WIKI chache baada ya Rais Jakaya Kikwete kutoa agizo akitaka uzio wa viwanja vya michezo Jangwani ubomolewe, imebainika kuwa agizo hilo limeshindwa kutekelezeka kwa sababu eneo hilo limeuzwa kwa mwekezaji ambaye ni raia wa China.
Hivyo watendaji wa Halmashauri ya Ilala na Wizara ya Ardhi wanabanwa na masharti ya mkataba unaodaiwa kuingiwa baina yao na mwekezaji huyo.
Imebainika kuwa Rais Kikwete alitoa agizo hilo Aprili 3 mwaka huu baada ya kupewa taarifa potofu na hivyo kutoa amri ambayo haitekelezeki kisheria.
Akiweka jiwe la msingi la upanuzi wa barabara ya New Bagamoyo, eneo la Mwenge-Tegeta, Rais Kikwete aliagiza uzio huo ubomolewe lakini hadi jana hakuna bomoabomoa yoyote iliyokuwa imefanywa katika eneo hilo.
Chanzo chetu kutoka ndani ya halmashauri ya Ilala kilisema mkataba huo umempa mwekezaji huyo haki ya kujenga maghala mbalimbali ‘magodauni', kwa makubaliano kwamba yangeinufaisha pia halmashauri hiyo.
Ilibainishwa zaidi kuwa mkataba huo uliingiwa kibinafsi na baadhi ya viongozi wa Ilala kutokana na tamaa ya fedha huku wakishindwa kuzingatia kuwa eneo hilo ni maalum kwa ajili ya michezo.
Baadhi ya madiwani wamekuwa wakipiga kelele za mara kwa mara kuhusu uwanja huo wa michezo wa Jangwani lakini hakuna hatua zilizochukuliwa hadi sasa licha ya Rais Kikwete kutoa agizo lake.
"Ni vigumu kwa watendaji wa halmashauri hiyo kuvunja uzio huo kwa sababu wao ndio walioshiriki kuingia mkataba huo mbovu.
"Haya ndiyo mambo tunayopigia kelele kila wakati lakini hatusikilizwi maana halmashauri ina wataalam wa ardhi wa kutosha iweje wanashindwa kujua umuhimu wa viwanja vile?" kilihoji.
Kilisisitiza kuwa kutokana na Rais Kikwete kuwa ndiye mhimili mkuu wa dola basi ana jukumu la kuhakikisha maagizo anayoyatoa yanatekelezwa ipasavyo.
Rais Kikwete ametakiwa kuingia na kusimamia agizo hilo binafsi kwa kwenda na kuvunja uzio huo mwenyewe kwani sio rahisi kwa walioingia mkataba kusimamia agizo hilo kutokana na kulinda maslahi yao.
Hadi habari hii inaandikwa uzio wa mabati bado upo ndani ya viwanja hivyo huku wizara ikiitaka halmashauri ya Ilala ibomoe lakini majibu yanayotolewa na halmashauri hiyo ni kwamba wamezuiwa kufanya utekelezaji huo.