JK aanza Kufunikwa!

JohnShaaban

JF-Expert Member
Aug 23, 2007
464
114
Mwalimu mkuu atimuliwa kazi kwa kusaini mkataba feki

2008-01-05 10:15:24
Na Francisca Jeremiah

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Abasi Kandoro, amemuagiza mkurugenzi wa halmashauri ya Kinondoni Bw. Noel Mahyenga kuwasimamisha kazi mara moja mwalimu mkuu wa shule ya msingi Makumbusho, afisa mtendaji wa kata hiyo, mratibu wa elimu wa kata hiyo pamoja na mwenyekiti wa kamati ya shule.

Hatua hiyo imefikia baada ya viongozi hao kuingia mkataba na kusaini hundi ya Sh. million 136, kati yao na mwekezaji mmoja ambaye jina lake halikufahamika, kwa makubaliano ya kujenga uzio wa shule hiyo utakaokuwa na maduka ya kufanya biashara kwa muda wa miaka 20, bila ya kupata kibali toka mamlaka husika.


Soma zaidi
Nahisi kama mwaka huu utakuwa mbaya kwa JK maana baadhi ya watendaji wake wameanza kumuonyesha jinsi gani anatakiwa kushughulikia issues kama BUZWAGI, BoT na nyingine ambazo zina utata. Una'act' promptly pale unapoona maslahi ya jamii yanachezewa!
 
huu ni uonevu.. iweje mwalimu afukuzwe kazi wakati wengine wanaundiwa tume!? Na kuna ubaya gani kama Mwalimu Mkuu anafuata mfano tu wa viongozi wa ngazi za juu? Tangu lini kusaini mikataba mibovu ya "uwekezaji" ni kosa?
 
Kitu cha kuona hapa ni kuwa ni rahisi kumfukuza kazi mwalimu lakini "vingunge" wanaohujumu uchumi kwa kiwango kikubwa zaidi wanaachiwa na kuundiwa tume mpaka watu wanasahau.

Baadaye vingunge hao hao wanakuwa marais (read IPTL) halafu tunawategemea watabadilisha kitu.
 
kosa ni kosa jamani sio kwa sababu vingunge hawakushughulikiwa na yeye(mwalimu) asishughulikiwe,lazima awajibike kama kuna kosa kafanya,n kwa nini maeneo ya shule wanajenga maduka? wanahitaji kupanda miti pawe na hewa nzuri na mazingira safi sio maduka ya kuongeza traffic na uchafu na makelele
 
Bomoa uzio, mamalishe, kituo cha mafuta, gorofa, hotel! bomoa tu tutajenga kesho.
 
Msilaumu...Mbona CITY council wamejenga uzio na maduka shule ya UHURU mchanganyiko/CITY HIGH SCHOOL?..binafsi siungi mkono shule kugeuzwa Shopping Centers...its should remain Educational Centers...
Kandoro kumwadhibu Mkuu wa Shule si kwajili ya mradi, bali kwajili ya INVESTOR hajulikani au wao wamekosa 10% yao ktk huo mradi...BONGO UFISADI KWENDA MBELE...
 
masikini weee huyu mwalimu mkuu waweza kuta labda hana hata kadi ya ccm,else angemezewa..au kuundiwa tume au kupewa shule nyingine as procedure za kichama pindi ufisadi wako ukishtukiwa..as hana tofauti na karamagi kabsaaaa lakini si mwaona mkuu bado anapeta???
 
Hapana kumbe hamjui huyu ni JK anachemka kuifanya kazi ial kamwagiza mkuu wa mkoa au ?????????????????????????????
 
huu ni uonevu.. iweje mwalimu afukuzwe kazi wakati wengine wanaundiwa tume!? Na kuna ubaya gani kama Mwalimu Mkuu anafuata mfano tu wa viongozi wa ngazi za juu? Tangu lini kusaini mikataba mibovu ya "uwekezaji" ni kosa?

Nakubaliana na wewe, ni uonevu mkubwa!! Hao Siyo wawekezaji? lol!
Angalau iundwe tume basi. Bajeti ya kutosha (kama TZS 300 milioni hivi) itengwe, ifanye kazi yake vizuri.

Teh! Teh! Teh!
 
Hii inafanana na message iliyoko kwenye katuni hii ya mchoraji Said Michael.
akatunisaid2.jpg
 
Kaonewa? sijui....kitu kimoja ninachojua ni kwamba zamani corruption ilikuwa almost non existent kwenye primary schools kwa sababu kulikuwa hakuna pesa.Pesa zote zilikuwa halmashauri.
Halmashauri ndio zilikuwa responsible kununua kila kitu.
Issue kama hii ya ujenzi wa ukuta wakati huo,ni halmashauri ndio ingeamua na hapo shuleni wangeona tu ukuta unajengwa.
Lakini sikuhizi pesa za vitabu,ukarabati wa majengo na nk zinapelekwa moja kwa moja kwenye shule zinazohusika,na walimu wakuu wanazipiga kisawasawa!Kuanzia kwenye pesa za vitabu.Kuna wengine walishafungwa.
Kwangu mimi corruption ni corruption tu.Kwa hawa walimu,hicho ndio kiwango cha juu wanachoweza kuiba na wanaiba sana tu,ina maana hata ingekuwa ni bilioni or so,wangeiba.HAo wanaoiba mabilioni ni kwa sababu ndio pesa zilizo mbele yao.
Ninacholaani mimi,ni pale PCB wanapoenda kutumia resources kubwa tu kumkamata hakimu anayehongwa shs laki tatu au tano na kesho yake kuisoma kwenye gazeti-front page,wakati haohao wanasema mkataba wa Richmond ni swaaafi,lakini huo ndio ulimwangusha Lowassa NEC na bado unazua mjadala Bungeni na kwingineko.
Hapo tu!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom