JK amcheza bintiye ngoma

..mwacheni bwana acheze ngoma ya kwao..ndio gharama hizo....lazima tuwepo kumlinda..au sio,...hangeweza kuacha kumcheza mwanae just kwa kuwa ni rais...na serikali isingeacha kutupia jicho pale just kwa kuwa yupo ngomani........

...labda mseme cheki ya kugharamia shughuli hii ilitoka ikulu???.......au tuseme ngoma zetu ni za kishenzi..???...

kumbuka rais aliwatetea wale watu wa uyui ..amabapo mkuu wa wilaya alipiga marufuku ngoma kwa saababu ya mimba...akasema mbona mijini hakuna ngoma na mimba zinaingia,,,..alitaka viongozi waheshimu mila na desturi za watu..
 
..hivi Raisi angekuwa Mmaasai halafu akampeleka kijana wake jandoni mngelalamika?

..mila na taratibu tunapaswa kwenda huko tukizirekebisha na kuziboresha zilingane na mazingira yetu ya sasa.

..wasomi kama Raisi Kikwete na Mama Salma ndiyo wenye credibility ya kwenda Msoga na Lindi na kuwaelekeza wananchi jinsi ya kuziboresha mila zetu.

..nina hakika binti ya Kikwete aliyechezwa atakuwa amesoma shule. sasa huo utakuwa mfano mzuri sana kwa wananchi wa Msoga na Lindi kwamba mila na elimu vinaweza kwenda pamoja.

..kuhusu matumizi mabaya ya kodi ya wananchi, hilo linazungumzika. tunaweza kuweka mipaka kwa masuala binafsi na yale ya kiserikali. lakini lazima tufahamu kwamba ULINZI WA RAISI ni suala ambalo halina mjadala.

NB:

..kuna mila kama ukeketaji wanawake ambazo ni mbaya na zenye madhara kwa afya ya binadamu. hizo tunapaswa kuzikataa.
 
Katika hali ambayo si ya kushangaza, Rais JK amemcheza ngoma bintiye (yaani kufundwa jinsi ya kuishi na mume)....

Kumbe katika hali ambayo si ya kushangaza !! Basi kama si ya kushangaza, tuendelee na thread nyingine, kwani hali hiyo ni ya kawaida (according to the thread starter).
 
Mwendawazimu akizindukia kwenye pipa la pombe si kitu cha ajabu! JK bwana mara hili mara lile...Ukimaliza kumcheza mwanao, rudi utucheze na sisi Watanzania wenzako pia! Tunakusubiri
 
haya ndio mambo ninayoyapenda mie...sio udhungu tuuuuu

na asikuongopee mtu huwezi kijiita mtoto wa mjini halafu ukaenda kuoa mwanamke ambaye hajachezwa
 
haya ndio mambo ninayoyapenda mie...sio udhungu tuuuuu

na asikuongopee mtu huwezi kijiita mtoto wa mjini halafu ukaenda kuoa mwanamke ambaye hajachezwa

Unajua wewe kajamaa uko kashamba sana. Unahusudhisha utoto wa mjini utadhani kuna uspesho flani hivi kumbe hakuna lolote. DNA ya mtoto wa mjini na yule wa kijijini haina tofauti. Wote mavi yao yananuka na wote watakufa na kuoza na kugeuka kuwa funza, nyungunyungu, taka, tope, udongo na mazagazaga mengine.....
 
JK amefanya jambo jema kumcheza mwanae, hii ni heshima kwake na kuwa mfano kwa wengine. Penda chako, jenga chako.
Kwa upande wa gharama za sherehe wala sio issue, JK ni mtu wa watu, Mama Salma pia ni mtu wa watu, natumaini Mashosti 10 tuu wa Mama Salma wangeweza kuwakesesha Bagamoyo siku 7. Kwa wajuao mambo ya ngoma, shughuli ni usiku mchana ni wanandugu tuu,
Ulinzi pia sio issue, hata kama wewe una kajisherehe chako nyumbani, toa taarifa kituo cha polisi, utapatiwa ulinzi. Hata ukitaka Traffic wa pikipiki aongoze msafara wako wa harusi, na yale mabenzi meusi 100 ya State Excecutive cars, unapewa.
JK mwenyewe alitia timu siku ya kilele tuu. Jamaa ana ulinzi wake siku zote popote. Hata kama akienda tembelea mabesti wake kama RA, anakwenda na kikosi chake.
Na mwisho, hata JK has the right to privacy. That was not a State Banquet but a private function, kutaka kujua gharama na nani kalipa is none of our bussiness.
Any body paid by taxpayers money, the public has the right to know their public and private conduct. Kuchezwa ngoma ni shughuli ya kinamama. Salma kamwalika Jakaya siku ya kilele, hivi nayo inakuwa nongwa?. Where is his right to privacy?.
 
hakuna tatizo kumweka binti yake unyagoni asijemwita mme wake "babue" na kuwaaibisha wazazi wake akiwamo mtukufu rais. nampongeza sana kwa kutunza mila. Hata hivyo sipendi bili ile ilipwe na mimi kwa vile huyu siyo binti wa taifa eti. Ningependa kujhua nani alikuwa anwalipa wale FFU waliokaa pale kwa siku hizo zipatazo kumi.
 
Utatambuaje kama Tanzania tuna Raisii,MAtendo jamani,jamani matendo,matendo jamani matendo yake utamtambua eeeee..... ukitaka kujua kama ni raisi,hauna haja yakuuliza watu,matendo jamani matendoo,matendo jamani maatendo utamtambua eeeeee....
 
Utatambuaje kama Tanzania tuna Raisii,MAtendo jamani,jamani matendo,matendo jamani matendo yake utamtambua eeeee..... ukitaka kujua kama ni raisi,hauna haja yakuuliza watu,matendo jamani matendoo,matendo jamani maatendo utamtambua eeeeee....

Mkuu hii mbona imekaa kama chorus.....JF kuna watu wa kila fani!! Loooh
 
Nadhani tunakuwa wepesi kukimbilia kwenye kulaumu au kunung'unika kabla hatujapata ukweli wa jambo lenyewe. Hapa hatujaambiwa ni kiasi gani kimetumika katika sherehe hizi. Je ni kiasi ambacho JK mwenyewe kama JK hawezi kukimudu! Tupate details kwanza.

kunguni nakuunga mkono yani lawama zimeanza hata watu hawana dataz kamili za shughuli yenyewe na pia watu wakumbuke kua sherehe kama hiyo haiwezi kumshinda rais kuigharamia mwenyewe hata kwa mshahara wake tu.kwa hiyo tusiwe kila kitu afanyacho rais tuone ni ubadhilifu tu tukumbuke yeye ni mtu wa kama sisi na anafamilia na anamaisha pia
tuacheni haya mambo,maana sasa sijui mnataka rais aishije ?

Urambo Tabora
 
Nampongeza sana Rais kwa kuendelea utamaduni wake. Suala la gharama za ulinzi sioni mantiki yake maana hata baada ya kuisha hiyo ngoma walinzi watakuwepo tu. Hata sasa hivi wapo pale pale (labda wapunguzwe). Kuhusu kuacha kazi kwenda kucheza ngoma, nadhani hilo lipo mikononi mwa waalikwa. Maana hawakulazimishwa. Naamini wasingealikwa pale wangekwenda kucheza ngoma kwa mwingine. Mkuu ameamua kumfunda mwanae kama inavyotakiwa. Ametimiza wajibu wake kama mzazi. Asingetimiza, wengine wangedai "Pamoja na uwezo wote alionao ameshindwa hata kumfanyia hata kasherehe kama hako mtoto wake mwenyewe?"
 
Back
Top Bottom