Jinsi ya Kuscan Data - Kompyuta

Yona F. Maro

R I P
Nov 2, 2006
4,202
218
Jinsi ya Kuscan Data au Komputa .

Yona Fares Maro , May 2010
www.ictpub.blogspot.com

Utakachosoma hapo chini ni kwa ajili ya kujifunza , inawezekana hii taarifa isiweze kukudaidia wewe lakini ikasaidia mwingine na inawezekana unapojaribu kuscan vitu fulani vikafutwa au ukapatwa na mshituko mwingine - ni bora kuwasiliana na wataalamu kabla hujaamua baadhi ya vitu hapo chini

Kuscan ni nini ?

Kwenye ulimwengu wa programu za ulinzi kama antivirus ni ile hali ya programu yako kutafuta virus kwenye faili zilizo ndani ya computer au kwenye vifaa vingine ambavyo umeambia programu hiyo ifanye .

Lakini ni vizuri kujua kwamba Antivirus Nyingi na programu nyingi za masuala ya usalama wa computer na vifaa vyake huwa inascan saa zote na wakati wote ambapo computer hiyo inawaka .

Usisahau kwamba kuna programu zingine ndogondogo zinazoweza kuscan baadhi ya vitu vinavyochomekwa kwenye computer yako kama flash na HDD hizi huwa zinaangalia vitu vichache sana tofauti na antivirus au internet security na Firewall .

Kwanini unahitaji Kuscan ?

Kama Wewe ni mlinzi wa nyumba unatakiwa kuzunguka nyumba yako kujua usalama wa nyumba hiyo na kuweza kufukuza wezi na vibaka ambao wanaweza kuvamia nyumba hiyo muda wowote lakini tofauti ni moja --- Kwamba kwenye komputa mara nyingi mashambulizi yake ni kwa njia ya mawasiliano .

Tofauti ya Antivirus na Internet Security ni nini ?
Antivirus ni programu inayosaidia kupambana na kuondoa mashambulizi ya virus kwenye computer au vifaa vingine vinavyochomekwa au vya mawasiliano kama Simu kwa siku za karibuni wakati Internet Security inaweza kufanya vyote ambayo antivirus inaweza kufanya sema ina maongezeo mengine mfano baadhi ya Internet Security zina Firewall wakati Antivirus zake hazina ingawa hii haipo kwenye bidhaa zote inategemeana na Kampuni .

Kuna aina mbalimbali za kuscan .

1- Njia ya kwanza ni ile ya kwanza ambayo ni lazima kwa programu yako kuwekwa kwenye computer na iwe inascan saa zote kwaajili ya kulinda na kuondoa mashambulio yoyote ambayo unaweza kutokea kwenye computer na vifaa vyake .

2- Njia ya pili ni vile mtu anavyoamua kuanza kuscan komputa hiyo na vifaa vyake wakati hafanyi kazi mara nyingi mtindo huu ni mzuri kwa sababu utaweza kuscan vitu vyote kwenye computer kwa undani zaidi .

3- Njia ya tatu ni pale ambapo kifaa kwenye computer yako kama flashdisk , au external hdd imeshambuliwa na virus unapoamua kuichukuwa na kuichomeka computer iliyosalama kwa ajili ya kuiangalia virus na kuondoa matishio mengine .

4- Njia ya nne ambayo wengi hawaitumii ni pale computer yako inaposhindwa kufanya kazi kwenye hali ya kawaida sasa unawasha kwenye safemode ndio uanze kutafuta virus na kuondoa virus au matishio hayo . lakini unatakiwa ukumbuke sio antivirus zote zinafanya kazi kwenye safemode ni chache sana zinazoweza kufanya kazi kwenye safemode .

5- Tano ni kuscan computer hiyo kwa njia ya boot inaitwa Bootscan ni pale ambapo komputa yako inapowaka tu ndio ianze kuscan hapo hapo kabla haijawa moja kwa moja hii ni njia nzuri sana haswa kwa kuondoa virus waliojificha ( Hidden ) kwa hili kuna aina chache za antivirus zinazoweza kufanya hivyo .

6- Njia nyingine ni ile ya kuscan file na folder kwa njia ya mtandao ndani ya office moja ambayo ina computer nyingi zilizounganishwa pamoja au zile ambazo ziko sehemu mbalimbali duniani lakini zinaangaliwa toka sehemu moja kwa matatizo au shuguli kadhaa , Hii njia ya mwisho ni nzuri sana kwa sababu inapunguza gharama za vifaa na programu zingine za masuala ya ulinzi na hata wafanyakazi wanaweza kuwa wachache tu .

Hizo ni njia kadhaa mtu anazoweza kutumia kuscan komputa na vifaa vyake taarifa zingine na maelezo unaweza kutafuta kwa njia ya mtandao kutokana na bidhaa mbalimbali za masuala ya ulinzi na usalama zinavyotoka au zile zilizokwepo kuendelea kuimarishwa zaidi .

Na mwisho ni kwa mtu kujua kwamba sikuhizi kuna matishio mbalimbali yanayoweza kuharibu computer yako na taarifa zako zingine zilizohifadhiwa kwahiyo ulinzi wa computer yako na programu zake ni kitu muhimu sana , suala la kuupdate programu za computer yako pamoja na antivirus ni kitu muhimu sana .

Bila kusahau watu kujenga mazoea ya kununua au kupata programu ambazo ni halali sio za bandia kama wengi wetu tunavyozoea unavyonunua programu bandia tena kwa kujua kabisa unahatarisha usalama wa computer yako na vile vilivyomo ndani .

Yona Fares Maro , May 2010
www.ictpub.blogspot.com
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom