JK akiri serikali haiaminiki - AFICHUA KISA CHA KUACHWA MA-DC

eti anasema hao wakuu waache kugawa ardhi ovyo...kwani ni nani anayegawa ardhi kama sio yeye na mawaziri wake... huyu mkuu wetu sijui anafikiri anaongea na watoto wa darasa la pili ama vipi
 
Rais wetu JK mara nyingi matendo yake tofauti kabisa na matendo ameteua wakuu wa wilaya ambao wengi ni wanajeshi na askari wantafu anaposema wazee watoke wawaachie vijana anamanisha nini, kijana ni under 45 karibu robo tata ya wakuu wa wilaya alioteua ni over 45 ambao tayari si vijana
 
Hii ya Wazee kuwapisha Vijana Haraka Haraka italisababishia Serikali ya CCM matatizo makubwa haswa; Ukiangalia Utendaji ya wajumbe wa CC Vijana na ni Wasomi ni hatari kama Vile Mchemba na Nape ni kama Vile hawajaenda Shule hawana Mwamko hawana Hekima, Muda wao Wote ni Ugomvi yoyote aliye upinzani ni Adui wao.

Nakubaliana na wewe kabisa katika hili.

Ni kweli, mie mwenyewe ni kijana na ningependa kuona vijana wanapewa fursa ya uongozi lakini usimamizi wa karibu kutoka kwa Wazee unahitajika sana. Maana sie vijana tukishatoka home kwa baba na mama tunataka tujaribu kila kitu tunachofikiri kuwa ni sahihi wakati mwingine pasipo kuomba hekima za Wazee matokeo yake Wizara zinaweza kuwa kama hostel za huko vyuoni tunakotoka.
 
Nngu007,
Mzee Kawawa aliwahi kusema ukifanya jambo Adui yako akakusifia ujue umekosea, lakini ukifanya adui yako akalalamika ujue uko sahihi! Toka Nape awe katibu mwenezi amekuwa akitukanwa kila aina ya matusi, kisa amekuwa mwiba kwa upinzani nchini!! Mbona kabla ya hapo alionekana shujaa?!!!! Mkimsifu kwa kila sifa, sasa anatukanwa mpaka matusi ya nguoni.... Siasa hizi za hovyo, siasa za kuamini ili mradi hakuungi mkono ni mshenzi hana maana, akigeuka leo kukuunga mkono anakuwa shujaa ghafla.... Huu ni upuuzi.

Ngoja Lowassa aipate hii message.......
 
Rais wetu JK mara nyingi matendo yake tofauti kabisa na matendo ameteua wakuu wa wilaya ambao wengi ni wanajeshi na askari wantafu anaposema wazee watoke wawaachie vijana anamanisha nini, kijana ni under 45 karibu robo tata ya wakuu wa wilaya alioteua ni over 45 ambao tayari si vijana

Hata mie nimejiuliza sana kuhusu hiyo kauli nikafikiri ni mie peke yangu ndio simuelewi.

Jamaa anachohubiri hadharani ni tofauti kabisa na anachokifanya akiwa kajifungia kwa ofisi yake.

Matokeo yake akichemka, mbio kuwasingizia Watendaji wake wanamuangusha. Kwa mfano anasema baadhi hakuwateua tena kwa tabia ya kuchelewa kutoa maamuzi, simuelewi hata kidogo wakati yeye mwenyewe issue ya Luhanjo, aliyekua katibu wizara ya madini, Mponda na Nkya. Mbona alichelewa kuchukua maamuzi mpaka mashinikizo yatoke bungeni.

Kwa kifupi anajisafisha tu lakini ukweli ni kwamba yeye binafsi anachangia sana kwa Wananchi kuichukia serikali yake maana yeye ndiye aliyeshika mpini.
 
JK, preach what you do. Juzi tu hapa umetoka kumwapisha Mwandosya, umri umekwenda,anaumwa, leo unawaambia wazee waachie ngazi! Kwani Mwandosya asingeweza kuwa mshauri bila uwaziri?

nafikiri ndo mana kampa wizara isyo na shughuli maalum. Mi ndo nilikua najiuliza shughuli zisizo maalum ni zipi? nae hizi mwezi wa 6 analeta bajeti? sasa hizo shughuli zisizo maalum zinahitaji bajeti? au ndo maeneo ya kuiba pesa za watz?
 
Colleagues,

Wachangiaji ni wengi topic hii. Kama ili limesemwa tayari basi wazo hili lionekane marudio (kwa mtizamo mwingine wazo hili lichukuliwe kama msisitizo). Niliwaza sana juu ya kauli za JK hasa aliposema Ma-DC na Ma-RC wasiwe mawakala wa watafuta U-rais. Hivi nini litakalozuia viongozi wetu hawa wasifanye hivyo? Wao ni wateule wa Rais, let's say hawa waliopo by the time JK anaondoko watahitaji wajijendekeze kwa yeyote mteule wa U-rais ili wateuliwe tena la sivyo wanatemwa na anayefuata (successor wa JK). Ikumbukwe naye alifanya hivyo (sina ushaidi wa kutosha) kwa wale ambao hawakuwa-supportive hawakuteuliwa naye. Mfumo uliopo sasa unawafanya viongozi hawa wajikombe kwa ngeli yoyote hile ili na wao waendelee kuwa wateule wa Rais. JK anajua hilo (na kama ndivyo basi ...)
 
Kama akina Shibuda ndo watoa Mada ktk Semina hizi elekezi, Unategemea kupata ma DC wa aina gani? Lawama hizi JK hawezi kukwepa kwa kuendelea kuteua watu wasio na sifa, kupeana vyeo kirafiki na upambe, na yeye kukosa uwezo wa kuwasimamia viongozi anao wateua kumeiondolea uhalali wa ccm kuendelea kuongoza.
 
je hana uhusianao na madc aliowateua wakina kirigini,mayenga na mbunge wake wa zamani wa chalinze maneno aliyempa udc kigoma? Mifano hii michache inatosha!! Usitake tusema mengi kwani nani asiyejua ukware wa huyu mkweree na jinsi anavyohonga vyeo kwa washikaji zake!!

edwin mtei muasisi wa cdm huku mkwewe aliyeoa binti yake bwana freeman mbowe akihakikisha anampa uenyekiti wa cdm,tundu lissu mbunge wa singida dada yake ni christina lissu mbunge viti maalumu cdm,rose kamili mke m kubwa wa dk slaa ni mbunge viti maalumu wa cdm,grace kiwelu ambaye ni mbunge wa viti maalumu ni mkwe wa mzee ndesamburo ambaye ni mjumbe wa kamati kuu ya cdm,mfadhili na mbunge wa moshi mjini huku binti yake wa kumzaa akiwa pia mbunge wa viti maalumu sasa wapi ambako hakuna vyeo vya kishikaji ?
 
It is high time Kikwete started walking his talk; anasema wazee wawapishe vijana ili wao wawe washauri lakini wakati huo huo anawateua wazee useless kabisa kuwa wakuu wa wilaya ; mfano ni Luteni mstaafu Yamungu huyu licha ya uzee pia ni mlevi na kitu anacholingia ni kwamba Kikwete ni rafiki yake!! Akumbuke pia kuwa ujana sio mara zote kuwa ishara ya kuweza kuwa mtendaji kuliko watu wa umri mkubwa; mifano ya kina Maige na Masha tunayo ingali hai!!
Naomba kuliweka sawa hili,kuhusu utendaji wa serikali bila kujali umri wa mtu ni vema tukaangalia mchango wa mtu katika ujenzi wa taifa kwani kuna vijana tunao lakini wanakosa busara uongozi na kuna wazee pia tunao wanakosa busara uongozi hivyo ni vema tukawapima kwa utendaji wao wenye busara uongozi bila kubagua kwani yatupasa kutambua kuna wazee wenye upeo mkubwa na wanahitaji mawazo yao kuwaachaia vijana wenye upeo kuweza fanikisha maendeleo ya wananchi
 
edwin mtei muasisi wa cdm huku mkwewe aliyeoa binti yake bwana freeman mbowe akihakikisha anampa uenyekiti wa cdm,tundu lissu mbunge wa singida dada yake ni christina lissu mbunge viti maalumu cdm,rose kamili mke m kubwa wa dk slaa ni mbunge viti maalumu wa cdm,grace kiwelu ambaye ni mbunge wa viti maalumu ni mkwe wa mzee ndesamburo ambaye ni mjumbe wa kamati kuu ya cdm,mfadhili na mbunge wa moshi mjini huku binti yake wa kumzaa akiwa pia mbunge wa viti maalumu sasa wapi ambako hakuna vyeo vya kishikaji ?

Hii ya chadema si ushikaji hii ni ufisadi wa hali ya juu. Halafu mitaani huko wanazuga watu kuwa wao waadilifu, hapo kuna uadilifu? Na hapo ndio hawajakamata madaraka ya nchi.

Nimesoma kisa cha Chacha Wangwe kwenye nyuzi mojawapo humu, na kwa kuisoma post hii inanifanya niamini ile nyuzi. Ngoja nikaisome tena kwa kina na nii kopi kabla haijayeyuka.
 
lucy fedelis oweny,mbunge wa viti maalumu mkoa wa kilimanjaro ni binti ama mtoto wa mzee ndesamburo huku mhongo ruhwanya mbunge wa viti maalumu kutoka kigoma wakiwa na undugu wa karibu sana na mhe zitto kabwekuna wengi tu wengine ni mademu wa viongozi wa juu ukiondoa mama mushumbuzi ambaye ni mchumba wa milele wa dr slaa ambaye amepewa nafasi ya kazi ndani ya cdm
 
Yeye ana miaka 60+. AWAPISHE VIJANA. Ni ufinyu wa mawazo kwamba tukiwa na vijana tu serikalini nchi yetu itasonga mbele. Kuwa na watu wa rika mbalimbali katika uongozi wa nchi ndipo tutakapokuwa na mafanikio. Mawazo haya ya Rais ni hatari kwa ustawi wa taifa letu.
 
hakuna jipya ni yale yale ya miaka nenda rudi mbona naona kama kila sector wastafuu wanaongezewa muda au kama sio hivyo basi wana pewa nyadhifa zingine ina maana hakuna walaamu wengi nje ya hawa wazee? sioni kama anajipya bali ni uhuni tu na kujaza na kuuza magazeti na kutumia vibaya raslimali zetu
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom