Jiunge tanzanialifeclub sasa!

peter tumaini

JF-Expert Member
Feb 3, 2012
573
94
SALAAMS WANABODI!

Napenda kuwafahamisha kuwa tumeanzisha huduma ya kupata vitu mbali mbali bila kuathiri shughuli zako na muda wako.

Huduma unazoweza kupata ni zifuatazo kwa sasa;kusajili biashara yako,kampuni,kupata ofisi eneo lolote unalohitaji Tanzania,kupanga nyumba,kununua nyumba,kununua kiwanja na kuuza na hata vitu mbali mbali,kupata birth certificate,kumtafutia chuo au shule inayostahili.

Baadhi ya huduma gharama zake ziko fixed hivyo utachotoa ni commission kwetu tu kwa makubaliano maalum, hii itaokoa muda wako na kuepusha utapeli.

Kama una kiwanja unauza,nyumba unapangisha,una vifaa unauza leta taarifa kwetu na jukumu letu ni kukutanisha na mteja sisi tutachukua commission baada ya biashara kukamilika.

Hii ni mwanzo tunaanda Business yard kwa ajili ya watu kuleta bidhaa zao kuuza na watu kuja kununua.

Wasiliana nasi kwa e-mail hii;tanzanialifeclub@gmail.com.
 
mkuu ungeweka na ghalama kabisa ili tuangalie. mfano kusaidia kusajili kampuni ghalama zake na kazalika na hatua mnazo saidia
 
Mkuu nimekusoma ila mlolongo utakuwa mrefu sana na utachosha kusoma.

Mfano, pale Brela gharama za kampuni kusajili zinategemea mtaji wake(capital),hivyo kwa Brela ukiwa na Memorandum yako iliyosainiwa na mwana sheria gharama ya kusajili kwa Kampuni ya mtaji wa kuanzia Tsh mil.30 na kuendelea haizidi laki tano.

Kwetu tunapata commission ndogo ya paper work na time yetu haitazidi laki moja mkuu. Ni mfano.
 
Mkuu nawapongeza sana kwa hii innovative idea hasa katika changamoto hii ya ukosefu wa ajira. Advise yangu kwenu ni kuwa: business mnauoifanya inahitaji uaminifu na uadilifu wa hali ya juu hivyo basi mafanikio yenu yatategemea sana uaminifu wenu katika kufanikisha kazi mtakazopewa na wateja. Vilevile, utii wa sheria msije mkampa mteja document za kuchakachukua kama bith certificate
 
Huu ni udalali tu na ufisadi tu! Mi nashauri acha watz watumie muda wao kuchacharika na kujifunza zaidi ya kuwaongezea gharama za maisha kwa kuwataka wawalipe Commission. Eti usajili wa kampuni? Jamani!!!!!!!!!!!!!
 
SALAAMS WANABODI!

Napenda kuwafahamisha kuwa tumeanzisha huduma ya kupata vitu mbali mbali bila kuathiri shughuli zako na muda wako.

Huduma unazoweza kupata ni zifuatazo kwa sasa;kusajili biashara yako,kampuni,kupata ofisi eneo lolote unalohitaji Tanzania,kupanga nyumba,kununua nyumba,kununua kiwanja na kuuza na hata vitu mbali mbali,kupata birth certificate,kumtafutia chuo au shule inayostahili.

Baadhi ya huduma gharama zake ziko fixed hivyo utachotoa ni commission kwetu tu kwa makubaliano maalum, hii itaokoa muda wako na kuepusha utapeli.

Kama una kiwanja unauza,nyumba unapangisha,una vifaa unauza leta taarifa kwetu na jukumu letu ni kukutanisha na mteja sisi tutachukua commission baada ya biashara kukamilika.

Hii ni mwanzo tunaanda Business yard kwa ajili ya watu kuleta bidhaa zao kuuza na watu kuja kununua.

Wasiliana nasi kwa e-mail hii;tanzanialifeclub@gmail.com.

Hapo bold sujaelewa unapata birth certificate kutoka wapi?
 
Usikatishwe tamaa na hawa ma "toy soldiers" songa mbele kaka, hii huduma yako wanatoa pia Majembe Auction Mart mimi napelekaga bidhaa zangu kuziuza wanachukua 10% ya bei ya kuuzia, wana yard yao mwenge njia ya kwenda cocacola.Haya ndo mambo tunayotaka kuyasikia humu ndani.
 
Mkuu nawapongeza sana kwa hii innovative idea hasa katika changamoto hii ya ukosefu wa ajira. Advise yangu kwenu ni kuwa: business mnauoifanya inahitaji uaminifu na uadilifu wa hali ya juu hivyo basi mafanikio yenu yatategemea sana uaminifu wenu katika kufanikisha kazi mtakazopewa na wateja. Vilevile, utii wa sheria msije mkampa mteja document za kuchakachukua kama bith certificate

Aksante mkuu kwa ushauri.Pia mkuu hatuwezi kuongozwa na pupa pamoja na tamaa. Tuna uaminifu mkubwa na pia ni mwiko kwetu kutoa vitu feki tunaamini utawala wa sheria and we cant abuse the law.
 
Usikatishwe tamaa na hawa ma "toy soldiers" songa mbele kaka, hii huduma yako wanatoa pia Majembe Auction Mart mimi napelekaga bidhaa zangu kuziuza wanachukua 10% ya bei ya kuuzia, wana yard yao mwenge njia ya kwenda cocacola.Haya ndo mambo tunayotaka kuyasikia humu ndani.

Aksante mkuu,next time give me the business.
 
Hapo bold sujaelewa unapata birth certificate kutoka wapi?

Mkuu birth certificate zinatolewa RITA sisi kazi yetu ni kukusaidia kufanya taratibu za kuipata bila kuathiri mda wako na kazi yako unayofanya, badala ya wewe kwenda kupanga foleni tutapanga sisi kwa niaba yako.
 
Huu ni udalali tu na ufisadi tu! Mi nashauri acha watz watumie muda wao kuchacharika na kujifunza zaidi ya kuwaongezea gharama za maisha kwa kuwataka wawalipe Commission. Eti usajili wa kampuni? Jamani!!!!!!!!!!!!!

Mkuu usiwe hivyo hata waliotangulia kimaendeleo wana makampuni ya udalali pia sio dhambi kwa TZ kuwepo.Pia tunakusaidia kuokoa muda wako ili uendelee kuchakarika na maisha.
Fikiria mtu atoke Sumbawanga aje Dar kusajili kampuni,gharama atakazotumia na mda wake. wakati anaweza tuma documents kwetu tukafanya kwa niaba yake huku yeye akiendelea kuchakarika huko Sumbawanga.
Fikiria zaidi usipende kuponda tu mkuu kila kitu.
 
Nahitaji birth certificates za wanangu! Ni-pm au call 0754 75 45 93 nikuungishe. Big up mkuu.
 
Mmefanya jambo la maana mtatusaidia kweli kuokoa muda kama mtakuwa serious na kazi zenu. Vp Kama nahitaji mchumba mnaweza kunitaftia jamani? Commission nitalipa baada ya ndoa ila naomba isiwe kubwa.
 
Teh teh TEH TEH,mkuu hiyo ni too personal,hiyo services haipo.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom