JK akabidhi majina ya wauza ‘unga’

Fitinamwiko

JF-Expert Member
Aug 13, 2012
4,803
1,416
KAMISHNA wa Tume ya Kudhibiti Dawa za Kulevya nchini, Godfrey Nzowa, amesema baada ya Rais Jakaya Kikwete kuwakabidhi majina ya watu wanaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya, kitengo chake kimewafuatilia watuhumiwa na kuwakamata baadhi yao.

Akizungumza na Tanzania Daima Jumapili, Kamishna Nzowa alisema miongoni mwa waliokamatwa ni wale waliotajwa katika mitandao ya kijamii hivi karibuni, ambapo walipelekwa mahakamani chini ya kiapo maalumu.

Nzowa alitoa kauli hiyo wakati akijibu maswali ya mwandishi wa gazeti hili aliyetaka kujua kama kitengo chake kimekwisha kujishughulisha kuyapata majina yaliyokuwa kwa Rais Kikwete na kuyafanyia kazi.

Aliwataja baadhi ya watu waliokamatwa kuanzia mwaka 2007 na kupelekwa mahakamani chini ya kiapo maalumu kuwa ni Ally Hatibu, Ayubu Kiboko na mwingine aliyemtaja kwa jina moja la Shikuba.

“Kiukweli ni wengi wanatajwa, nasi tunafanya kazi na wengine tumewafikisha mahakamani chini ya kiapo maalumu kwa kuwa tunakuwa hatuna ushahidi wa moja kwa moja dhidi yao,” alisema Nzowa.

Aliongeza kuwa mwaka 2011 walifanikiwa kumkamata msambazaji mkubwa wa dawa hizo duniani na kwamba baada ya kumpekua walimkuta akiwa na mifumo (formula) ya kuzuia dawa hizo zisionekane katika mashine.

Alisema vita ya kupambana na dawa za kulevya ni kubwa, inayohitaji watu waaminifu kwa kile alichoeleza kuwa hata mashine za kukaguliwa zinatumiwa na watu ambao wanaweza kuizima pindi wanapotaka kufanya mambo yao.

Nzowa alibainisha kuwa kuanzia mwaka 2007 hadi Julai mwaka huu wameshakamata dawa aina ya heroin zaidi ya kilo 1,000 na cocaine kilo zaidi ya 370.

Alisema dawa hizo zina athari kubwa kwa jamii kwa kile alichoeleza kiasi kinachoweza kumlewesha mtu na kumuathiri ni wastani wa heroin ya gramu 0.11.

Aliongeza kuwa kwa sasa ukamataji umekuwa wa kiwango cha juu nchini, hali inayofanya dawa hizo kuuzwa kwa gharama ya juu tofauti na mwaka 2008.

“Asilimia kubwa ya dawa hizi tunakamata usiku baada ya kupata taarifa kutoka kwa wasamaria wema na njia kuu ni katika bahari, watu wanatumia bandari bubu kufanikisha mipango haramu ya kuingiza dawa hizi,” alisema Nzowa.

Source: Tanzania Daima, Jumapili August 4, 2013

Maoni yangu:
Nani Boss Rais au Kamishina?
Kulikuwa na haja gani kupoteza pesa za walipa kodi kumlipa huyu kamishina anayesubiri kupewa majina na Rais?
 
Imekuwaje kaja front kwenye press ?Hapa kuna namna sasa wanaumbuka kaambiwa aende .Je wako viongozi wa Kanisa humo ? Majina makubwa ni hayo tu ?Polisi bwana
 
mara baada ya kukabidhiwa majina alipaswa pia akabidhiwe barua ya kufukuzwa kazi kwa kulala usingizi na kusubiria majina.
 
porojo.uongo.magumashi. awez kukabiz majina. watashikwa punde tu. wakuu wenyewe awashikwi.
madawa yenyewe yanalindwa na jeshi na polis pia.
 
bora zingekua poroja..jamaa limekaa na wenzie,ndo wakapata story ya kuja kucover madudu yao!tatizo hata kutunga uongo hawajui
 
  • Thanks
Reactions: kui
Hayo majina ni ya wale tu wanaojihusisha kwa kiasi sana kwa nn wasitajwe vigogo wa hiyo bizz
 
Ni nani anayesambaza pale KAWE UKWAMANI na UBUNGO MAZIWA? Vijana wanakwisha maeneo Yale na wengi wa wateja wa ukwamani wanatokea MIKOCHENI.

Taifa hili litamalizwa na hawa hawa kina NZOWA maana Kwa kupita madawa pale airport kama alivyo sema Yule punda wa HONG KONG basi idara yake imekuwa implicated sharti achunguze watendaji wake na yeye pia nahisi kama anatakiwa kuchunguzwa maana inasemekana kupata Kiel kitengo lazima uwe mtu wao....
 
Lol Kinje na Rizone ni wabaya Kwa hii biashara namfahamu Kinje kunzia miaka ya 1998 na miaka hiyo alikuwa akiishi pale Kjitonyama nyuma ya Science karibu na kanisa la KKKT Kijitonyama na mpaka miaka ya 2002 alikuwa akiishi pale Kwa sasa sifahamu kama bado anaishi pale maake alikuwa amepanga jumba lote,huyu jamaa ni the big Boss anajifanya anauza magari lakini sie wajanja tulikuwa tunafahamu whats going on!!!Sasa Kwa list ya DHAIFU hawa nao wamo yaani Rizwani ambaye ni mwanae na huyu Kinje ambaye ni mwana wa kile kibabu kileee
 
Hapa formula ni ileile "Huwezi kata tawi ulilokalia"

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Abra kadra imeanza!

Na wale waliokamatwa mtwara akiwemo mtoto wa Liyumba wako wapi
 
Kumekuwa na matumizi ya FBI kwa baadhi ya matukio yaliyotokea hapa nchini, naomba kama selikali hii inayodai yenyewe ni sikivu iwe na uthubutu wa kuwashirikisha FBI katika hili la madawa ya kulevya halafu kina nzowa wawe pembeni hapo nitaamini matokeo .. Na si huu upuuzi
 
  • Thanks
Reactions: kui
Tatizo letu ni katika mfumo..........watendaji wengi wanasubiri maelekezo ya namna ya kufanya kazi zao za kitaalamu kutoka kwa wanasiasa...

Haiingii akilini wakati kamishna anayeshugulika na udhibiti wa madawa ya kulevya hana orodha ya majina ya wahalifu hao wakati Rais anayo.

...au labda ni yeye alimpelekea Mh rais ili amuelekeze cha kufanya???..kama ni hivyo kwa kifupi ni kibogoyo.....
 
Huyu Nzowa yeye kila siku miaka yote kulalama tu hamna yeyote anayekamatwa zaidi ya mateja.

Kule mwananyamala, kinondoni unga unauzwa waziwazi Nzowa unashindwa hata kuduatilia hiyo chain
 
Na mapusher mengine ya kukamata kama Faizafoxy,Hamy-D,ZeMarcopolo,scamble,uncle Deo hizi dili za unga ndio zinawaweka mjini hawana kazi na mmoja anaitwa Radhia sweety woote hawa hawana tofauti na Iddi Azzan na ndio wanamuuzia wakatae nimwage zaidi
 
Hivi wote wanaokamatwa kila kukicha nyinyi hamuoni? Na hakuna aliyetangaza kuwa sasa basi hatukamati tena. Sijui huwa mnafikiri kinyumenyume?
 
you know wht? Zzm&comp you've done enough damage to this country, the people and everything in it!, when are you going to stop upuuzi wenu nyamafu nyinyi msio haya wala taswira ya haya!, hii danganya toto si mkakae na haw..ala zenu ndo mdanganyane!, mxxxxxx! Hizo akili zenyu hazina hata akili, you literally think everybody's jinga like you!, you sucked enough from this country, money, natural resources, brains of those who're committed and trully love tz and now you're turning to our youngters's physical strengh and causing others to disappear 'somewhere on the planet' oneni haya sometimes mxxxxxx1, yaone kwanza masura yamewapalama ka ------ ya mlevi, mxxxxxxx!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom