunge huyo kijana.

Hivi karibuni wakati Rais Kikwete akihutubia Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi katika Ukumbi wa Kizota , mjini Dodoma aliahidi kuunda kamati hiyo itakayojumuisha wadau mbalimbali kwa ajili ya kuangalia mikataba mipya ya madini. Akizungumza na Mwananchi kuhusiana na uteuzi huo, Zitto Kabwe alisema kwamba amepokea uteuzi huo wa Rais Kikwete na atafanya kazi kwa maslahi ya Watanzania.

"Nimepokea kwa mikono miwili uteuzi, naahidi kufanya kwa umakini wa hali ya juu," alisema alisema Zitto na kuongeza kwamba uamuzi wa Rais unaonyesha jinsi alivyokomaa kidemokrasia tofauti na wabunge 274 wa Chama cha painduzi (CCM )walioko bungeni.
 
hapa ndio itabidi Zitto awe makini kabla ya kukubali huu uteuzi na ajue kabisa powerz zote za hii kamati na kile ambacho itafanya kabla ya kuingia mkenge
 
kauli ya zito kuwatusi wabunge inaweza kumfanya achukuliwe hatua zaidi..'RAIS KIKWETE AMEONESHA KUKOMAA KIDEMOKRASIA ZAIDI YA WABUNGE WA CCM 274` ..kwa mujibu wa vifungu vya bunge,Mbunge anakatazwa kusema maneno ya uzushi,au yanayoweza kushusha heshima ya mbunge mwingine ktk jamii..
 
"Nimepokea kwa mikono miwili uteuzi, naahidi kufanya kwa umakini wa hali ya juu," alisema alisema Zitto na kuongeza kwamba uamuzi wa Rais unaonyesha jinsi alivyokomaa kidemokrasia tofauti na wabunge 274 wa Chama cha painduzi (CCM )walioko bungeni.

Zito bwana anajibu mapigo hapo kwa papo. Mimi sina wasi wasi na Zito kwa sababu, amekwisha onyesha umakini wake hadi hapa alipofika, huzuni yangu ni pesa ya walipa kodi jinsi inavyochezewa kama vile haina mwenyewe........Wenyewe wapo wabongo na hawa viongozi wamesinzia usingizi wa pono wanawakumbatia mafisadi katika kuimaliza.
 
kauli ya zito kuwatusi wabunge inaweza kumfanya achukuliwe hatua zaidi..'RAIS KIKWETE AMEONESHA KUKOMAA KIDEMOKRASIA ZAIDI YA WABUNGE WA CCM 274` ..kwa mujibu wa vifungu vya bunge,Mbunge anakatazwa kusema maneno ya uzushi,au yanayoweza kushusha heshima ya mbunge mwingine ktk jamii..
Sio tusi, kwani alichofanya Rais ndicho kilichomfanya Zito aitwe muongo na wabunge hao hao 274, kama unabisha kuwa hawa jamaa hawajakomaa soma tena bajeti ya serikali ya mwaka 2007/2008, halafu ujiulize ni nani aliipitisha!
 
Mwakyembe ni lazima ajitoe mojawapo ya hizo Kamati ili ziwe huru! Tunataka tuone kama Kamati mbili huru na zisizoingiliana zinapoangalia ushahidi ule ule zitaweza kufikia suluhisho moja?
 
The more akifungiwa, the more anapata umaarufu. sidhani kama wanaweza kumfungia tena. they've got a lesson
 
Zito bwana anajibu mapigo hapo kwa papo. Mimi sina wasi wasi na Zito kwa sababu, amekwisha onyesha umakini wake hadi hapa alipofika, huzuni yangu ni pesa ya walipa kodi jinsi inavyochezewa kama vile haina mwenyewe........Wenyewe wapo wabongo na hawa viongozi wamesinzia usingizi wa pono wanawakumbatia mafisadi katika kuimaliza.

Mkuu Dua.

Kikwete anatapatapa right now. Aliwekwa ikulu na wezi na mafisadi. Mtoto wake anafanya kazi kampuni ya IMMA inayotetea na kulipwa pesa za mafisadi every other day! Kina Karamagi bado wanapeta tu wizarani, na leo anaunda kamati ya kina cheyo, bomani na mwakyembe?

Tanzania kweli ina pesa zaidi za kuharibu na Kikwete is the right guy kwa kufuja pesa za wabongo.
 
napendekeza mheshimiwa ZITTO ajitoe kwenye hiyo kamati ilikulinda heshima yake na upinzani kwa ujumla.kwenye hiyo kamati hakuna jipya zaindi ya kummaliza zitto na upinzani kwa ujumla.
 
i) Mpaka kieleweka et al.: Si kweli kwamba Issa Shivji na Tundu Lissu ndio watu pekee wanaoijua mikataba ya madini au wenye uchungu na Tanzania. Kwa hiyo mimi kutukuwepo hawa katika kamati sioni tatizo kabisa. Tuache kasumba ya kufikiri kwamba ni watu fulani katika jamii yetu wenye uwezo wa kufanya mambo, huo na ni utegemezi! Ile nchi ina watu mil 36 wenye vipaji mbalimbali. Watu wakipewa kazi, tuwasukumu na kuwatia moyo kuhakikisha wanafanya kazi ya vizuri.
ii) Ndio nasema kila siku kuwa nchi yetu ina uhaba wa mafanikio kiasi kwamba hata likitokea jambo dogo inabidi tushangilie kama mazuzu. Ndiyo tuliweza kubagawa hata Rashid kushinda mashindano ya BBA. Sasa na hili nalo sishangai. Lakini binaafsi, at the risk of being seen cynical, sioni cha kushangilia. Yaani mafanikio hapa ni nini hasa hadi tumsifu JK? Huyu mtu kuna siku tutamsifia hata atakapoamka mapema. Kosa la mikataba mibovu walifanya wao, sasa wanapochukua hatua za kurekebisha tena kwa shinikizo, sisi tunachosifia hapa ni kitu gani hasa? Tunamsifia baba kununua nepi za mwanae? Ndio kusema siku JK atakapoamua kuwatoa akina Karamagi itabidi tufanye maandamana ya kumpongeza, tuna wazimu au nini?
 
napendekeza mheshimiwa ZITTO ajitoe kwenye hiyo kamati ilikulinda heshima yake na upinzani kwa ujumla.kwenye hiyo kamati hakuna jipya zaindi ya kummaliza zitto na upinzani kwa ujumla.

Sidhani kama hii ni busara.Litakuwa jambo la kitoto na kishule zaidi kuliko utu uzima. ALichofanya JK ni kuunda kamati yenye sura ya multipartisan ili kuhakikisha talent mbalimbali anazitumia ndani na nje ya CCM. This is good na inaonyesha kukomaa na kukubali kwamba kuna watu wenye akili hata nje ya CCM. Actually, ningemshangaa na kumzomea sana Zitto kama angekata uteuzi, it would have been counterproductive and self-defeating. Anachotakiwa kufanya Zitto ni kuhakikisha kwamba yale mapendekezo yake aliyokuwa nayo yanaingia kwenye kamati. Pale ambapo hatakubaliana na baadhi ya vipengele na ikitokea kwamba wenzake wote wameng'ang'ania hivyo, basi anapaswa kuweka dissening opinion. Baadhi ya kamati kumaliza kazi yake, ahakikishe yale waliyokubaliana yanakuwa wazi. Wasikubali utamaduni wa kijinga kwamba tumeshawasilisha mapendekezo yetu kwa Rais halafu ni yeye pekee atakayoyatoa kwa wakati anaotaka.
 
usanii mtupu katika hiyo kamati..
natoa wasifu mdogo wa watu waliochaguliwa katika kamati hiyo,kesho ntamwaga zaidi..

bwana MACHUNDE,ni mwajiriliwa wa kampuni ya karamagi inaitwa tradex Investment.wametaja soko la hisa ili kuwahadaa watz,

bwana maige si mwanasheria na hana uzoefu wowote ktk sekta ya madini,ni Rafiki mkubwa wa mh. ngeleja<naibu waziri-madini>.
bwana cheyo,toka arudushiwe nyumba yake amekuwa kada invisible wa sisiemu,
itaendelea..

