Elections 2010 JK amtambulisha Shigongo Buchosa

Safari_ni_Safari

JF-Expert Member
Oct 5, 2007
23,268
17,097
Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM, Jakaya Mrisho Kikwete, amemtambulisha Mwalimu wa Kimataifa wa Ujasiriamali, Eric James Shigongo kwamba ndiye mpigadebe mkuu wa chama hicho jimboni hapa.

Kikwete, alimtambulisha Shigongo jana kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni jimboni hapa na kueleza kwamba ndiye atakayesimamia na kuongoza ‘mpango mzima’ wa kumnadi Mgombea Ubunge wa Buchosa,Dk. Charles Tizeba.

Shigongo, alikuwa mmoja wa wana CCM, walioomba kuteuliwa kugombea ubunge Buchosa katika kura za maoni, lakini Halmashauri Kuu ya chama hicho (NEC), ilipitisha jina la Tizeba.Katika hotuba yake jana, JK alimuelezea Shigongo kama kada mwaminifu wa CCM na kueleza kwamba alimuomba avunje kambi na kumuunga mkono Tizeba.

“Huna haja ya kununa, mimi mwaka 1995 nilishindwa na mzee Mkapa (Rais Mstaafu), nikakubali matokeo baada ya miaka 10 nikashinda na kuwa Rais,” alisema JK na kuongeza:
“Namfahamu Shigongo kwa sababu kwanza ni mtani wangu, halafu pale Dar es Salaam ana kampuni yake ya magazeti, nadhani mnayajua.”:lol:

JK aliendelea kusema: “Zaidi ya hayo yote Shigongo ni jirani yangu, ana shamba la mananasi kule Bagamoyo linapakana na la kwangu.”

Aidha, JK alitania na kuifanya hadhira iangue kicheko: “Kipindi fulani alitaka kusogeza mpaka wa shamba lake na kuingia kwangu, nikamwambia huku usifike.”:lol:

Baada ya kusema maneno hayo, JK alisema Shigongo ni safi na Tizeba ni safi na kusababisha umati uliohudhuria mkutano huo umshangilie kwa nguvu.

Kwa Hisani ya GP
 
Kweli huyu Mgombea ana matatizo kweli kweli. Hivi anamuona Sshigongo ni mtu wa maana? Mtu anayechapisha majarida yalioyojaa uongo, kughushi picha, mtu aliyetenganisha ndoa za watu na madhambi mengine kama vile kusaidia kuporomosha maadili katika jamii bado JK ana-mparedi mbele ya wananchi waliomkataa ktaika kura za maoni? Kweli tunaye mgombea wa rais!

Namkumbuka Mwl Nyerere -- asingeweza kufanya kitu cha namna hii kamwe. Na hebu nikumbushen hapo katika jimbo hilo si ndiko JK alimpigia debe la sapoti Mbunge aliyemaliza kipindi chake -- Chitalilo baada ya kutuhumiwa kughushi vyeti vya shule? Baada ya kauli hiyo ya JK waendesha mashitaka wa serikali walikataa kabisa kumshitaki Chitalilo! Kweli this is a really f****** country!!!!
 
Mbona anasoma zaidi speeches zilizoandikwa na watu wengine bila kutumia bongo yake?......sikuwahi kumuona Nyerere akisoma makaratasi yaliyoandikwa na watu wengine
 
Aidha, JK alitania na kuifanya hadhira iangue kicheko: “Kipindi fulani alitaka kusogeza mpaka wa shamba lake na kuingia kwangu, nikamwambia huku usifike.”:lol:

Inahuuusuu??
 
SHIGONGO.jpg
Bw. Eric Shigongo

08_10_k23f0h.jpg

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM, Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwahutubia wananchi
katika kata ya Nyehunge jimbo la Buchosa,wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza Juzi.

Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM, Jakaya Mrisho Kikwete, amemtambulisha Mwalimu wa Kimataifa wa Ujasiriamali, Eric James Shigongo kwamba ndiye mpigadebe mkuu wa chama hicho jimboni hapa.

Kikwete, alimtambulisha Shigongo jana kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni jimboni hapa na kueleza kwamba ndiye atakayesimamia na kuongoza ‘mpango mzima’ wa kumnadi Mgombea Ubunge wa Buchosa,Dk. Charles Tizeba.

Shigongo, alikuwa mmoja wa wana CCM, walioomba kuteuliwa kugombea ubunge Buchosa katika kura za maoni, lakini Halmashauri Kuu ya chama hicho (NEC), ilipitisha jina la Tizeba.
Katika hotuba yake jana, JK alimuelezea Shigongo kama kada mwaminifu wa CCM na kueleza kwamba alimuomba avunje kambi na kumuunga mkono Tizeba.

