Jitihada za JK si "SIFURI"

mwanatown

Member
Jun 14, 2010
9
0
*
Nimesoma maoni ya mwenzetu aliyo orodhesha Jitihada za Mh Rais. Sijui ndugu yetu hoja zake amezipataje lakini mimi nikaona nifuatilie hii suala na nimepata majibu yafuatayo,

1. Mikopo kwa wajasiliamali kupitia mabilioni ya JK = 0
Mi nimefuatilia hii issue na nikagundua kwamba; Mikopo iliyotolewa kwa wanachama wa vikundi vya ushirika imeongezeka kutoka shilingi bilioni 65.7 mwezi Juni 2005 hadi shilingi bilioni 380 mwezi Mei 2009 sawa na ongezeko la asilimia 478.0

2. Kupunguza ukubwa wa Serikali kwa kuunganisha Wizara na Idara ili kuleta ufanisi = 0
3. Kufanya Kilimo chetu kiwe endelevu kupitia umwagiliaji = 0

Ukifuatilia na issue hii kwa makini utakuta kwamba uzalishaji wa mazao ya chakula umeongezeka kutoka tani millioni 17.9 mwaka 2004 hadi tani millioni 21.3 mwaka 2009; Haya si maendeleo?

4. Kutoa ruzuku ya pembejeo ili kuboresha kilimo = 0
Ukweli ni kwamba Ruzuku ya pembejeo kwa mfumo wa vocha imelenga kuwanufaisha jumla ya wakulima 1,500,000 ikilinganishwa na wakulima 737,000 mwaka 2008/2009. Haaaabari ndo hiyoo!!!

5. Kumleta Maximo kwa gharama kubwa ili kuinua soka la Bongo = 0

Tusisahau kwamba timu ya Taifa stars ilikuaga kimeo kupitiliza, tangu aje Maximo angalau tumishinda mechi 24 za kimataifa na wamepanda kwenye chati ya FIFA kutoka timu ya 167 hadi kufikia 108.

6. Kuileta Real Madrid = 0
Real Madrid na Brazil ipi bora kwani? Nchi nyingine gani hapa Afrika Mashariki imefanikiwa kuleta wachezaji kama Drogba, Kaka, Ronabinho na Deof katika kipindi cha miaka mitano?
7. Kushawishi watanzania waliopo ughaibuni kurejea ili wawekeze nyumbani = 0
Yet; kwenye orodha ya mafanikio;
Kushawishi baadhi ya watanzania ughaibuni kurejea nyumbani ili kushika nafasi nyeti akiwemo Tido Mhando pale TBC nk. –sasa which is which hajafanikiwa hata kidogo au amefanikiwa?

kama kweli jitihada zake zingekuwa 0, hata huyo Tito angerudi? Na wengine kibao wapo!

8. Kuwasaidia wachimbaji wadogo wa madini = 0
Kumeongezeka kwa ajira katika Uchimbaji wa Madini kutoka wafanyakazi 7,000 mpaka 13,000. Yaani watu zaidi ya 6000 wamepata ajira na wao wapate vijisenti kidogo

9. Kuweka mfumo mzuri wa wazawa kunufaika kutokana madini yetu sawa na wawekezaji = 0

10. Kuileta Brazil ili kutangaza Tanzannia ikiwemo utalii wetu pia kupata kafaida kidogo = 0
Match ya Brazil Vs Tanzania imerushwa live katika nchi 160 duniani! Unahisi utalii utakuwa imeinuka kwa kiasi gani hapo? Tumeweka nchi yetu kwenye ramani ya dunia .
11. kuitangaza Tz kwa safari zake kibao za nje ya nchi hasa USA= 0
Watalii wanaoongoza kuja Tanzania kwa sasa ni kutoka Marekani, Wanakuja na Dola zao!
12. Kuleta mkutano wa kimataifa wa Lionel Sullivan hapa Bongo ili kutangaza wajasiliamali wetu = 0
13. Kuanzisha vituo vya kukodisha matrekta na kuleta matrekta = 0
Mpaka sasa kuna matrekta makubwa
Mpaka sasa kuna matrekta makubwa 472 na madogo 495 na majembe ya kukokotwa na wanyamakazi 62,194 yameingizwa bongo na makampuni na watu binafsi kati ya mwaka 2008 – 2009. –Vituo sasa vinatushinda wananchi kuanzisha wenyewe?

