Synthesizer
JF-Expert Member
- Feb 15, 2010
- 11,143
- 18,772
Tunapoelekea mwisho wa uongozi wa JK, ni kipi ambacho Watanzania tutamkumbuka kutuachia (legacy)?
Niliwahi kumwandikia JK kwamba lengo la Nyerere kukubali upinzani uanze lilikuwa ni kwa maslahi ya Taifa. Nikashauri kwamba ajitahidi aukuze upinzani japo yeye ni kiongozi wa CCM. Nilisema hata pakiwa na ziara za viongozi wa nje ahakikishe anaweka kwenye ratiba voingozi wa upinzani, vyama vyenye uwakilishi mkubwa bungeni, wakutane na viongozi hao wa nje, awahusishe viongozi wa upinzani katika baadhi ya ziara zake za nje na hata kuwaalika Ikulu kila mara kwa majadiliano juu ya matatizo makubwa ya nchi - kama mgomo wa madaktari, thamani ya shilingi, umeme nk.
Nilisema ajitahidi angalau chama kimoja cha upinzani kitufikishe kama ilivyo Marekani kwa Democrats na Republicans. Nilisema akifanya hivi ataacha CCM na hicho chama cha upinzani vyote vikiwa strong kwa maslahi ya taifa, na yeye akaheshimika sana baada ya kumaliza uongozi wake, nchini na kimataifa.
Tofauti yake, akiwa kama Mkapa, raisi mstaafu na viongozi kama yeye, wakatukana vyama vya upinzani na viongozi wao, wanapaswa kukumbuka kwamba Tanzania pia inaweza kutokea tukawa na raisi na serikali kutoka chama cha upinzani. Wanafikiri watachukuliwaje na raisi waliyemtukana pamoja na chama chake kabla hajachukua madaraka? Hata kwa mtu asiye na hulka ya kisasi, kutoa heshima inayostahili kwa raisi mstaafu aliyetukana wewe na chama chako kabla hamjachukua nchi ni ngumu sana. Wanaweza kujikuta siku moja huko mbeleni hata escort ya polisi hawapati tena na wanafoleni barabarani kwenye traffic kama raia wengine.
Mwana CCM yeyote mwenye akili anapaswa kusikitika akiona watu wanafanya kampeni za kuua vyama vya upinzani nchini. Maslahi ya taifa ndilo lililokuwa lengo la Nyerere kukubali vyama vya upinzani, sasa kwa nini kuwe na harakati za kuua upinzani?
Na ndio maana mwanasiasa yeyote mwenye akili hatatumia matusi juu ya chama kingine.