“Huna haja ya kununa, mimi mwaka 1995 nilishindwa na mzee Mkapa (Rais Mstaafu), nikakubali matokeo baada ya miaka 10 nikashinda na kuwa Rais,” alisema JK na kuongeza:
“Namfahamu Shigongo kwa sababu kwanza ni mtani wangu, halafu pale Dar es Salaam ana kampuni yake ya magazeti, nadhani mnayajua.”

JK aliendelea kusema: “Zaidi ya hayo yote Shigongo ni jirani yangu, ana shamba la mananasi kule Bagamoyo linapakana na la kwangu.”

Aidha, JK alitania na kuifanya hadhira iangue kicheko: “Kipindi fulani alitaka kusogeza mpaka wa shamba lake na kuingia kwangu, nikamwambia huku usifike.”

Baada ya kusema maneno hayo, JK alisema Shigongo ni safi na Tizeba ni safi na kusababisha umati uliohudhuria mkutano huo umshangilie kwa nguvu.

Duh nilishtuka sana kuona Jk eti anamtambulisha huyu jamaa maana najua alishidwa kumbe anamtambulisha kama mpiga kabobo aka debe wa Dr.Tizeba... Teh Teh, ila si bure huenda ameaahidiwa kitu huko mbeleni tusubiri tuone...

Nukuu in RED and bolded inashangaza kweli Rais waweza ongea maneneo haya???
 
Hii ndo naisikia kwa mara ya kwanza. Mpiga debe nae anatambulihwa?
 
Ni vema, kama Shigongo akijipanga vizuri atafanikiwa baadae!

Kwa Shingongo nadhani hiyo ni strategy nzuri sana. Ila huyo mgombea yuko hatarini kwani jamaa anaweza kumfunika sana. Na ikitokea matokeo yakatenguliwa na mahakama au 2015 takuwa tayri yuko ICU. Kwa hiyo Shigongo amepewa rungu la kuunda mtandao mwingine wa hatari kama ule wa 2005. The guy must have an evil mind, ngoja sisi tuendelee kukodoa macho. :glasses-nerdy:
 
Shigongo ana vigazeti vyake hapa vinahangaika na maisha binafsi ya watu maarufu. JK lazima amwogope kwa kuwa naye ni mtu wa makandokando mengi.
 
hilo shamba alilokuwa anasema JK kuwa Shigongo alikuwa anataka kusogeza mpaka ni kitu ingine kabisa wala sio shamba. Wajanja wanaijua.
 
hilo shamba alilokuwa anasema JK kuwa Shigongo alikuwa anataka kusogeza mpaka ni kitu ingine kabisa wala sio shamba. Wajanja wanaijua.

"Kipindi fulani alitaka kusogeza mpaka wa shamba lake na kuingia kwangu, nikamwambia huku usifike." Ina maana jamaa alitaka kuingia anga za mkuu nini hebu tufafanulie???
 
Jamani mbona mnamsakama mgonjwa wetu hivyo. Hizi kauli anazitoa kwa kuwa bado mgonjwa. Akipona ndo ataanza kuongea point. Hatujui atapona lini (may be in 7 years to come). Tumvumilie
 
Katika hotuba yake jana, JK alimuelezea [COLOR=darkred][B]Shigongo kama kada mwaminifu wa CCM[/B][/COLOR] na kueleza kwamba alimuomba avunje kambi na kumuunga mkono Tizeba.

"Huna haja ya kununa, [COLOR=darkred][B]mimi mwaka 1995 nilishindwa na mzee Mkapa (Rais Mstaafu), nikakubali matokeo baada ya miaka 10 nikashinda[/B][/COLOR] na kuwa Rais," alisema JK na kuongeza[/QUOTE]

Ukizoea mambo ya ushindi wa avatar yangu huwezi kuacha! Jk sasa hivi nadhani medulla kwishnei​
 
Mgonjwa kapona jamani na anaendelea na kampeni kama kawaida

Kapona au kapata ahueni....huewezi kuanguka mara nne ukapona......

Syncope is the medical term for fainting, a sudden, usually temporary, loss of consciousness generally caused by insufficient oxygen in the brain either through cerebral hypoxia or through hypotension, but possibly for other reasons. Typical symptoms progress through dizziness, clamminess of the skin, a dimming of vision or greyout, possibly tinnitus, complete loss of vision, weakness of limbs to physical collapse. These symptoms falling short of complete collapse, or a fall down, may be referred to as a syncoptic episode.
 
"Kipindi fulani alitaka kusogeza mpaka wa shamba lake na kuingia kwangu, nikamwambia huku usifike." Ina maana jamaa alitaka kuingia anga za mkuu nini hebu tufafanulie???

ishu flani ya mwanamuziki maarufu, upo kaka?
 
Back
Top Bottom