Elections 2010 JK aazime busara hii!!!!!

Inahitaji upeo mkubwa wa kutowasema wenzako vibaya hata kwenye vinyang'anyiro kama cha urais.

Uamuzi uwe wa wananchi na sio viongozi walio madarakani... Tujifunze kutoka demokrasi zilizoendelea ..kuwa na busara hata pale tunapoona kwamba hatujahukumiwa(judged) vilivyo kutokana na matendo yetu au sera zetu....na tuwape wananchi haki yao kuamua badala ya kuwatisha kwamba wakiamua kutoa ridhaa kwa wengine watakuwa wanaipeleka nchi kwenye uwagaji damu....
Tuchukue mifano ya majirani zetu...ukiondoa kenya,uganda na rwanda.. Zambia walimwondoa Kaunda hawakumswaga damu..malawi walimwondoa Muluzi hawakumwaga damu Tutambue kwamba hakuna mwenye hatimiliki ya kutawala isipokuwa wapiga kura.. Mzunguko wa demokrasia hautakamilika iwapo mawazo mapya ya uendeshaji nchi hayatapewa nafasi na MAADILI YA TAIFA KAMA HAKI ZA BINADAMU,UTAWALA BORA ZIKAZINGATIWA NA KILA CHAMA
 
Back
Top Bottom