Kikwete abadilisha wakuu wa wilaya

Ilulu

Senior Member
Mar 22, 2008
161
31
*Atengua uteuzi wa DC Temeke

Na Elisante Kitulo
24 October 2009


RAIS Jakaya Kikwete amefanya mabadiliko madogo ya vituo vya kazi kwa baadhi ya wakuu wa Wilaya nchini ikiwa ni pamoja na kufanya uteuzi mpya wa mkuu wa wilaya mmoja.

Wakati huohuo, Rais ametengua uteuzi wa Bw. Said Mkumbo aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Temeke na kumhamishia katika Idara nyingine ya Serikali.

Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana na kusainiwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI)ilieleza kuwa Rais amemteua Bw. Anatory Choya kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mbulu ambapo uteuzi huo umeanza Oktoba 10 mwaka huu.

Rais pia amefanya mabadiliko madogo ya vituo vya wakuu wa wilaya ambapo Bw. Francis Isaack aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Mbulu sasa anahamia Wilaya ya Bunda na Bi. Chiku Gallawa amehamishiwa Wilaya ya Temeke akitokea Wilaya ya Bunda.

Bi. Gallawa amehamishiwa Wilaya ya Temeke kuziba nafasi inayoachwa wazi baada ya Rais kutengua uteuzi wa aliyekuwa Mkuu wa Wilaya hiyo Bw. Saidi Mkumbo.

Taarifa hiyo inaeleza kuwa kutokana na utenguzi huo, Rais ameagiza Bw.Mkumbo ahamishiwe katika Ofisi ya Waziri Mkuu. Hata hivyo taarifa hiyo haikueleza sababu za utenguzi huo.
 
Hivi haya mabadiliko ya kila wakati ya hawa wakuu wa wilaya hayana gharama? Kuna haja gani ya kuwabidilisha vituo kila kukicha?

Amandla........
 
Hivi haya mabadiliko ya kila wakati ya hawa wakuu wa wilaya hayana gharama? Kuna haja gani ya kuwabidilisha vituo kila kukicha?

Amandla........

labda kwa kufanya hivyo anaonekana anafanya kazi yake ya urais vyema; vinginevyo mtajuaje ana madaraka fulani?
 
swali langu moja tu kwa wale waliokuwa na ufahamu zaidi wa jinsi serikali yetu inavyooendeshwa.hivi kuna sheria inayomzuia raisi kumsimamisha mtu kazi bila kumuamishia kitengo kingine au ndio urafiki unafanya watu wawe wanaamishwa sehemu hii na kupelekwa nyingine? nataka kufahamu tu manake naona kila siku watu wanaamishwa sasa sijui ni kwanini kama mtu hajafanya kazi vizuri akapigwa chini tu au ni kitu gani kinamfanya raisi afikirie huyo mtu ataenda kufanya kazi kitengo kingine vizuri?
na hii njia kuzungurusha zungurusha watu wale wale ndio inafanya nchi hii isiendelee popote kwani imeshikwa na akili zile zile kila siku.
 
Hii move yote ni kisasi kwa Mkuu wa wilaya Temeke...mmesahau Temeke walimfanya nini mkuu siku juzi juzi hapa.

MJ
 
*Atengua uteuzi wa DC Temeke

Na Elisante Kitulo
24 October 2009

Taarifa hiyo inaeleza kuwa kutokana na utenguzi huo, Rais ameagiza Bw.Mkumbo ahamishiwe katika Ofisi ya Waziri Mkuu. Hata hivyo taarifa hiyo haikueleza sababu za utenguzi huo.

Wakazi wa Temeke walimtoa nishai bosi, kwa kumzuia barabarani akitokea Airport.
 
Kama sikosei chiku alikuwa nesi hapa dar, na sifa zake na ukaribu na jikoni zimekaa kimtindo... Hongera chiku, CCM inakulea vizuri!!
 
Wakazi wa Temeke walimtoa nishai bosi, kwa kumzuia barabarani akitokea Airport.

Sio kweli, huyu jamaa (Said Mkumbo) ni mgonjwa, hata siku Wakazi wa Temeke walipotaka kumzuia Rais alikuwa anaumwa na nafasi yake ilikuwa inakaimiwa na Bw. Rugimbana ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni.
 
Haya Mabadiliko madogo ya wakuu wa Wilaya nafikiri yaliwalenga zaidi Mkuu wa Wilaya ya Temeke Bwana Said Mkumbo na Mkuu wa Wilaya Mpya wa Mbulu Bwana Anatoly Choya.

Said Mkumbo amekuwa Mgonjwa kwa muda sasa,kutokana na ugonjwa wake amekuwa nje ya kituo cha kazi,na inaonekana Uongozi wa kata,Tarafa na hata serikali za mitaa Wilayani Temeke umekuwa unatoa malalamiko mara kwa mara Ofisi ya Tamisemi (Wizarani) kuhusu utendaji kazi wa Mkuu wa Wilaya hiyo.Itakumbukwa kuna wakati Madiwani kadhaa walitupiana maneno makali na ya dharau Ofisi kwa Bwana Mkumbo.

Rais Kikwete amemteua Bwana Anatoly Choya kwa mara ya pili kuwa Mkuu wa Wilaya.Bwana Choya alishawahi kuteuliwa mwezi April/2009 kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga,Lakini baadaye Rais alitengua Uteuzi huo baada ya kugundulika kuwa Bwana Choya alikuwa ana kesi mahakamani kwa kosa la kutoa Rushwa.Bwana Choya ambaye ni M/kiti wa CCM wa Wilaya ya Biharamulo pia aliwahi kuwa Mbunge wa Biharamulo mwaka 2000. Katika Uteuzi huu Mpya amepewa Ukuu wa Wilaya ya Mbulu Mkoani Manyara.
 
Sio kweli, huyu jamaa (Said Mkumbo) ni mgonjwa, hata siku Wakazi wa Temeke walipotaka kumzuia Rais alikuwa anaumwa na nafasi yake ilikuwa inakaimiwa na Bw. Rugimbana ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni.

Kweli kabisa mkuu,Mkumbo ni mgonjwa sana na kuna kipindi alipelekwa India kwa matibabu alivyorudi Bongo hali bado ikawa tete akapelekwa Aga Khan ambako alilazwa na hata siku tukio la Kipawa latokea jamaa bado alikuwa hospitali...Jamaa ni mgonjwa wakuu,mgonjwa sana tu
 
Hivi hawa wakuu wa wilaya si huwa wanateuliwa aidha toka uraiani (not public servant) au maofisini sasa anapoachishwa u-DC anapelekwa Wizarani - TAMISEMI huko kuna budget yake? kuna vacant post to fill? Nilidhani akiachishwa u-D.C anarudi kwenye kazi yake ya awali kama mkulima, mwanasiasa nk
 
Hivi haya mabadiliko ya kila wakati ya hawa wakuu wa wilaya hayana gharama? Kuna haja gani ya kuwabidilisha vituo kila kukicha?

Amandla........

Fundi Mchudo,
Your well intended off-the-cuff criticism proves one thing ( if it even needs proving) and that is, the President will never be able to satisfy everybody, which is no great revelation!

In some recent past JF discussions some members were incensed by the fact that the President didn’t get rid of Masha after he was associated with a string of highly publicized scandals involving the plans he was advocating for Mengi to mitigate his influence in the national political scene, and his interference in the National ID tendering process that was taken up by a Parliamentary committee, not to mention his ineffectiveness in dealing with the albino murders. Some still have a bone to pick with the President because of that.

Now the Prez has decided to make a minor shuffle to his administration. Someone had suggested that these recent changes were triggered by the fact that the Temeke DC is unwell (I am not sure whether that is true or not). Now we are at it again, heaven spare us all! We are ready to usher in the second coming of our never ending list of complaints. You are loudly wondering if the shuffling of the deck can be cost justified while, like many of us, I suspect you don’t even know whether these changes are necessary! Perhaps it can be argued, with some legitimacy, that the changes are driven by a strategic imperative that far outweighs any associated costs. Your job is to determine what that is before you complain.

One thing is clear, the Prez is in a no win situation: He is reviled by us for making changes and he is blamed big time if he does not make changes! I am not even sure if at your vantage point you are in a position to judge if the changes made are necessary or crucial before you begin to skin the Prez alive with criticism. Sometimes we have to put the national interest above self-interest and partisan politics and give the President the benefit of the doubt.
Don’t get me wrong, I am not trying to muzzle your voice or anybody else’s for that matter, nor do I claim to have the power to do so, but we need to demonstrate reasonableness in our criticism so that the powers that be would find the justification and motivation to factor our suggestions into the day-to-day running of the government.

Suffice it to say that being Presidency is a lonely and thankless job that comes with a lot of stress and pressure, and we definitely have to share some of the credit for making it even tougher than it otherwise ought to be. This also explains why the Prez may be forced to ignore the noises that we are making masquerading as constructive criticism”.

Kumaliziya, tuendeleye kukosowa lakini lazima tujiwekeage malengo badala ya kupayuka tu kila tukipata nafasi na keyboard.
 
Mnawapamba tu. Ma dc hawana kazi yoyote zaidi ya kuhakikisha sisi m inabaki madarakani kwa nguvu.

Hata wakitoka wote maendeleo yetu yatakuja kama kweli serikali imejiwekea mikakati mizuri tu. Sasa mbona wamekuwapo kwenye system ya nchi hii tangu uhuru na hakuna mabadiliko ya maana zaidi ya wizi wa pesa zetu tu?

Hata akiugua huyo said mkumbo mwaka mzima na wilaya ikabaki bila dc kama wanataka maendeleo yatakuwepo.

Shida ni kwamba sisi m wamewanywesha bangi ya kisiasa wa tz kiasi hawawezi kujiondoa kwenye bakuli ya umaskini wakifikiri short cut ni ma dc.

Mwisho ni kwamba huyu Saidi si yule aliyekuwa mwandishi wa habari wa ofisi ya waziri mkuu wakati wa BWM?
 
Kweli kabisa mkuu,Mkumbo ni mgonjwa sana na kuna kipindi alipelekwa India kwa matibabu alivyorudi Bongo hali bado ikawa tete akapelekwa Aga Khan ambako alilazwa na hata siku tukio la Kipawa latokea jamaa bado alikuwa hospitali...Jamaa ni mgonjwa wakuu,mgonjwa sana tu

Balantanda,endelea mbele kidogo.....Mr Mkumbo anaumwa nini hasa?
 
Back
Top Bottom