JK Ampeleka Augustino Mrema kutibiwa India?

Kiranja

JF-Expert Member
May 19, 2007
751
336
Taarifa nilizozipata hivi punde Nikiwa hapa mjini Dodoma kutoka kwa source ya kuaminika ni kuwa Agustino Mrema amepelekwa Nchini India kutibiwa .

Aliyemsafirisha ni Rais Jakaya Kikwete.

My take;
Ndio maana alikuwa anampigia filimbi JK kumbe alikuwa anataka kupata malipo?
Akirudi anaweza naye kuwa mtabiri kama Sheikh Yahaya,juu ya urais wa JK?
 
Ameondoka jana na ameenda kutibiwa hospitali ya Appolo iliyopo India.
 
kwani anaumwa nini

Amekuwa akisema kuwa anasumbuliwa na kisukari kwa muda mrefu sana ,ugojwa ambao ulipelekea hata sura yake kuwa kama mtu aliyeunguzwa na maji ya moto-yaani kupauka na kuwa na mabakamabaka usoni.
Hata kwenye mikutano yake ya hadhara alikuwa hawezi kuongea zaidi ya nusu saa bila kunywa maziwa akiwa jukwaani .

Kwa wale waliowahi kumwona siku za usoni wataelewa alivyokuwa amedhoofu afya yake.
 
kwani anaumwa nini

Ninavojua yule mzee wa kiraracha huwa ana tatizo la kisukari.

Nadhani kama amepata nafasi hiyo anastahili kwa kuangalia aliyoyafanyia nchi hii wakati akiwa waziri wa mambo ya ndani na 'naibu waziri mkuu'.

Sioni ubaya hapo zaidi namwombea apate nafuu/apone haraka
 
Umejuaje amelipiwa na JK.

Amelipiwa gharama zote na JK ,na hapa sisemi kuwa ni serikali no. Ni JK personaly ndio amelipia gharama zote kuanzia tiketi ya ndege hadi matibabu yake yote akiwa huko.
 
Taarifa nilizozipata hivi punde Nikiwa hapa mjini Dodoma kutoka kwa source ya kuaminika ni kuwa Agustino Mrema amepelekwa Nchini India kutibiwa .

Aliyemsafirisha ni Rais Jakaya Kikwete.

My take;
Ndio maana alikuwa anampigia filimbi JK kumbe alikuwa anataka kupata malipo?
Akirudi anaweza naye kuwa mtabiri kama Sheikh Yahaya,juu ya urais wa JK?

well.. kuna stori behind all this..
 
JK ndio zake hata Sheikh Yahya alishamlipia...huwa wakirudi wanapaparika sana kumpamba....bado mtikila
 
Amelipiwa gharama zote na JK ,na hapa sisemi kuwa ni serikali no. Ni JK personaly ndio amelipia gharama zote kuanzia tiketi ya ndege hadi matibabu yake yote akiwa huko.

Ni haki yake kulipiwa kwanza amelitumikia taifa hili kuliko huyo Shekhe Yahya ambaye naye alilipiwa na JK kweli Mrema amelitumikia Taifa hili kwa hali na mali uaminifu wake kwa taifa ndio ulimpoza ndugu yangu alifikiri wako wengi wa aina yake serikalini kumbe yupo pekeyake.
 
nadhani hapa duniani hakuna kitu chenye thamani kubwa kuliko uhai wa binadamu; haununuliki. Kwa hiyo, juhudi zozote za kurefusha uhai wa binadamu yeyote bila kujali itikadi yake ni jambo la muhimu sana. Namshukuru JK kwa hilo ingawa nilisikitika sana kusikia kuwa General Nyirenda hakupewa msaada wa namna hiyo alipokuwa mgonjwa.


Ninadhani kuwa jambo kubwa lisiwe la kuwapeleka hao wateule kutibiwa nje na kuwaacha akina Kichuguu wajifie Mwananyamala bila hata kitanda. Kinachotakiwa ni kujenga huduma za afya nchini ziwe za ubora wa juu kiasi kuwa hata watu wa nje waje kutibiwa kwetu. Tumeona siku hizi wachezaji wa mpira kutoka nje wanakuja kucheza kwenye vilabu vyetu, inabidi hata huduma zetu za elimu na afya pia tuziinue katika viwango vya kukubaliwa kimataifa kusudi watu wa nje nao waje kuzifuata kwetu.
 
Ndugu zangu waTZ, hivi utaratibu wa kupeleka watu nje kwa matibabu unaratibiwa vipi na nani?
  1. Inaonekana kutibiwa nje ya TZ nako sasa imekuwa ni hongo ya mkuu wa nchi kwa wanaompigia magoti, je hili sio la kweli?
  2. Kwa nini kila high profile citizen ndio tu inakuwa rahisi kwenda kutibiwa nje ingawa tunaolipia matibabu yao ni sisi kwa kodi zetu?
  3. Kwa nini list ya wanaotarajia kupelekwa nje kwa matibabu isiwekwe wazi wizarani, kwenye gazeti la serikali n.k., ili kuondoa upendeleo?
  4. Kwa nini gharama ya kila mgonjwa anayepelekwa nje zisiwekwe wazi ili tuone tofauti na gharama za wagonjwa wanaotibiwa TZ?
 
namtakia mrema kila la kheri arudi salama na pia namuombea uzima yoyote aliyemsaidia mrema kupata tiba

angalizo, kisukari cha kutibiwa india hicho lazima kitakua cha pekee
 
Kutibiwa ni kura ya turufu ha ha ha ha kweli nchi hii imekuwa biashara. Pesa ya walipa kodi, hivi hii ndiyo kazi mojawapo ya rais kuchagua nani apelekwe kwenda kutibiwa mje ya nchi.

Serikali ya Chama cha Majambazi badala ya kuimarisha huduma za ndani kutibu magonjwa kama haya nchini wanaona ufahari kutuma wagonjwa wake nje ya nchi. hii ni aibu kubwa kwa waliokabidhiwa dhamana ya kuona haki inatendeka.
 
Ndio maana alikuwa anampigia filimbi JK kumbe alikuwa anataka kupata malipo?
Akirudi anaweza naye kuwa mtabiri kama Sheikh Yahaya,juu ya urais wa JK?
Kwani Yahaya Hussein na Mrema... si wote watu wa TISS, sasa tatizo nini wakilipiwa matibabu...!? Wote si wapo kwa ajili ya kuendeleza utawala wa chama tawala?
 
Back
Top Bottom