Elections 2010 Jk aendelea kuvunja sheria ya uchaguzi

urasa

JF-Expert Member
Aug 12, 2010
434
2
Jamaa amechelewa kutua hapa kahama,ameanza kuhutbia saa kumi na mbili jioni hii na bado anaendelea hadi sasa wakati hap juzi cuf waliongeza dakika 10 tu polisi wakawatoa mbio,amekuja na msafara wa magari ya serikali kama kawaida yake akisahau yupo kwenye kampeni za chama
 
Anajua hawezi kushinda hivyo anaona bora avunje sheria tu. Hiyo inasaidia kujua na kuthibitisha yeye ni msanii tu
 
tendwa na lewis makame , wapo wapi? wamelala au ni sehemu ya hilo tatizo?
 
Hata katika soka ukiona timu inapokosa matumaini ya kushinda huanza kucheza rafu ili filimbi zikiwa nyingi waseme wanaonewa. CCM safari hii hawatoki, na JK kutokana na maradhi yake yaleee ujuwe yameshapanda kichwani ndiyo maana hajali na wapambe wanaogopa kumweleza ukweli. HUYO NDIYO KIHERE HERE NAMBARI WANI
 
Hivi hii inakuwaje mtu anavunja sheria hachukuliwi hatua?
Sina imani na vyombo vya dola vya tanzania kama vinatenda haki. badala ya kukamata wahalifu vinakamata raia wema na kuwabambikizia kesi za wahalifu
 
Ila Kama polisi wangekuja na virungu vyao na kumfukuzia mbali Rais wakati akihutubia mkutano ingekuwa hatari! Maasi!

Lakini hakuna sababu Lewis Makame ashindwe kukemea ukiukwaji wa sheria za uchaguzi.

Vile vile, sijajua ni kwa nini Jaji Mkuu hajathubutu kukemea kitendo cha Rais kusema kesi ya Mramba ni ndogo tu, na atashinda. Mahakama ni nguzo mojawapo ya serikali. Nguzo ya Utendaji ikivuruga sheria inabidi ikanywe. Mheshimiwa Ramadhani, timiza wajibu wako wa kikatiba. Taifa linasubiri lisikie utasemaje.
 
Nina wasiwasi kama Jaji Mkuu anaweza kuongea lolote. Mtu ambaye alishindwa kuthubutu kusimamia kanuni za ofisi yake katika kutoa uwakili na kuruhusu mtoto wa Rais kupewa uwakili bila kuzingatia misingi na taratibu za kutoa uwakili leo athubutu kumgusa mkubwa mwenyewe ambaye anashikilia mpini wa kula yake ya kila siku..!!..??

Ninachokifahamu ni kuwa, watakaa pale State House na kukubaliana kuwa ajifanye anapiga mkwara kwenye media kuwa wagombea wasiongolee kesi zilizoko mahakamani ili kutuliza wananchi na baada ya hapo arudi kwenda kukamua mvinyo huku akigonga Cheers na aliyempiga mkwara.
 
Hiyo ni ishara kuwa JK is becoming unpopular as days go on na anadhani kwa kuvunja sheria ataweza kupanda chati wakati ukweli ni kinyume chake. Wapinzani wanatumia huo upuuzi wake wa kuvunja sheria za uchaguzi kumning'iniza zaidi.

Hayo yote yanachangiwa na Jaji Makame na NEC yake kwa kutoa kauli za jumla-jumla kuhusu vyama kuvunja sheria za Uchaguzi. Ni matumaini yangu kuwa sasa NEC itamkemeka waziwazi mgombea huyo wa CCM na Chama chake.
 
Huwezi kujua kilicho tokea, yawezekana kashikwa ile issue akiwa angani na hivo kusubiri arudishe fahamu. Kama fahamu zimerejea muda umesha kwenda wafanyeje? Jua kwamba huyu mtu amesha tabiri kushindwa!
 
Back
Top Bottom