Jirani sio mstaarabu

Duh! Uswahili mzigo. Huyo wala usihangaike nae, atahama soon manake wa hivyo kila mwaka anahama nyumba!
Ila siku moja ukitoka kazini ingia home kwako, weka mziki full blast halafu funga nyumba uende ukajirushe na wewe utumie hela ikuzoee. Kalale hotel u-relax kidogo. Urudi kesho yake mchana. Atatia akili labda.
 
hivi kumbe na mie natesa majirani???

Tena mie nafanya na mazoezi ya vocal
ngoja niache hii tabia, sikujua kama ni tabia mbaya.
 
tafuta kiwanja jikaze kila mwezi peleka tofali
ukiona zimefika 2000 nunua kokoto na mchanga, cement, nondo tafuta fundi weka msingi
tumejenga kwa style hiyo hadi nyumba ikaisha
utapanga hadi lini?
 
Miaka minne unapanga?

mungu kamleta huyu akusumbue ili ujenge

shukuru kwa kweli........ingekuwa full amani usingeshtuka

wenzio woote walioteseka na nyumba za kupanga
sasa wamejenga

Mkuu kujenga sio sababu, kuna watu wako kwenye nyumba zao na wanakerwa na majirani zao kwa staili hiyo.... dawa hapo ni kununua mziki mnene na kusongesha kama yeye anavyofanya, mwenyewe atatafuta suluhu
 
Hahahahahaha hiyo na mwenyewe itamkera ati

Sent from my BlackBerry 9100 using JamiiForums
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom