Elections 2010 JK amesema uongo?

MwanaHaki

R I P
Oct 17, 2006
2,401
705
Ingelikua nimeambiwa, wala singediriki kuyasema haya, lakini kumbe ni uongo?

Kwanza, JK ametamka jana kwenye kampeni mkoani Kilimanjaro kwamba Serikali imefanikiwa kuwapeleka watumishi 47 wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, kwenda India, Marekani na Israel (ni baadhi tu ya nchi alizotaja...) kusomea uuguzi, nusu kaputi na udaktari wa magonjwa wa moyo, lengo likiwa kuwa na uwezo wa kufanya upasuaji wa moyo hapa nchini.

JK amesema kwamba "hawa ni vijana wadogo lakini ni very bright people", yaani wana uwezo mkubwa. Kudhihirisha hilo, JK amesema kwamba mwaka huu, tayari upasuaji (open heart surgery) umefanyika kwa wagonjwa 258.

Nimewadadisi baadhi ya madaktari wa Muhimbili, wamesema hilo si kweli.

JK anazidi kudhihirisha jinsi yeye mwenyewe na Serikali yake wasivyo makini. Jambo kama hili, la takwimu, unapaswa kuwa na takwimu ZINAZOTHIBITIKA, sio za KUFIRIKIKA!

Kwa mtaji huu, tutarajie Serikali itakayoendesha shughuli zake kwa dhana na hisia, si kwa uwazi na ukweli!

Unataka mabadiliko toka kwa CCM? Hakuna mabadiliko. Ni SI-HASA tu!

Kama bado unaamini kwamba CCM ndicho chama kinachofaa, utakapounguzwa kikaangoni usilalamike hukuonywa.

Siku njema.

-> Mwana wa Haki

Paople's Power! 2010 Hatudanganyiki! Join the Movement for Change NOW!
 
USA kuna kitu wanaita "facts check" Kila mwanasiasa akitoa issue, wako wataalamu wanacheck kama kweli kuna ukweli au uongo kw akitu alichozungumza, na wanarule kuwa either the assetion ni misleading au ni correct. I think tunahitaji kitu kama hicho Tanzania, itasaidia sana kuwakomesha wanasiasa wanaotoa data ambazo :mad2:hazina vichwa wala miguu. Niliona hata Salma Kikwete anatoa data, kweli kuna kazi sana TZ
 
Well said mkuu, Ndiyo maana tunahitaji midahalo ili kila mgombea aeleze jinsi gani atatufanyia watanzania kwa ahadi zake anazosema wakati wa Kampeni!
 
Aaaaah jamani kwani ni mara ya kwanza kwa Mkwere huyu kudanganya au kudanganywa? kazi yake kusoma hotuba aliyondaliwa na kwa kuwa anareasoning capaciy ndogo basi anaisoma kama ilivyo, huyu ni mpambaji wa jukwaaa tu, Kweli rais unaweza kutoa ahadi ya bajaji kama ambulacne tena vijijini? Huu si upopopo jamani? Tumuacheni tu msanii wetu ashangiliwe kwa pumba zake jukwaani.
 
mimi niliwauliza madakatari pale muhimbi wakaniambia kweli. sasa aaminiwe mimi au wewe?
Kwakuwa wewe ni JK, na umezoea kudanganywa, na kila mtu anajua wewe ni kichwa cha mwendawazimu kwakuwa huwa unakiri hadharani kupotoshwa na wasaidizi wako, na kwakuwa huwa huwachukulii hatua yoyote wanaokudanganya basi hata hao madaktari wa Muhimbili walikuwa wanatamani sana kukujaribu waone kama ni kweli unadanganyika wakakupa takwimu za uongo! Wameamini kuwa kumbe kweli ukiambiwa huchanganyi na za kwako (kama zipo) bali unakwenda na ulichoambiwa hivyo hivyo kizima kizima. Sasa wataandika pepa kuwa kuna kiongozi zuzu anataka watanzania waendelee kuwa mazuzu ili tanzania iendelee kuwa ya mazuzu!

Pole JK, do your homework sometimes! Uki-copy na ku-paste tu always madhara yake ndio haya...! Mbona Nyerere hakudanganyika? Unajua kwa nini? Alikuwa anafanya homework yake!
 
mimi niliwauliza madakatari pale muhimbi wakaniambia kweli. Sasa aaminiwe mimi au wewe?

yaya kumbe upo? Naomaba maelezo ni kwanini ccm inakubali kupokea invoice in foreign currency kinyume cha sheria, ilihali mara kwa mara benki kuu imekuwa ikitoa adhari kuwa dolalarisation of the economy is responsible for the ever rising inflation in the country?

Acha kuchagua post
 
Ikiwa mkuu alidanganywa kwenye kufungua hoteli ya Arusha,Kwenye kukabidhi gari la wagonjwa Ikulu, na kuambiwa akilipa mishahara ya wafanyakazi kama TUCTA wanavyotaka itakuwa trilion6, na kali kabisa kukabidhiwa kadi mpya za CHADEMA akidanganywa ni za wanachama waliohama wakati hata mtoto mdogo angegundua hilo, si ajabu kadanganywa tena katika hili!
 
Kwakuwa wewe ni JK, na umezoea kudanganywa, na kila mtu anajua wewe ni kichwa cha mwendawazimu kwakuwa huwa unakiri hadharani kupotoshwa na wasaidizi wako, na kwakuwa huwa huwachukulii hatua yoyote wanaokudanganya basi hata hao madaktari wa Muhimbili walikuwa wanatamani sana kukujaribu waone kama ni kweli unadanganyika wakakupa takwimu za uongo! Wameamini kuwa kumbe kweli ukiambiwa huchanganyi na za kwako (kama zipo) bali unakwenda na ulichoambiwa hivyo hivyo kizima kizima. Sasa wataandika pepa kuwa kuna kiongozi zuzu anataka watanzania waendelee kuwa mazuzu ili tanzania iendelee kuwa ya mazuzu!

Pole JK, do your homework sometimes! Uki-copy na ku-paste tu always madhara yake ndio haya...! Mbona Nyerere hakudanganyika? Unajua kwa nini? Alikuwa anafanya homework yake!

Hapa umenena vema, sidhani kama kuna msaada mwingine utakaohitajika kumsaidia zaidi ya huo uliompa huyo jamaa.
 
Back
Top Bottom