JK amemsimamisha Jairo kupisha uchunguzi wa Bunge - PINDA

tatizo kikwete ni kama rais wa chuo kila muda anasubiria management imtolee maamuzi, hii ni aibu kwake na kwa taifa zima
 
UPDATES: 25/8/2011

Ikulu ya cheza picha la kihindi! Jana baada ya mkuu wa kaya kurudi magogoni kilikalika kikao na bwana Luhanjo akatoa taarifa ya kikao chake na akina Jairo na ikajadiliwa hali ya mambo bungeni!
Moja ya nilichokitafsiri ni kuwa Ikulu na Bungu wanatofautiana sana juu ya Jairo!
Maamuzi ya kikao cha usiku wa jana ni kuwa kwakuwa mda wa Luhanjo kustaafu ulishafika na mpaka leo yupo kwa hisani ya mkuu wa kaya basi walizuge taifa kuonyesha umma kuwa ikulu imesikitishwa na maamuzi ya Luhanjo hivyo imemtimua kazi!
Wazo hilo alilito Luhanjo mwenyewe, japo kikwete alisita kidogo lakini Luhanjo alifafanua jinzi mbinu hii itakavyo badili upepo na hali ya mambo itakuwa shwari ndipo mkuu wa kaya akakubali wazo hilo!

Spika wa bunge aliwasiliana na mkuu wa kaya mida ya saa nne na dk kumi na akamueleza dhamira ya bunge kuomba ushauri:
1. Nani awaweke katika kamati
2. Nini wakifanye hao wanakamati

Mkuu wa kaya akaomba kuwa ngoja atulize kichwa kwanza atatoa dokezo!!
Kikubwa msitegemee jipya kutoka ktk kamati hiyo kwakuwa inateuliwa na ikulu!
Last edited by Jason bourne; Today at 08:15 AM.​

sonma hapo juu what next akisimamishwa?
 
Hongera JK kwa kufanya maamuzi mazito, magumu na ya kiume. Sasa wapinzani wako sijui watapata wapi cha kuongea? Umethubutu, Umeweza sasa hebu SONGA MBELE!

Au walazimishwe kulisukuma gari la Jairo kuelekea nje ya ofisi za wizara! They have to undoe their Yesterday's actions.
 
Raisi J K amemsimamisha kazi Bwana Jairo, Hii ni kauli iliyo tolewa na Waziri mkuu wakati akijibu swali la Mh. Mbowe asubuhi hii

Safi sana, tunangoja amsimamishe na Luhanjo
 
Je Rais na hili la pembeni halioni?
images
 
na wale wafanyakazi wa wizara ya nishati na madini waliosukuma gari lake nao wasimamishwe haraka sana

Wlionekana wakimsindikiza kuondoka ofcn jana mchana, hukuwaona?
 
na wale wafanyakazi wa wizara ya nishati na madini waliosukuma gari lake nao wasimamishwe haraka sana

Mimi siungi mkono hili hata kidogo kwa hali halisi hawa wafanyakazi walikuwa na nia tofauti. Wengi wao itakuwa ni WOGA kwani Luhanjo alisema waliotoa siri wachukuliwe hatua sasa wewe utaona wenzio wanasherehekea na wewe ukae tu ofisini?? si ndo mwanzo wa kushilkwa uchawi hapo??

Nyie acheni tu Organization Politics za SIRIKALI ni ngumu sana
 
hiyo naona haiko sawa, nilitegemea SERIKALI ingetoa jibu la namna hiyo kabla ya kuulizwa swali. Funika kombe mwanaharamu apite
 
Hongera JK kwa kufanya maamuzi mazito, magumu na ya kiume. Sasa wapinzani wako sijui watapata wapi cha kuongea? Umethubutu, Umeweza sasa hebu SONGA MBELE!

Mpe pole na si ongera, ina maana hapo hakuna mawasiliano au maelewano mazuri kati yake na katibu mkuu, naqwasilisha
 
Back
Top Bottom