Weka newz zaidi mkombozi kama unazo!
 
Sidhani kama hii ni busara.Litakuwa jambo la kitoto na kishule zaidi kuliko utu uzima. ALichofanya JK ni kuunda kamati yenye sura ya multipartisan ili kuhakikisha talent mbalimbali anazitumia ndani na nje ya CCM. This is good na inaonyesha kukomaa na kukubali kwamba kuna watu wenye akili hata nje ya CCM. Actually, ningemshangaa na kumzomea sana Zitto kama angekata uteuzi, it would have been counterproductive and self-defeating. Anachotakiwa kufanya Zitto ni kuhakikisha kwamba yale mapendekezo yake aliyokuwa nayo yanaingia kwenye kamati. Pale ambapo hatakubaliana na baadhi ya vipengele na ikitokea kwamba wenzake wote wameng'ang'ania hivyo, basi anapaswa kuweka dissening opinion. Baadhi ya kamati kumaliza kazi yake, ahakikishe yale waliyokubaliana yanakuwa wazi. Wasikubali utamaduni wa kijinga kwamba tumeshawasilisha mapendekezo yetu kwa Rais halafu ni yeye pekee atakayoyatoa kwa wakati anaotaka.

Kitila,

Heshima mkuu. Ni kweli kuwa Zitto inabidi aingie katika kamati hii na kuhakikisha kuwa mawazo yake hayabafungwi na spin master Mwakyembe!

Hata hivyo swali bado linabaki hapa! Wanaccm wengi hapa akiwemo mkuu FMES wameshasema kuwa mikataba iliyokwishasainiwa haiwezi kuvunjwa unless tunataka kuleta mambo ya IPTL!

Hii kamati utofauti wake ni nini na ile ilokuwa inapitia mikataba wakati Karamagi na Lowasa wakisaini mkataba wa Buzwagi!
 
Maswali haya nilimuuliza Mkurugenzi wa TAKUKURU na hakujibu hata mojawapo. Kwa vile tume imeundwa kuangalia Richmond, nimeonelea ni wapi maswali ambayo yatawasaidia katika kuongoza uchunguzi wao bila ya shaka na maswali mengine waliyokuwa nayo wao...

Kwanza, ilikuwaje kampuni ya hiyo ya Richmond Richmond Development (RDC) ipewe tenda hii? Majibu aliyoyatoa Bw. Hosea ni majibu ya kitoto na ya shule ya msingi. Iweje kampuni ya kupiga chapa na kuchapisha vijitabu na vielelezo ipewe tenda ya nishati? Tangu mwanzo wa suala hili kampuni hii imejivika majina ya ajabu ajabu na kutangaza uwezo wake.

Kinachoshangaza ni kuwa hakuna mtu katika serikali yetu aliyethubutu kuangalia kama kampuni hii ya RDC ina rekodi yoyote ya kushughulika na masuala ya nishati ukiondoa maelezo ya kwenye tovuti yao. Je, watendaji wetu walipitia ushahidi gani wa kazi za RDC na kuridhishwa nayo hadi kuamua kuwapa tenda ya mabilioni ya shilingi? Katika kuwapatia tenda hiyo, sheria ya manunuzi ya serikali ilizingatiwa kwa kiasi gani?

Pili, Wakati Balozi Andrew Daraja alipokwenda kutembelea Houston na kukaribishwa na viongozi wa kampuni ya Richmond Printing alioneshwa kitu gani hadi kukubali kuwa kampuni hiyo ina uwezo wa kushughulikia masuala ya nishati? Je aliona orodha gani ya nchi zilizoridhishwa na utendaji kazi wa RDC hadi kuipigia debe serikalini? Kama siyo yeye ni nani basi aliyesema kampuni hiyo ina uwezo wa kutuletea majenereta?

Tatu, kabla ya kampuni ya RDC kupewa tenda ya Nishati, ilipewa tenda nyingine ya kujenga bomba la mafuta toka Mwanza hadi Dar, bomba ambalo mradi wake ulibuniwa na kampuni ya Africommerce. RDC ilipopewa tenda hiyo kiulaini, watu wa Africommerce walilalamika kupokonywa mradi huo lakini viongozi wetu hawakujali hilo wakawapa RDC.

Miezi kumi na nane baadaye RDC walishindwa kufanya lolote na badala yake mradi huo ukapewa kampuni nyingine toka Uarabuni. Ilikuwaje kwa kampuni iliyoshindwa kuanza kutekeleza mkataba wa bomba la mafuta kwa miezi 18 kupewa mradi wa kuleta majenereta ndani ya wiki 14?

Jambo moja ni dhahiri. Mtu yule yule aliyeipigia debe kampuni hii hadi ikapewa mradi wa bomba la mafuta ndiye yule yule aliyeipigia debe na ikapewa mradi wa majenereta. Bw. Hosea yuko tayari kuwaambia na kuwathibitishia Watanzaina wenzake kuwa watu wale wale waliohusika na bomba la mafuta siyo waliohusika na mradi wa majenereta?

Nne, Kutokana na rekodi zilizoko kwenye ofisi ya Tarafa ya Harris (Harris County) kwenye jimbo la Texas, kampuni ya RDC imeorodheshwa kuanzia mwaka 2003 ikiwa ni sehemu ya kampuni mama ya Richmond Printing. Cha kushangaza ni kuwa chini ya mwaka mmoja baadaye kampuni hiyo ikapewa tenda ya bomba la mafuta nililotaja kwenye swali la tatu, na hivyo kina Elisante Muro kunyang'anywa mradi wao.

Je, Bw. Hosea na wakubwa wa Wizara ya Nishati na Madini wanaweza kuwaeleza Watanzania ilikuwaje kampuni changa namna hiyo kupewa mradi mkubwa wa nishati wakati haina historia ya biashara ya sekta husika? Je tukiwaambia kuwa hiyo ndiyo sababu ya mabenki ya Marekani kuikatalia mkopo wa fedha za awali kampuni hiyo kwa vile hawana historia ya mikopo kama kampuni ya nishati kina Hosea watakataa?

Kama Wamarekani wameona kuwa kampuni hiyo haina uwezo wa kustahili mkopo mkubwa wa fedha kiasi hicho ilikuwaje wasomi wetu na maafisa waliotajwa na Bw. Hosea wakakubali kuipa tenda? Ni nani huyo aliyeipigia debe kampuni hiyo na mtu huyo ana maslahi gani?

Tano, wakati Rais Kikwete anazungumza na wananchi mapema mwaka huu alielezea kusita kwake kukubali kampuni hiyo kupewa malipo ya aina yoyote na akawahakikishia wananchi kuwa RDC haikulipwa kwani alikuwa na mashaka nayo.

Je, TAKURU walimhoji Rais Kikwete awaelewe kwanini alisita na ni nani aliyemshawishi hadi akaacha mkataba huo kuendelea? Tukiwaambia kuwa yule aliyeipigia debe kampuni hii kwa Rais Kikwete na yule aliyehakikisha kampuni changa namna hii ilipewa tenda kuwa aidha ni mtu mmoja au wana udugu wa damu, Bw. Hosea anaweza kutuonesha kinyume chake?

Sita, inawezekana ni kweli kuwa hakukuwa na rushwa iliyolipwa moja kwa moja na ikapewa jina "rushwa" kwenye mchakato wa mkataba wa RDC. Hata hivyo hatuna budi kumuuliza Bw. Hosea kama alianza kuangalia mchakato huu kabla ya mkataba kuingiwa na umbali gani wa historia ya nyuma alienda.

Sijui kama Bw. Hosea anafahamu uhusiano wa karibu wa Bw. Msabaha na familia ya kina Gire uliodumu kwa miaka kadhaa sasa (kabla ya mikataba hii). Inapotokea kuwa rafiki wa familia anapewa mikataba miwili inayohusu sekta moja ambayo rafiki yao ndiye Waziri wa wizara hiyo hatuna budi kuhoji na kuchunguza mikataba hiyo.