14. Kujenga madarasa =0
Yani ukicheki hesabu za fasta fasta tu toka 2006 – 2009 shule za msingi zimeongezeka kutoka 14,70 hadi kufikia 15,727. Nadhani katika hizo shule madarasa hayatakosekana au vipi?

15. Kujenga zahanati = 0
Huyu jamaa sijui anatoa wapi mahesabu yake, mi nimedadisi na kuperuzi idadi ya zahanati zimeongezeka kutoka 3,292 mwaka 2005 hadi 4,559 mwaka 2010.

16. Kuongeza ajira za waalimu na kuboresha maslahi yao = 0
Kwenye shule za private (my mummy my daddy) na za kiserikali (St. Kanumba) idadi ya walimu (Maticha) imeongezeka kutoka 10413 mwaka 2005 hadi 15368 mwaka 2009

17. Kuongeza mishahara ya watumishi wa umma =0

Katika kipindi cha miaka mitano ze goverment imeweza kupandisha vyeo watumishi 140,797 waliokua wamelundikana katika cheo kimoja for long time kitambo, pamoja na upandishaji huo wa vyeo na mishiko pia imeongezeka

18. Kupunguza matukio ya uhalifu = 0

Kwani hii ni kazi ya JK au ya Kova tunayemsifia kila siku? Kwahiyo na huyo ni ziro????????

19. Kuwachukulia hatua wote watakaojisisha na ufisadi = 1x 0
Kwani Sasa JK ni rais wa Jamhuri wa Tanzania au jaji mkuu? Lawama zingine bwana!
20. Kupunguza kero za foleni = 0
Suala ya foleni sasa naona ni juu ya ongezeko ya magari kwa jinsi watu tulivyokuwa juu zaidi! Kwa sababu traffic wamezidi kumwagwa na bararabara zimeongezeka kama vile barabara ya msimbazi mpaka ubungo maziwa, mwenge- tegeta na kadhalika.tuache basi kununua magari
21. Kupunguza ajali za barabarani = 0
22. Kupunuza foleni kwa utaratibu wa njia tatu = 0
Barabara zenye hali nzuri zimeongezeka kutoka kilomita 6000 mwaka 2005 hadi kilomita 29,500 mwaka 2009.
23. Kupunguza utegemezi wa wahisani kwenye bajeti ya Serikali = 0
Mapato ya ndani ya serikali yameongezeka kutoka shillingi billioni 1,951.3 mwaka 2005/06 hadi shilliingi bilioni 5,096.0 mwaka 2009/10, Na kwa hivyo angalau tunapunguza utegemezi wa wahisani wa nje.
24. kupunguza mfumuko wa bei = 0.
As a matter of fact mfumuko wa bei za vyakula umeshuka kutoka asilimia 18.1 hadi 9.6 machi 2010 na naamini utaendelea kuteremka.

Tatizo la wabongo tunapenda tu kulaumu bila facts, hizi ni takwimu nilizo out source fasta fasta kwa muda mchache tu. Mdau stay tuned kwa part II ambapo ntamalizia kukupatia facts za ndugu yetu huyu…ze saga continues!!!

TAKWIMU HAZIDANGANYI! JK KAKAMUA!!!!!!!!!
 
1. Mikopo kwa wajasiliamali kupitia mabilioni ya JK = 0
Mi nimefuatilia hii issue na nikagundua kwamba; Mikopo iliyotolewa kwa wanachama wa vikundi vya ushirika imeongezeka kutoka shilingi bilioni 65.7 mwezi Juni 2005 hadi shilingi bilioni 380 mwezi Mei 2009 sawa na ongezeko la asilimia 478.0

Mimi siye huyo mtu unayemsema ila naona unaleta propaganda zisizo na mshiko, ebu sema ukweli hiyo nyongeza imetokana na mabillioni ya JK au wadau wengine? Kumbuka kuna FINCA, saccos karibu zote zinakopa CRDB etc. Unatakia ulete data zinazoonyesha hiyo nyongeza imetoka wapi. FYI: Kikwete mwenyewe ameshakiri kuwa mabilioni yake yaliliwa na wajanja wachache.

