JK aichangishia UDSM 1.4/- bilioni kujenga kituo

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
Rais Jakaya Kikwete amezindua harambee ya kuchangia ujenzi wa kituo cha wanafunzi cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), iliyofanikisha kupatikana kwa jumla ya Sh. 1,430,583,000.
Uzinduzi wa harambee hiyo ulifanyika Ikulu juzi usiku jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na watu mashuhuri wakiwemo Mabalozi Alonso Leinhardt (Marekani), Bjarne Sorensen (Denmark), Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Profesa Benno Ndulu, Mawaziri na wafanyabiashara.
Akizungumza wakati wa harambee, Rais Kikwete alisema: “Mimi ni mkereketwa wa elimu na ndio maana sikusita kukubali ombi la Profesa Mukandala (Rwekaza) aliponieleza mpango huu.”
Rais Kikwete ambaye aliahidi kuchangia Sh. milioni 10, alisema atakuwa balozi wa kuomba michango kwa marafiki zake na kwamba suala hilo ataliwasilisha kwenye serikali yake ili nayo ichangie.
Kadhalika, aliwasilisha ahadi za marafiki zake ambao waliahidi kuchangia Sh. bilioni moja.
Rais wa wahitimu wa UDSM ambaye pia ni Mwenyekiti wa kamati ya ujenzi wa kituo hicho, Waziri Mkuu Mstaafu, Jaji Joseph Warioba, alisema chuo hicho kwa sasa kinakabiliwa na tatizo kubwa la miundombinu zikiwemo nyumba za walimu, ofisi, madarasa na hosteli za wanafunzi.
Alisema ujenzi wa miundombinu hiyo hauwezi kufanikiwa kwa kuitegemea serikali pekee na kwamba mkakati uliopo ni kujenga utamaduni wa kushiriki ujenzi wa vyuo hususani kule walikosoma.
“Tumeshakaribia asilimia 20 ya gharama za ujenzi wa kituo hiki,” alisema.
Kwa upande wake, Makamu Mkuu wa chuo hicho, Profesa Rwekaza Mukandala, alisema gharama za ujenzi wa kituo hicho unakadiriwa kuwa Sh. bilioni 17.
Alifafanua kuwa kitakuwa na maeneo ya kupumzika wanafunzi, hosteli, sehemu za michezo, maktaba, huduma za vyakula na benki, ofisi za serikali ya wanafunzi na kituo cha intaneti.
Alisema kwa kuanzia, wafanyakazi chuoni hapo, wamechangia Sh. bilioni 1.2.
“Kituo hiki kinajengwa kama kumbukumbu ya miaka 50 ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambacho kilijengwa Oktoba, 1961 miezi michache kabla ya uhuru,” alisema Profesa Mukandala.
Katika harambee hiyo, Sh. milioni 64 zilikuwa fedha taslimu wakati ahadi ni Sh. 1,366,583,000.
CHANZO: NIPASHE
 
tutarajie nini kwa udsm!!je kutakua na mabadiliko makubwa??hasa upande wa miundo mbinu na vipaumbele vilivyotajwa endapo tu usimamizi wa pesa hiyo utakua mzuri!
 
tutarajie nini kwa udsm!!je kutakua na mabadiliko makubwa??hasa upande wa miundo mbinu na vipaumbele vilivyotajwa endapo tu usimamizi wa pesa hiyo utakua mzuri!

Mabadiliko yatakuwepo makubwa lakini ya kimiundombinu. Tunahitaji kuboresha si tu simiundombinu lakini mfumo mzima wa utoaji elimu kwa kuondoa vikwazo vyote vya kujifunza kama upatikanaji wa fedha za kujifunza na maktaba. JK amejitahidi
 
Mabadiliko yatakuwepo makubwa lakini ya kimiundombinu. Tunahitaji kuboresha si tu simiundombinu lakini mfumo mzima wa utoaji elimu kwa kuondoa vikwazo vyote vya kujifunza kama upatikanaji wa fedha za kujifunza na maktaba. JK amejitahidi
unajua jk ni kweli kaingia kuichangishia udsm ila angeangalia na mfumo wa bodi ya mokopo yeye kama msimamizi kwa kweli imekua kero kubwa sana may be angeomba maoni ya wanafunzi kwamba wanaona iweje mie nadhani yangesaidia sana katika kurekebisha kuliko kutegemea maoni ya upande mmoja tu ndio maana wanaoishia kuumia ni wanafunzi muhimu sana na wao kushirikishwa katika maamuzi ni sio wanafunzi kutoka vyuo vya serikali tu ijumuishe vyuo vyote!!!
 
Back
Top Bottom