Jizuie kupiga

mutisya mutambu

JF-Expert Member
Nov 21, 2010
208
82
MAMBO vipi mtu wangu, mpango mzima vipi, vipi weekend, ‘ishu’ zinaendaje? Kuna jipya gani, mambo tambarare au ndo kila kukicha afadhali ya jana.

Namshukuru Mungu mambo si mabaya, Mungu anasaidia maisha yanaendelea, nashukuru kwa kile ninachokipata, na sitachoka kumuomba yeye kwa kuwa naamini kwamba, bila yeye mimi si kitu, mapenzi yake yatimizwe.

Nawakumbusha vijana mkumbuke kujilinda ili muendelee kuishi. Nimewahi kuwaeleza vijana wajizuie kupiga, wakijifanya gonga gonga watakuzika, wanakusahau.

Hata kama una salio la kutosha jizuie kupiga, usione noma kutuma SMS, acha sifa za kijinga kujifanya kijogoo wakati unajimaliza, acha kujiangamiza.

Zitunzeni simu zenu , ni muhimu kwa maisha yenu na Tanzania kwa ujumla, msipende kupiga piga, gharama yake ni kubwa kwenu na kwa taifa hili.

Kama ikibidi upige hakikisha simu yako iko kwenye kipochi, jifanye dereva wa pikipiki anayeheshimu sheria za usalama barabarani, haendeshi pikipiki bila helmeti ili hata akipata ajali asiumie kichwani.

Ikibidi kupiga kumbuka usalama wa maisha yako, usipige nanihii kwenda nanihii, ni hatari, unashauriwa kutopiga ule mtandao unaoaminika kuwa ni wa gharama nafuu, inaweza kuharibu kabisa mfumo wa mawasiliano ya simu yako.

Naamini simu yako inafanya kazi vizuri na una hamu angalau ya kubeep, hii nayo ni hatari, wengine ukibeep tu wanapokea, hawana longolongo, wanasema wapo kibiashara zaidi.

Kutokupiga si ujinga, jambo la msingi si kupiga ila unachokiongea, na kumbuka kwamba, jambo la msingi ni mawasiliano, ukijali ufahari hiyo ni juu yako, simu ni simu tu, madhumuni yake yanafanana.

Usidanganyike na simu kuwa eti ina kamera au double-skrini. Hizo ni mbwembwe tu. Kuna simu nyingi sana feki siku hizi zinauzwa zimevishwa vifuniko vipya, usidanganyike mwanangu, usikimbilie samaki wabichi bila kuuliza wamevuliwa wapi, bila shaka ‘umenisoma’, nawasilisha


source: Habari leo,24 nov,2010,basil msongo :A S 101:
 
Back
Top Bottom