Je, Bw. Hosea ameweza kumhoji Bw. Msabaha chini ya kiapo na kuhakikishiwa hakupokea yeye (au ndugu zake) kitu chochote ambacho kinakatazwa katika sheria ya manunuzi ya umma ya mwaka 2004 na sheria nyingine?

Ni kwa kiasi gani urafiki wa Msabaha na kina Mohammed Gire,Naeem Gire, Zahor Gire, Abdul Gire, Imaduddin Gire, Mumtaz Gire, Adam Gire, Sharrifa Gire na ndugu zao walioko Ulaya na waliopo nyumbani ulichangia kwa wao kupewa tenda hizo?

Saba, katika maelezo yake kwa wananchi Bw. Hosea alisema wazi kuwa kutokana na dharura iliyotokea ya nishati Waziri Mkuu aliingilia kati na kuunda kamati ya watu watatu kuharakisha utatuzi wa tatizo la nishati. Swali langu kwa Bw. Hosea, je ni sheria gani inayompa madaraka Waziri Mkuu kusimamisha sheria ya ununuzi wa serikali ya 2004 na kuweza kuingilia utaratibu wa utoaji tenda?

Waziri Mkuu alipoingilia utaratibu uliowekwa wa kutoa tenda alifanya hivyo kwa mamlaka gani? Kusema kuwa ulikuwa ni "wakati wa dharura" ndio mwanzo wa kuleta maamuzi ya kiimla.

Kwa vile mtanzania mwenzetu ni Waziri Mkuu isiwe ni kisingizio cha mti huyo kupinda/kuvunja sheria kwani, ni wakati wa dharura ndipo tunataka kuona viongozi wetu wazisimamie sheria kwa umakini zaidi.

Kama kamati aliyounda Waziri Mkuu haina mamlaka ya kisheria, maamuzi yake basi pia ni batili hata kama yamefanywa kwa nia nzuri! Kwa maneno mengine, mkataba wa RDC uliingiwa kinyume na sheria na hivyo hauna nguvu ya kisheria, isipokuwa pale Bw. Hosea na wenzake watakapotuonesha utaratibu uliotumika kutoa tenda hiyo usiopingana na sheria ya Manunuzi ya Serikali ya mwaka 2004.

Nane, Bw. Mohammed Gire Afisa Mkuu Mtendaji wa RDC amekuwa akitoa michango wakati wa kampeni na bila ya shaka ndugu zake nao hufanya hivyo. Inafahamika kuwa kina Gire waliichangia CCM na kampeni yake ya uchaguzi ya mwaka 2005 (mwaka mmoja baada ya kampuni kuundwa).

Je, Bw. Hosea anaweza kuwaambia Watanzania ni kiasi gani kilipokewa toka kwa kina Gire kusaidia kampeni ya Rais Kikwete, ya Lowassa, na ya Msabaha? Tukimwambia kuwa kina Gire walichangia ya kutosha kampeni hizo wakiwa na matarajio ya kupewa mkataba wa Bomba la mafuta na kupewa mkataba mwingine wa nishati atatukatilia?

Je, michango ya namna hiyo haiwezi kuonekana kama ni rushwa? Kama CCM watapinga kuwa hawakupokea michango toka kina Gire, wako tayari kutoa orodha ya wachangiaji wao wakubwa wa ndani na nje ya nchi? Bw. Hosea anaweza kutaka orodha hiyo akapewa?

Tisa, katika suala hili zima, jina moja limekuwa likihusishwa na kupatikana kwa mkataba huu na kupewa tenda kwa RDC. Jina hilo ni la Waziri Mkuu Mhe. Edward Lowassa (Monduli - CCM). Wakati huo huo kumekuwa na tuhuma kuwa mmojawapo wa watu waliohusika katika kuipigia debe kampuni hii ni kijana mmoja mwenye mahusiano ya damu na Waziri Mkuu.

Ni kweli kuwa kijana huyo hayupo sasa kwenye orodha ya viongozi wa kampuni hiyo (kama alivyodai mmoja wa viongozi).

Swali kwa Bw. Hosea, je wakati wowote katika mchakato wa tenda hii kuna ndugu wa kiongozi aliyekuwa na nafasi ya uongozi na baadaye akajiondoa/kuondolewa kwa sababu ya kuonekana mgongano wa maslahi? Mtu huyo ni nani na nafasi yake ni ipi? Je serikali ilipata nafasi ya kumhoji?

Kumi, tumeambiwa kuwa RDC hawakulipwa na serikali kwa sababu ya kushindwa kutimiza mkataba, hilo linawezekana kuwa ni kweli lakini ni kweli kuwa fedha za serikali hazikufikia mifuko ya kampuni hiyo? Ni nani aliuza mkataba wa RDC kwa Dowans?

Kama Richmond waliuza mkataba huo kwa kipengele walichoweka kwenye mkataba, na serikali ikailipa Dowans dola milioni zaidi ya mia moja, je RDC hawakulipwa na Dowans? Bw. Hosea anaweza kuuhakikishia umma wa Watanzania kuwa hilo la kuuza mkataba halikuwa "janja ya nyani" kwa RDC kulipwa bila ya kufanya kazi!

yeye ni kama nani ajibu hayo maswali ? hakunegotiate chochote, yeye kazi yake ni kudeal na before na aftermath ya matukio na hakuwemo katika hilo sakata !

mtafute karamagi muulize, mpigie simu uongee nae !
 
Kitila,

Heshima mkuu. Ni kweli kuwa Zitto inabidi aingie katika kamati hii na kuhakikisha kuwa mawazo yake hayabafungwi na spin master Mwakyembe!

Hata hivyo swali bado linabaki hapa! Wanaccm wengi hapa akiwemo mkuu FMES wameshasema kuwa mikataba iliyokwishasainiwa haiwezi kuvunjwa unless tunataka kuleta mambo ya IPTL!

Hii kamati utofauti wake ni nini na ile ilokuwa inapitia mikataba wakati Karamagi na Lowasa wakisaini mkataba wa Buzwagi!

Well, mimi nafikiri kazi kubwa ya hii kamati ni kutafuta ukweli juu ya mikataba yetu ya madini. Je, ni kweli kwamba mikataba ndiyo tatizo au tatizo ni usimamizi wa mapato yanayotokana na madini yetu? Kama mikataba ndiyo,tatizo basi kamati inabidi itoe mapendekezo ya radical changes. Utekelezaji wake ni wa hao tuliowakabidhi nyenzo za kufanya maamuzi.

Angalizo ambalo akina Zitto lazima waliangalie ni ukweli kwamba wale wazungu wenye makampuni ya madini watawafuata sana kuhakikisha kwamba hawapendekezi radical changes. Sasa akina Zitto wana options mbili: kuamua kuibuka matajiri for once and all kutokana na mapesa watakayopewa na hawa wazungu ili kuhalalisha yasiyohalalishika yaliyopo kwenye mikataba, au kufanya kazi ya maana kwa utaifa ili kuibua ukweli wa mambo na kupendekeza radical changes zitakazotufanya nasi tufaidi kasehemu kadogo kaliko baki kwenye yale mashimo-na kwa kufanya hivyo waibuke mashujaa wa taifa in the rest of their life. Mimi siwajui sana wengine, lakini nina imani ya kutosha na Zitto. Lakini hatuwezi kufumbia macho ukweli kwamba hawa wote walioteuliwa ni wanasiasa, sasa don't forget the three enemies of a politician: money, sex and an insatiable thirsty for power!
 
Zitto kajinyamazisha mwenyewe! J.K tactics will work if you consider practical guidelines of forming a committee for instance....
the government has affirm its confidence in the integrity of members who are appointed to serve on this committee:- By appointing a bipartisan committee. To say the committee has a vacuum of akilimali is to say You have no confidence in the Presidents decision ! Yet an affirmation of the integrity of these mambers....
Conflict of Interest
Because of the nature of the work of such committee, those who serve on them must be especially sensitive to conflict of interest situations and the appearance of impropriety.

A conflict of interest occurs when an individual's personal or private interests may lead an independent observer reasonably to question whether the individual's professional actions or decisions are influenced by considerations of significant personal or political party interest, financial or otherwise. And to say it was bipartisan! I think there is a need to think wiser.
Confidentiality
There is also the issue of confidentiality you know a good committee member need to maintain a high degree of confidentiality regarding the committee’s discussions, both oral and written.
Mind you committee members need to feel free to speak frankly in a closed session, knowing that their comments will not be repeated outside that room, and that they preserve the right to speak for themselves outside of that closed session.
Here ziito will find himself in a dillema...with his glamourized tactics and also mamber of such commitee he might be bound with both hands and feet!
When it comes to KUPIGAMAKELELE there are Guidelines on publicity which members might not reveal or publicize any confidential information learned through service on the committee; nor should they make such confidential information available to non-committee-members(kama vile mwanakijiji)LOL.

Members of the committee who run or participate in social networking web sites(we see Zitto here sometimes) or software, including blogs, wikis, electronic discussion lists, and the like, should not engage in any discussions about their committee work, or about the status of commitees work during their term of committee service. Will Zitto adhere to such?
Once they sign of such a guideline their work is only known to His Excellency J.K And in such it is likely Zitto might go green!
source:Google/Wikipedia/
 
Watanzania ni rahisi sana kudanganywa kama watoto kwa peremende,eti kamati ya kuangalia upya mikataba ya madini? na kwa akili zenu mnaamini kabisa hapo kuna mikataba itabadilishwa kutokana na mapendekezo ya hii kamati,yaani ni kichekesho kweli kweli mpaka inatia huruma
 
Zitto kajinyamazisha mwenyewe! J.K tactics will work if you consider practical guidelines of forming a committee for instance....
the government has affirm its confidence in the integrity of members who are appointed to serve on this committee:- By appointing a bipartisan committee. To say the committee has a vacuum of akilimali is to say You have no confidence in the Presidents decision ! Yet an affirmation of the integrity of these mambers....
Conflict of Interest
Because of the nature of the work of such committee, those who serve on them must be especially sensitive to conflict of interest situations and the appearance of impropriety.

A conflict of interest occurs when an individual's personal or private interests may lead an independent observer reasonably to question whether the individual's professional actions or decisions are influenced by considerations of significant personal or political party interest, financial or otherwise. And to say it was bipartisan! I think there is a need to think wiser.
Confidentiality
There is also the issue of confidentiality you know a good committee member need to maintain a high degree of confidentiality regarding the committee’s discussions, both oral and written.
Mind you committee members need to feel free to speak frankly in a closed session, knowing that their comments will not be repeated outside that room, and that they preserve the right to speak for themselves outside of that closed session.
Here ziito will find himself in a dillema...with his glamourized tactics and also mamber of such commitee he might be bound with both hands and feet!
When it comes to KUPIGAMAKELELE there are Guidelines on publicity which members might not reveal or publicize any confidential information learned through service on the committee; nor should they make such confidential information available to non-committee-members(kama vile mwanakijiji)LOL.

Members of the committee who run or participate in social networking web sites(we see Zitto here sometimes) or software, including blogs, wikis, electronic discussion lists, and the like, should not engage in any discussions about their committee work, or about the status of commitees work during their term of committee service. Will Zitto adhere to such?
Once they sign of such a guideline their work is only known to His Excellency J.K And in such it is likely Zitto might go green!

Umeeleza vyema Atanaye,
Hata hivo ushauri wa bure kwa Zitto ni kwamba hapa kapewa turufu ya hatma yake ya baadae kisiasa sasa ni ama:

Ajimalize mwenyewe kwa kukubali kunyamazishwa na 'kuturn green' kama ulivo sema,

Ama asimamie upande wa haki ili kungalisha turufu yake kama ilivo anza kuchanua.

Ukweli ni kwamba kila mtu atafatilia sana kamati hii hasa kwa mategemeo makubwa kwamba Zitto sasa ata tumia nafasi hii kuweka wazi na kuanzisha kile ambacho kimewavuta watanzania wengi juu yake! Natumaini he will not go that much cheap kwa ajili ya mafanikio yake ya mbele na mapenzi ya taifa letu kwa ujumla.
 
Back
Top Bottom