Jinsi ya kutunza uso

Michael Amon

JF-Expert Member
Dec 22, 2008
8,775
3,610
daily-soaps-1.jpg


Uso ni sehemu ya kuonyesha uhalisia kwa mwanamke na unapotaka kujua ni jinsi gani mwanadada au mwanamke anapenda urembo basi utamwangalia usoni.


Kwa mtazamo huo utaona yule mpenda urembo akiwa amepaka baadhi ya vipodozi usoni kwa mfano:- Poda, Lip-Stick, Wanja n.k na utagundua kwamba niliyekutana naye ni mmoja kati ya wanawake wanaopenda urembo.


Leo imekuletea mada ya jinsi unavyoweza kusafisha uso wako na ili uelewe hilo fuata haya yafuatayo:-


a)Penda kuosha uso wako kwa maji safi na salama na ili kujiepusha na mlipuko wa maradhi yatokanayo na maji.


b)Kama uso wako wa mafuta basi tumia maji yenye uvugu vugu, ili kupunguza mafuta usoni mwako na ili kuuwezesha uso kuwa mkavu na kama unasura isiyo kavu, basi nakushauri utumie maji yoyote unayopenda kama ni vugu vugu au ya kawaida.


c)Tumia sabubi yoyote nzuri uitumiayo kunawia uso wako siku zote, ili kuiboresha ngozi ya suo wako.


d)Ila penda kutumia sabuni zisizo kali pindi usafishapo uso wako na itakuepusha na baadhi ya matatizo ambayo wanawake wengi huyapata kwa utumiaji wa sabuni kali.


e)Tumia kitambaa safi na salama au taulo laini lililosafi na salama ili usipate matatizo ya michubuko usoni mwako, kitu kitakachopelekea kutokuwa na ngozi nzuri usoni.


f)Usipende kutumia kilevi cha aina yoyote na kama ni mtumiaji usitumie kupita kiasi, kwani itapunguza uzuri wa sura yako kwani ulevi siku zote ni mbaya hupunguza baadhi ya vitamins mwilini mwa mwanadamu.


g)Pia usipende kutumia sigara si nzuri kwa uboreshaji wa sura yako na afya yako kwa ujumla.


h)Jitahidi usiwe mtu wa kutoka toka sana usiku ili upate muda mrefu wa kupumzika na uzidi kuboresha na kuirutubisha ngozi ya uso wako na kuifanya ipendeze daima.


i)Pia unashauriwa kunywa maji, kula mboga za majani na matunda kwa wingi, na kwa kufanya hivyo utazidi kuonekana ni mwanamke mwenye sura safi, nyororo na iliyo na afya njema na yenye kuvutia daima machoni mwa jamii inayokuzunguka.


E-mail: meezy@youngmaster.co.tz
 
Hivi we si mwanaume?
Mbona unasema wapenda kujitunza tupe siri ya mafanikio?

Hapo ndipo wanaume tunapokosea na ndio maana tunapigwa vibuti na mademu zetu kila kukicha. Nina nani aliyesema kuwa mwanaume hapaswi kujitunza? Unadhani kuna mwanamke ambaye anapenda mwanaume asiyejitunza?
 
Hapo ndipo wanaume tunapokosea na ndio maana tunapigwa vibuti na mademu zetu kila kukicha. Nina nani aliyesema kuwa mwanaume hapaswi kujitunza? Unadhani kuna mwanamke ambaye anapenda mwanaume asiyejitunza?
kwa iyo unatunza sura ili usipigwe chini na demu wako? madogo wa siku izi bana tabu tupu?
 
Back
Top Bottom