2. Kupunguza ukubwa wa Serikali kwa kuunganisha Wizara na Idara ili kuleta ufanisi = 0
3. Kufanya Kilimo chetu kiwe endelevu kupitia umwagiliaji = 0

Ukifuatilia na issue hii kwa makini utakuta kwamba uzalishaji wa mazao ya chakula umeongezeka kutoka tani millioni 17.9 mwaka 2004 hadi tani millioni 21.3 mwaka 2009; Haya si maendeleo?

Come on look this katika miaka 6 uzalishaji wa mazao ya chakula umeongezeka kwa tani 3.4million tu. Sasa jiulize mahitaji ya chakula yameongezeka kwa kiasi gani? idadi ya watu imeongezeka kwa kiasi gani? mshikaji achana na hizi cheap propaganda. Hii ni negative growth tena siyo zero ndugu yangu.
 
17. Kuongeza mishahara ya watumishi wa umma =0

Katika kipindi cha miaka mitano ze goverment imeweza kupandisha vyeo watumishi 140,797 waliokua wamelundikana katika cheo kimoja for long time kitambo, pamoja na upandishaji huo wa vyeo na mishiko pia imeongezeka

Wafanyakazi walipandishwa vyeo na madaraja baada ya Mkapa kuunda Tume ya Maboresho ya Serikali za Mitaa ambayo Kikwete ameiua licha ya kutokamilisha kazi yake. Nikichukulia mfano walimu waliokuwa kazini kipindi Kikwete anaingia madarakani hawajapandishwa vyeo mpaka leo. Kuna walimu wa Sekondari kibao wanaolipwa TGTS C1 (wenye diploma za ualimu) wamebakia katika mshahara huo licha ya walimu wapya wenye elimu hiyo hiyo and no experience kuajiriwa kwa misharaha ya juu zaidi. You can imagine ni kwa kiasi gani unamvinja moyo mwalimu aliyefanya kazi kwa miaka 6 au 7 anazidiwa mshahara na mwajiriwa mpya (first appointment) wakati elimu yao wote ni diploma na hakuna ziada tena walikuwa wanafunzi wao miaka 2 au 3 iliyopita.
 
23. Kupunguza utegemezi wa wahisani kwenye bajeti ya Serikali = 0
Mapato ya ndani ya serikali yameongezeka kutoka shillingi billioni 1,951.3 mwaka 2005/06 hadi shilliingi bilioni 5,096.0 mwaka 2009/10, Na kwa hivyo angalau tunapunguza utegemezi wa wahisani wa nje.
24. kupunguza mfumuko wa bei = 0.
As a matter of fact mfumuko wa bei za vyakula umeshuka kutoka asilimia 18.1 hadi 9.6 machi 2010 na naamini utaendelea kuteremka.

Tatizo la wabongo tunapenda tu kulaumu bila facts, hizi ni takwimu nilizo out source fasta fasta kwa muda mchache tu. Mdau stay tuned kwa part II ambapo ntamalizia kukupatia facts za ndugu yetu huyu…ze saga continues!!!

Hapa nazira kusema kabisa! kukopa Stanbic bank kwa ajili ya recurent budget ndiyo kupunguza utegemezi? mzee ni afadhali mara 100 kukopa nje kuliko ndani tena kwenye commercial banks.

Mfumuko wa bei! mwe!
 
Huyu ndugu yetu anahitaji darasa.....corporate banking rates unaweza linagnisha na misaada ya wafadhili amabyo almost haina interest zaidi ya political pushes?....na zitaibwa zaidi maana Stanbic hawana uwezpo wa kuibana serikali kama wafadhili na wala haitajishughulisha na vipi pesa imetumika kama ilivyo kwa wafadhili
 
Kila shetani na mbuyu wake....hata Hiltler pamoja na mauza uza yote he had many individuals ready to die for him.
Kwa namna ya pekee kabisa kipindi cha leo kila mtu mawazo yake yanapaswa kupewa nafasi, ili mradi havunji sheria. Kwa mtazamo wangu mimi hajanishawishi kama he has performed this time around ila kaharibu big time.
 
Back
Top Bottom